Nchi iliharibiwa na CCM haiwezi kujengwa na CCM

Umeongea kwa uchungu mdogo wangu pole sana,mtu aliyetumia bilioni nane kununua Kivuko kibovu na kukibinafsisha jeshini mradi tusihoji ataweza kumchukulia hatua anayemiliki mali alizopewa na mwekezaji 'GSM' bila kufanya utafiti kwanini apewe.

Leo vita ya watu wawili ianitwa vita ya kitaifa ya MADAWA.Kwa sasa tumekwisha kabisa.
Sielewi ni kwanini , lakini baada ya kusoma andiko lako nimepata ujasiri mkubwa sana !
 
TUNAPIGA HATUA 2 MBELE TUNARUD HATUA 10 NYUMA
CCM WAMEHARIBU SANA HII NCHI. HAWA WAKOLON WEUSI UTAFIKA TU MWISHO WAO.
Uzuri wanaoishabikia na wana chama wa sisiem akili zao ni ndogo hata elimu ya kuchanganua mambo hawana.
Wachache sana wenye akili na wanaojitambua km mm na mtoa uzi.
"Hii nchi imeharibiwa na ccm na haiwezi kujengwa na ccm''
 
Yes, si ulimwona hadi Mwakyembe alikuwa naye?

Mimi siyo mpiga ramli. Upiga ramli nakuachia wewe.

umenielewa sanaaaa.....

na slaa aliondoka na watu, sijui nao walinunuliwa?
 
Acha uongo wewe! Kama CCM haikujiweka hapo kwanini iliichakachua rasimu ya Warioba iliyoandikwa na wajumbe wengi toka CCM!? Kwanini inaogopa Tume huru ya uchaguzi na kung'ang'ania kitengo chao cha wizi wa kura na chaguzi!? Uongo wako peleka lumumba siyo humu.

nchi inaanziwa kujengewa nyumbani kwako sio kwenye vyama vya siasa.
wananchi kwa akili zao tumamu walitoka majumbani mwao kwenda kuiweka CCM hapo ilipo, CCM haikujiweka mkuu.
 
visingizio vyenye muundo malalamiko. kuuita uongo ni mtazamo wako ambao sio lazima uwe sahihi.
Ile ni rasimu au mapendekezo ambayo yalipaswa kujadiliwa kwa kina. Sasa mkakimbia na kususa kisha baadae kidogo mkaanza tena kusalitiana wenyewe kwa wenyewe ikionyesha hamkuwa na nia endelevu, kukaibuka ukawa na CCM hiyo lawama ni kwa wote maana hakukua na maslahi ya wananchi bali siasa ziliibuka. Chanzo cha tatizo ni kutowabana walioshiriki wote UKAWA na CCM kugombea uchaguzi uliokuwa unafuata ili kuwa na mawazo huru.

Tangu Siasa Za vyama vingi zimeanza, Hasa Uchaguzi uliopita sijawahi kuona Ushahidi wowote kuwa CCM wameiba kura za NEC zaidi ya tuhuma nyepesi za kutafuta huruma za wananchi kama excuse ya kushindwa.
 
Utawahi kuona wapi wizi wa kura na wewe ni mnufaika wa wahuni wa MACCM. Mabilioni yalitumika na Kikwete akawajaza MACCM katika tume ile kwa kujua wataandika rasimu ambayo MACCM wataipenda. Na timu ikasheheni Mawaziri Wakuu wawili ambao wote hjawakuwa na sifa ya ufisadi akina SAS na Warioba na wajumbe wengi wengine ambao waliwahi kushika nyadhifa mbali mbali Serikalini.

Wajumbe wale wakaamua kuweka mbele maslahi ya nchi na hivyo kutusikiliza Watanzania tunataka nini kwenye katiba. Na wakaja na rasimu nzuri sana, lakini wahuni wa MACCM walivyoona kiama chao cha kung'ang'ania madaraka kimefikia kiama wakaamua kuichakachua rasimu ile.

