Nchi iliharibiwa na CCM haiwezi kujengwa na CCM

H.T.P

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,169
1,298
Ni kweli watanzania tunadharaulika sana duniani kote kwasababu ya kuishi maisha mnyama kondoo.

Kondoo sio mnyama muoga kama watu wanavyodhani hapana, ila hata anapojua anaenda machinjoni kwasababu ya uvumilivu wake, huwa hasumbui anaenda tu na kisu kikipita shingoni wala hapigi kelele hunyamaza hadi kufa.

Hii nchi imeliwa na tangu Uhuru mpaka Leo, na hawa kwasababu wanamuelewa mtanzania kama kondoo, wamekua wakibadilishana lijiti kila iitwapo Leo wakitumia mbinu tofautitofauti lakini ni walewale.

We kama huyu tuliyenaye kweli ni mtetezi Wa wanyonge? Sikia haya;

Asiyeweza kulipa ada ya shiringi 200 apige mbizi kama samaki,

Hii bukoba kila majanga nyie tu, ukimwi nyie, matetemeko nyie,
Kama mnategemea msaada Wa serikali mwafaa!!

Sitaki kuyataja yote nisiwavuruge watu, hoja yangu ni kwamba, ndani ya CCM hakuna Mwenye nia wala hatakuwepo walikomboa taifa hill, kwasababu;
Wote wameshiriki kuliharibu hivyo wanalindana, wale waliokataa uovu wao waliwafukuza, hebu jiulize swali!

Hivi MTU aliyehonga kimada Nyumba za serikali, anaweza kumwajibisha MTU aliyenunua mabehewa feki?

Wewe mtu anatolewa mifano hai kabisa kwamba, huyu mkuu Wa mkoa ni muhujumu uchumi, alafu bila kufanya tafiti yoyote anasema msimchafue!! Ah mi nakasirika sana acha niachie hapa,, endeleeni wengine mnaoona kama ninavyoona mimi
 
Umeongea kwa uchungu mdogo wangu pole sana,mtu aliyetumia bilioni nane kununua Kivuko kibovu na kukibinafsisha jeshini mradi tusihoji ataweza kumchukulia hatua anayemiliki mali alizopewa na mwekezaji 'GSM' bila kufanya utafiti kwanini apewe.

Leo vita ya watu wawili ianitwa vita ya kitaifa ya MADAWA.Kwa sasa tumekwisha kabisa.
 
walioharibu nchi washahamia chadema. walikuwa watendaji wakuu wa serikali more specific pm`s. hata wenye ccm ya zamani waliokuwa drawing board nao wako chadema more specific kingunge. wenyeviti wa mikoa kibao waliokuwa ccm ya zamani wako chadema, tuseme hivi chadema=ccm ya zamani. ccm Mpya ilizaliwa upya na kubatizwa kwa moto na ndo itarekebisha uharibifu wa ccm ya zama I(chadema)
 
Ni kweli watanzania tunadharaulika sana duniani kote kwasababu ya kuishi maisha mnyama kondoo.

Kondoo sio mnyama muoga kama watu wanavyodhani hapana, ila hata anapojua anaenda machinjoni kwasababu ya uvumilivu wake, huwa hasumbui anaenda tu na kisu kikipita shingoni wala hapigi kelele hunyamaza hadi kufa.

Hii nchi imeliwa na mbwa mwitu tangu Uhuru mpaka Leo, na hawa mbwa mwitu kwasababu wanamuelewa mtanzania kama kondoo, wamekua wakibadilishana lijiti kila iitwapo Leo wakitumia mbinu tofautitofauti lakini ni walewale.

We kama huyu tuliyenaye kweli ni mtetezi Wa wanyonge? Sikia haya;

Asiyeweza kulipa ada ya shiringi 200 apige mbizi kama samaki,

Hii bukoba kila majanga nyie tu, ukimwi nyie, matetemeko nyie,
Kama mnategemea msaada Wa serikali mwafaa!!

Sitaki kuyataja yote nisiwavuruge watu, hoja yangu ni kwamba, ndani ya CCM hakuna Mwenye nia wala hatakuwepo walikomboa taifa hill, kwasababu;
Wote wameshiriki kuliharibu hivyo wanalindana, wale waliokataa uovu wao waliwafukuza, hebu jiulize swali!

Hivi MTU aliyehonga kimada Nyumba za serikali, anaweza kumwajibisha MTU aliyenunua mabehewa feki?

