Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

No body cares.....yaani ukimuuliza mtu anaejua kilimo. Kulima ekari 20 is not a joke.......gharama tu zilizotumika hadi unapata mazao nimechoka guys,...
Mkuu uko mkoa gani?mahindi yameshapanda bei sasa manyara ni 45 mpka 50 elfu...kma unaweza kuvumilia mpka mwezi dec utauza kwa bei nzuri fungia mzigo ghalani
 
Magu alikua mpigaji hakuna mfano wake,sgr,bwawa la umeme,daraja busisi,kununua madege yasiokua na kazi...yani ufisadi wake ni trilioni za kutosha....uliona wapi miradi inapitishwa na rais bila bunge,wakandarasi katafuta yeye mwenyeweccm wote majambazi sugu
bwawa la umeme ni la nyumbani kwake
 
Mkuu 'misasa', tunazunguka tuuu na maneno mengi lakini nadhani sote tunajua tatizo lilipo.

Tatizo lipo huko huko kwenye hiyo serikali unayosema "ina mkono mrefu", lakini haina uwezo wa kuutumia mkono huo mrefu kwa manufaa ya wananchi wake.

Tatizo ni nini? UZEMBE.

Nchi hii hata kutafuta na kuweka takwimu sahihi tu ni shida tupu!
Serikali katika hali ya kawaida kabisa ingeweza kuwa na uwezo wa kujua kiasi cha mazao yanayotegemewa kuzalishwa katika msimu fulani, kabla hata mazao hayajavunwa.
Serikali inao uwezo wa kupata taarifa za masoko duniani kote kabla ya mazao hayajavunwa; na kujua ni nchi gani zitakuwa na uhitaji mkubwa wa mazao hayo, kabla ya msimu wa mazao husika. Hii siyo kazi ya kubahatisha unayoanza kuifanya wakati tayari mazao ya wakulima yakiwa ghalani!

Serikali ina uwezo wa kujenga maghala ya kuhifadhia mazao ya ziada ili kama soko hali siyo nzuri mazao ya wakulima yahifadhiwe, yasiharibike ili soko likipatikana yauzwe.

Serikali ina uwezo kabisa wa kufanya mipango ya kuwakaribisha wawekezaji ili kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa kwa ziada. Mfano. Mahindi siyo chakula cha binaadam pekee. Mahindi yanatoa mafuta ya kula, nasi hapa tunao uhaba mkubwa wa mafuta ya kula, mbona hatutumii mahindi kutuzalishia bidhaa hiyo?
Mahindi yanatengeneza "ethanol' inayoweza kuchanganywa kwenye petroli ili tupunguze gharama za uagizaji wa mafuta, n.k., nk..
Kama kuna malighafi ya kutosha na ya kuaminika (mahindi) itashindikana vipi kuwapata wawekezaji wa kuitumia malighafi hii?

Hebu angalia, kuna wakati ilipigwa kelele nyingi kuhusu zao la mihogo na utengenezaji wa wanga. Kiwanda kikajengwa, nadhani Ruangwa kwa Majaliwa. Wakulima wa mihogo nao sijui ilikuwaje, kiwanda kikasuasua hadi leo hakisikiki

Serikali, kama ulivyosema, ina wajibu wa kuyasimamia mambo haya, si swala tu la kuyapigia kelele kwa msimu na kuyaacha yafe!

TATIZO LIPO SERIKALINI, SIYO KWA WAKULIMA.
Asante sana na umemaliza kila kitu na naunga mkono mkuu.

Serikali inawajibu na haiwezi kukwepa kuhusu wakulima kukosa soko la mazao hususani wa mahindi.

Kitu kingine wananchi hatuna meno kuwajibisha viongozi wazembe wanaoshindwa kutatua matatizo yetu,wananchi tumekuwa wasikilizaji na watendaji kila tunachoamuliwa na viongozi wetu.

Na ulichosema wange create database ya kutambua idadi ya mazao yatakayo vunwa msimu mzima na kutambua masoko yanapatikana wapi yasingetokea haya.

Najuuliza kazi za maafisa masoko wa halmashauri au manispaa ni zipi? maafisa kilimo pia na hawa so called TANTRADE au mazao mchanganyiko majukumu yao ni yapi?
 
