Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Mkuu kwanza pole sana kwa hali unayokutana mimi pia ilinikuta 2018.

Nakushauri punguza ekari za kulima ili uzihudumie vizuri na upate magunia mengi hizo ekari 20 ulitakiwa uwe na gunia 400+ mpaka 500.

Lima ekari kumi zihudumie vizuri kwa huduma ya ekari 15. hizo utapata gunia 200+ hivyo utakuwa umepunguza gharama za uzalishaji na kupata mavuno mengi.

Kuhusu soko nchi hii sasa hivi soko la nafaka liko chini sana mimi nina gunia zangu za mpunga lakini kwa bei iliyopo niko tayari kuzifungia ndani mpaka mwakani.
Niuzie hizo gunia za mpunga maana siyo leo wala kesho mpunga utapanda bei mkuu ..nitakupa 30k kwa kila gunia chukua hela hiyo nataka gunia 200
 
Niuzie hizo gunia za mpunga maana siyo leo wala kesho mpunga utapanda bei mkuu ..nitakupa 30k kwa kila gunia chukua hela hiyo nataka gunia 200
30k hapana siwezi kuuza kama hazitapanda bei nitasubiri mwakani nikilima nikipata zingine probably zitakuwa umepanda bei na mimi nitakuwa nao mwingi.
 
Mafuta ya kula yakipanda bei ni fursa kwako mkulima. Sasa lima alizeti upige pesa. Kuhusu mahindi NFRA wamepewa pesa wayanunue. Tafuta vituo vyao ukauze.
Unayakumbuka mabilioni ya pesa kwa ajili ya vijana mikoani yaliyotolewa enzi za awamu ya nne!?
 
Biashara na ufugaji
Mkuu sekta ya biashara haijakaa vizuri, kuna kodi ambazo hazina msingi wake, hizo kwa kiwango kikumbwa ndizo zilizozalusha wamachinga wengi ambao kwa sasa ndio tishio la watawala. Ufugaji ni shughuli pevu, ni lazima uwe na eneo lako, jambo ambalo ni ngumu. Aidha migogoro ya wakulima na wafugaji bado haijapatiwa ufumbuzi. Ni kazi kwelikweli.
 
Pole Sana lakini kumbuka usifanye kilimo Cha kibiashara kama unategemea mvua .Nakushauli uwe unanunua mazao kwa wakulima faida ipo kubwa Sana.
Mkuu ushauri wako ni mzuri sana, tatizo mtaji. WaTZ wengi hatuna mitaji ya uhakika. Unaweza ukaanza na akiba kidogo uliyonayo kwa bahati mbaya mtaji ukakata hapo ndio basi tena.
 
kasanga70
Nimeona concern yako kwenye bandiko lako. I myself at your place, could possibly have argued along that same line. However, you would better hope for the better, if not the best. Just try maintaining a very positive outlook so that you ought see several future miraculous possibilities God has in store for you
Rais wa nchi kutwaliwa na Bwana si jambo dogo, ni kubwa muno, na hasa linapokuwa kama first experience kwa nchi husika kama iambavyo limekuwa kwa nchi yetu
Mimi ni muumini wa dini ya kikiristo, naamini sana katika matendo makubwa ya Mungu. Mungu ameridhia kumchukua Rais aliyetupatia mara ya kwanza na akaamua kuweka mwingine yeye mwenyewe. Kumbuka kuwa hajakushirikisha kwenye mchakato wa kumchukua aliyekuwepo, alimchukua tu halafu ndiyo akakushirikisha sasa kumpata huyu aliyepo kwa kutumia kitu kinachoitwa Katiba. Kwa hiyo Mungu bado yuko pamoja na sisi kwa kiwango kikubwa mno na cha ajabu muno. tuendelee kumuombea mama atafanya makubwa. Sasa hivi ni mapema mno, bado tuko kwenye ile after-shock ya kuondokewa na Rais wetu mpendwa
Kwenye ulimwengu wa roho, hii nchi iko hivi, huwa inakuwa several times, twisted na mwovu Ibilisi kuelekea kwenye negative edge na inapokuwa imetokea hivyo, kwa kipindi fulani huwa inaonyesha kukubali kabisa kuelekea kwenye upande huo, halafu tena ALL OF A SUDDEN baada ya hapo, inakuja restore back quickly kuelekea kwenye POSITIVE edge.Believe me! Tanzania iko hivyo kwenye ulimwengu wa roho
Kwenda zako huko. Mungu hawezi kuweka ma-rais wauaji (aliyefariki) na goigoi (aliyepo). Hawa marais wamepatikani kwa kutumia madhaifu makubwa ya kibinadamu tuliyonayo.
 