Wewe mtu anatolewa mifano hai kabisa kwamba, huyu mkuu Wa mkoa ni muhujumu uchumi, alafu bila kufanya tafiti yoyote anasema msimchafue!! Ah mi nakasirika sana acha niachie hapa,, endeleeni wengine mnaoona kama ninavyoona mimi

Sahihi sana mkuu

Tatizo ni mbadala au huyo anayetarajiwa kujenga hii nchi

I strongly believe chadema ya slaa na zitto ndio ingekuwa nzuri kabisa kujenga nchi, kuliko ya Lowassa....ambaye katoka CCM

Hapo ndio tatizo..tena kubwa
 
walioharibu nchi washahamia chadema. walikuwa watendaji wakuu wa serikali more specific pm`s. hata wenye ccm ya zamani waliokuwa drawing board nao wako chadema more specific kingunge. wenyeviti wa mikoa kibao waliokuwa ccm ya zamani wako chadema, tuseme hivi chadema=ccm ya zamani. ccm Mpya ilizaliwa upya na kubatizwa kwa moto na ndo itarekebisha uharibifu wa ccm ya zama I(chadema)
Hauitaji cheti kilichogongwa muhuli wa moto au cheti kutoka milembe kudhibitisha kama wew..............
 
I strongly believe chadema ya slaa na zitto ndio ingekuwa nzuri kabisa kujenga nchi, kuliko ya Lowassa....ambaye katoka CCM
Nakubaliana nawe juu ya Lowasa. Lakini siyo juu ya Slaa. Slaa huyu huyu aliyekubali kutumika na CCM wakati wa uchaguzi?!? Huyo siyo mwanamageuzi wa kweli; kwa kukorofishana na chama chake cha zamani, angekaa zake kimya na kujiondoa kwa staha na heshima. Lakini kwa alivyotumika, sisi tuliomwaminia, tulimtoa maana kabisa.
 
alitumikaje mkuu? au kuonyesha yuko against na lowasa automatically aliwekwa upande wa ccm?
 
walioharibu nchi washahamia chadema. walikuwa watendaji wakuu wa serikali more specific pm`s. hata wenye ccm ya zamani waliokuwa drawing board nao wako chadema more specific kingunge. wenyeviti wa mikoa kibao waliokuwa ccm ya zamani wako chadema, tuseme hivi chadema=ccm ya zamani. ccm Mpya ilizaliwa upya na kubatizwa kwa moto na ndo itarekebisha uharibifu wa ccm ya zama I(chadema)

kuna mmoja kawa waziri mkuu miaka kumi

mwingine kawa waziri na mbunge miaka kama 20

na katumika chama kile miaka 30!
 
  • Thanks
Reactions: mmh
acha ujinga wewe........kwahiyo hii nchi iongozwe na jeshi......ni bora useme unatamani baba yako akachukue fomu agombee urais lakini sio upumbavu unaosema.
Umejuaje je kama baba angu ndio mkuu wa majeshi??

Bora jeshi lichukue nchi tujue moja kuliko huu usanii unaoendelea!
 
Mtu wanchi wakuonyesha mabango yanayoontesha kuwa mahindi yamekauka kabla ya kuzaa, wewe unawaambia mkivuna uzeni bila kuingiliwa na watu kutoka serikalini!!!!!hii ni aibu gani jamani
 
ıtajengwa na wananchi wenyewe hakuna chama cha siasa kinachoweza kujenga nchi wakati vimejaa walafi wa madaraka na wezi wa fedha za umma

Hao wananchi wataongozwa kutoka sayari ya jupita? au wanahitaji viongozi ambao ni wanasiasa kuwaongoza??
 
Ben carson "unataraji mwanasiasa atatue matatizo yako wakati yeye ndo alioyatengeneza" .
Tusitarajie kutoka kwao wenyewe ni kama lowasa fisadi na mbowe mkwepa kodi ukenda chama dume ndo madudu hiyo ni ndoto
 
Ni kweli mbinu za kuikomboa nchi kiuchumi na kifikra hazionekani ndani ya ccm kwani bora elimu bado inaendelea,bora kilimo bado inaendelea,mifumo mibovu ya utawala yaani utawala wa kutegemea utashi wa raisi bado unaendelea,elimu ya veta bado si kipaumbele,malipo mazuri kwa wanasiasa badala ya wataalamu kiasi cha kusababisha wataalam kukimbilia siasa na kuacha nchi bila wataalam waliobobea ktk sekta maalum za maendeleo haya mambo bado yanaendelea.Hivyo hakuna jipya kuelekea nchi ya viwanda kwa sababu ccm ni ileilena mbinu zinazotumika ni zilezile na wenye mamlaka ni walewale na wananchi ni walewale waliojazwa unga wa ndwele
 
tunachosubiri sisi kina gogo la shamba ni kuambiwa tumepata faida kiasi gani baada ya mwaka mmoa kununua ndenge mpya mbili
 
Back
Top Bottom