Kama CCM inajiamini basi iruhusu katiba ya rasimu ya Warioba, iruhusu tume huru ya uchaguzi nchini. Halafu uchaguzi wa haki na huru tuone kama Watanzani hatujaizika CCM milele. Watanzania wawachague kwa lipi hasa mlilolifanya ndani ya miaka 55!? Nchi tajiri sana lakini hakuna hata kitu kimoja chetu ambacho tunaweza tukasema hiki Watanzania tunajivunia . Si elimu, afya, huduma muhimu, usafiri, uchumi ni shakalabaghala tu mbele kwa mbele.

Kwa akili yako finyu na uwezo mdogo wa kutoona mbali zaidi ya ilipo pua yako utakuja na kauli kama hiyo ya excuse ya kushindwa.

sawa ya katiba tutafanya marudio ya Mijadala kitu ambacho ni upotevu wa rasilimali Muda maana hata hiyo ya warioba Inamaswali na mapungufu lukuki ukiiangalia bila jicho la kishabiki, japo mazuri nayo yapo mengi.
Ila kwa uzoefu mdogo huwa mna antagonistic excuses katika kila kushindwa. Kama sio TUME HAIKO HURU, MTAKIMBILIA TUMEIBIWA BILA USHAHIDI IKISHINDIKANA KABISA NA MKAONA HAKUNA PA KUTOKEA, MNAANZA KULAANI WAPIGA KURA KUWA NI WATU WASIOJITAMBUA NA ACHA WAISOME NAMBA.

Kuhusu CCM, CCP ilizaliwa 1921 lakini maendeleo halisi yalitokea 1978 china baada ya mabadiliko makubwa ya kisera na kifikra ndani ya chama. Haiihitaji Upinzani usioeleweka kuleta mabadiliko nchini bali Mtu akiwa popote pale, mwenye uwezo nia na team sahihi. Usilete ule uchwara wa EL, pale mkuu palikuwa ni usanii mtupu mjipange mtafute mtu sahihi, muache kufumba macho mchana na kusema tanzania yote ni giza. Wananchi hawawaelewi huo ndio ukweli mwororo.

siku njema.
 
Ni mwenye akili finyu tu anaweza kuandika upuuzi kama huu ulioandika hapa kwamba katiba mpya ni upotevu wa rasilimali. Rasilimali ngapi za nchi ambazo zimepotea chini ya wahuni wa MACCM tangu kuanzia Mwinyi na Mafisadi wengine wote baada yake na hakuna hata mmoja ambaye alipandishwa hata kizimbani. Matrilioni ya pesa za Watanzania yamekwapuliwa na wahuni mbali mbali ndani ya chama chenu. Kama mngekuwa mnajali upotevu wa rasilimali za Watanzania wahuni wote hawa wangekuwa lupango sasa hivi tena kifungo cha muda mrefu. EPA, IPTL, MV DAR, RICHMOND, ESCROW, na madudu mengine chungu nzima.

Hebu acha kuandika upuuzi wako wewe mnufaika wa ufisadi.

Mimi nafikiri Nchi itajengwa kwa kurudisha mfumo wa elimu wenye kumjali mwl, hii maana yake ni katika utoaji bora wa elimu na si huu wa waliofail kujiunga sekondari.
 
Ni mwenye akili finyu tu anaweza kuandika upuuzi kama huu ulioandika hapa kwamba katiba mpya ni upotevu wa rasilimali. Rasilimali ngapi za nchi ambazo zimepotea chini ya wahuni wa MACCM tangu kuanzia Mwinyi na Mafisadi wengine wote baada yake na hakuna hata mmoja ambaye alipandishwa hata kizimbani. Matrilioni ya pesa za Watanzania yamekwapuliwa na wahuni mbali mbali ndani ya chama chenu. Kama mngekuwa mnajali upotevu wa rasilimali za Watanzania wahuni wote hawa wangekuwa lupango sasa hivi tena kifungo cha muda mrefu. EPA, IPTL, MV DAR, RICHMOND, ESCROW, na madudu mengine chungu nzima.