Nikifunga kiwanda cha kusaga sembe songea mfano kuleta dar, ili kuleta unga dar natakiwa niwe na risiti ya efd ambapo kila kiroba tra watakula si chini ya 3000 kww point kuwa unga umeuzwa hata kama bado sijauza, ila nikisafirisha mahindi toka songea kuja dar ntalipia ushuru wa halmashauri 1000 kwa kila mfuko wa kg 100. Kwa semitrailer la viroba 300 ntalipia 300000 kama ushuru tu. LAkini nikisafirisha unga kama naenda kuuza bei ya 17000 ntalazimika ntaingia gharama ya almost 3600000 kabla hata sijajua bei kama itapanda au kushuka.
Serikali inaua kila kitu kwa mikodi isiyo na maana kama hii, tumekuwa watumwa na maskini kwa sheria zetu wenyewe inabidi wenye akili wapigane kuziondoa, jaribu kuweka investment kwenye storage/maghala ya kisasa, unanunua wakati bei ipo chini unayatoa yakiwa juu labda itasaidia
 
Mkuu sekta ya biashara haijakaa vizuri, kuna kodi ambazo hazina msingi wake, hizo kwa kiwango kikumbwa ndizo zilizozalusha wamachinga wengi ambao kwa sasa ndio tishio la watawala. Ufugaji ni shughuli pevu, ni lazima uwe na eneo lako, jambo ambalo ni ngumu. Aidha migogoro ya wakulima na wafugaji bado haijapatiwa ufumbuzi. Ni kazi kwelikweli.
Bora biashara
 
Kuna kitu kinakula moyo wangu I finally must vent out.

1. Nimevuna gunia 200 baada ya kulima ekari 20 za mahindi nataka kupeleka sokoni bei ya gunia tshs elfu 30, so nitapata million sita nikiuza yote. Kweli jamani this is too much. The leadership is seriously imposing new tax? Mnashindwa kuadress market challenges kwa watu million 45 walioko Shamba? Really?

2. Kuna influx ya vyuo Vya afya now than ever before. Ni mwendo Wa lab technician's, nursing, pharmacy, medical assistance courses etc. Nimeproject in 5 years to come tutakuwa na mrundikano Wa wataalamu Wa afya kuliko kawaida watakaokuwa hawaajiliki. Utapeli utaanza, kila chumba kitakuwa hospital bubu, madawa kuuzwa ovyo nk hii imeshaanza njmeiona somewhere. Afya zetu zitakuwa rehani. Ni kama hakuna sekta nyingine za kutrain serikali na taasisi binafsi zote ziko huko now. Sioni influx ya trainee kwenye lead productive sectors.

3. Ajira hakuna, kila mtu sasa analima masoko hakuna, mbinu za kujenga uchumi unaokuwa sizioni serious. Kuna ahadi tu za kuendelea kujengewa majengo mengi ya huduma mbalimbali za serikali bila kujenga watu Vya kutosha.

4. Nikirudi kwenye mfumuko Wa bei bei za mafuta, visavis gharama za uzalishaji wa mazao tozo barabarani usumbufu wa wakaguzi mazao, matrafiki, nk nk naishiwa hamu kabisa.

5. Ukiwaangalia viongozi concentration haipo kudeal na 80 % ya walipo watz inadeal na vitu very Petty.....

6. Upigaji umerudi kwa kasi ya ajabu. Sasa hivi kila ofisi ya umma hasa hizi nyeti zisizokwepeka deal zinapigwa balaa

My question is....watoto wetu wataikuta Tanzania ya namna gani sijui.

Jamani eeeh sijui kama hii tabu naipata Mimi tu. Kuna majibu hapa

Its soo frustrating.
Hili swali lako ndo kinachonifanya na mi nijiulize!
 
Back
Top Bottom