Hebu acha kuandika upuuzi wako wewe mnufaika wa ufisadi.
soma taratibu ujibu kwa uelewa wa kilichoandikwa, Relax
sawa ya katiba tutafanya marudio ya Mijadala kitu ambacho ni upotevu wa rasilimali Muda
mimi na wewe kujadili Rasimu ya warioba leo, wakati mengi yamejadiliwa wakati wake ni vain repetition. sasa kama unaamini Katiba ile ni bora mno Piga kelele, Kama unaamini Iliyoundwa baadae, Piga kelele pia. Ile iliyoundwa na ya warioba nakubaliana nayo ila naamini inamapungufu makubwa na haikufaa kupitishwa moja kwa moja. Mijadala hii itafaa siku suala la katiba likiibuliwa tena. Lakini kwa sasa,

1: Katiba Bora ni ya Muhimu sana kwa Taifa.
2: Ninakubaliana na Tume ya Warioba lakini pia nakubali kuwa Rasimu ilikuwa na mapungufu mengi mno yenye kuhitaji Umakini mkubwa kuliko ule wa bunge la katiba.

3: Sikubaliani na Mfumo mzima wa Bunge la katiba na huo ndio chanzo cha malalamiko yako na sio kwa sababu wengi wanasadikika kuwa CCM bali Walipaswa kuwekewa masharti magumu mno yatakayowafunga kisiasa kwa zaidi ya miaka hata kumi. Hapo naamini CDM wote na CCM wengi wangekimbia hiyo sacrifice maana siasa wengine ndio ugali. Hivyo Vacancy ingejazwa na watu sahihi.

Kuhusu Tuhuma za Ufisadi zilizopita, kila chama kina mapungufu makubwa sana tukijadili ya chadema na uongozi wake tu, Unaweza kurusha hata SOFTNGUMI kupitia keyboard. Ya CCM yanamadhara makubwa kwa sababu keki tamaniwa iko mikononi mwake miaka mingi. Kama chama chochote duniani na Chenyewe kinapitia katika masahihisho angalau kuzuia leakages nyingine kama hizo kwa faida ya wananchi. Hakuna kwenye andiko lolote la CCM watu wanaambiwa Waibe, wawe mafisadi, na orodha uliyoitoa. Ni kama yale yale tu yaliyotokea Mbinguni. Kiumbe msafi rucifer akageuka kuwa Shetani na kutia hasara Mbingu haiifanyi mbingu kuwa Haifai bali Itafanya mabadiliko ili asitokee Shetani mwingine.
 
walioharibu nchi washahamia chadema. walikuwa watendaji wakuu wa serikali more specific pm`s. hata wenye ccm ya zamani waliokuwa drawing board nao wako chadema more specific kingunge. wenyeviti wa mikoa kibao waliokuwa ccm ya zamani wako chadema, tuseme hivi chadema=ccm ya zamani. ccm Mpya ilizaliwa upya na kubatizwa kwa moto na ndo itarekebisha uharibifu wa ccm ya zama I(chadema)
Wezi wa escrow,rada,mikataba ya madini,mabehewa feki,m.v.bagamoyo,nyumba za Siri Kali kuporwa,mikopo elimu ya juu,ujangili,tokomeza mifugo,samaki wa wachina na upuuzi mwingine ni Lowassa!, kivipi au uko kazini kufunika kombe na kupiga kampeni?
Ysonekana in mmoja wa wanufaikaji wa uozo huu!Huyu atakuwa ndugu yako!
2eff159ffdf9d88b2567869b41f6c49f.jpg
 
nchi inaanziwa kujengewa nyumbani kwako sio kwenye vyama vya siasa.
wananchi kwa akili zao tumamu walitoka majumbani mwao kwenda kuiweka CCM hapo ilipo, CCM haikujiweka mkuu.
Haikujiweka lakini imegeuka king'ang'anizi
 
Back
Top Bottom