Tatizo inawezekana unabishana ila unakuta hujawahi kodisha hata Fuso wewe ukaweka mafuta na kumlipa dereva. Ujuaji mwingiii na kuilaumu serikali wakati wao wameshiba na mishahara minono. Amka, hii nchi ina mpaka usafiri wa bure as long as mzigo ulio nao una faida na unao mzigo wa kutosha.
Usafir wa bure??
 
Pole Sana lakini kumbuka usifanye kilimo Cha kibiashara kama unategemea mvua .Nakushauli uwe unanunua mazao kwa wakulima faida ipo kubwa Sana.
 
Mbowe anajua faida ya siasa inakuja kipindi kwa kipindi. Jaribu kufikiria sera ya kubadilisha gia angani ambayo ilibuniwa na kuasisiwa na cdm. Wamevunja rekodi hamna kitu kama hicho popote duniani.
Pia kiliwashushia heshima sana
 
Naelewa yanayokukuta na pole na mapambano.....

Hizo gunia chache sana, lazima uumie na usafiri maana huwezi hata tangaza tenda na kampuni za logistic na ufinyu wako wa elimu na connection kujua wapi upeleke mahindi.

Unatakiwa kujua kuwa wakati nchi inasema usitoe mahindi nje kuna wenzako wanajua namna ya kuyauza.... wewe unawatajirisha wao kwa kuwapa kwa bei nzuriiii ya faida. Sasa utafute hiyo elimu na ongeza production.
Songea Nina gunia 870 ila pia kuna jamaa ka 3 nawafahamu wamekwama soko SASA mzee wa connection unatusaidiaje!??
 
Mbowe anajua faida ya siasa inakuja kipindi kwa kipindi. Jaribu kufikiria sera ya kubadilisha gia angani ambayo ilibuniwa na kuasisiwa na cdm. Wamevunja rekodi hamna kitu kama hicho popote duniani.
Na light bwana yule angelishinda 2015, hakuna wa kumcontrol hata mumoja ambaye angeliweza kumzuia.
 
Kilimo cha mahindi hakijawahi kuwa na tija na faida ya kuaminika kwa mkulima

Huu ni ukweli mchungu bora hata maharage bei zake zipo stable.

Ifike mahali tukubali mahindi na mpunga ni mazao ya kulima ili kupata chakula tu

Mpunga unalima eka ili hiyo eka ikupe walau faida ya laki 8 ni lazima kuanzia kupanda kuvuna kuweka store utamaliza mwaka ndo upate hiyo 800k km faida.

Lakini kuna mazao ya kawaida kabisa yasiyo na stress km bamia tu unaweza kupata pesa nzuri sana kwa mda mfupi sana bila stress

Hivyo hivyo kwa mahindi saivi debe 4000 mahali nilipo tukizungumzia mbolea tunazungumzia 80000-120000 yaani uuze debe 20-30 kupata mfuko mmoja wa mbolea.

Mazao hayo ni ya kulima eka nyingi sana walau upate faida.

Tuache kulima kimazoea.Kuhusu huyu mama mi ndo simuelewi kabisaaaaaaa
Upo sawa mkuu, niliwaza kufunga machine ya kukoboa na kusaga mahindi, lakini nikashituka nikaenda kwa Ya mpunga.
 
Si mama yenu alienda mkasema karudisha mahusiano? Mpaka akili itawakaa nchi sio nyumbani kwako! Urafiki na kenya ni unafiki tu! Hakuna urafiki hapo ila watu mapimbi ndo huwa wanaaminishwa hivyo!
Unafiki kwenye diplomasia unalipa sana. Unaweza kuta China, Syria na Urusi wanashirikiana vitu vingi sana na Marekani kuliko unavyoimbishwa kwenye media!
 
Nikifunga kiwanda cha kusaga sembe songea mfano kuleta dar, ili kuleta unga dar natakiwa niwe na risiti ya efd ambapo kila kiroba tra watakula si chini ya 3000 kww point kuwa unga umeuzwa hata kama bado sijauza, ila nikisafirisha mahindi toka songea kuja dar ntalipia ushuru wa halmashauri 1000 kwa kila mfuko wa kg 100. Kwa semitrailer la viroba 300 ntalipia 300000 kama ushuru tu. LAkini nikisafirisha unga kama naenda kuuza bei ya 17000 ntalazimika ntaingia gharama ya almost 3600000 kabla hata sijajua bei kama itapanda au kushuka.
Una Hangaya wateja wa Dar na Nairobi, kwakua hela ya Kenya ina nguvu mauzo yake yanafidia hasara nyingine.
 
Wewe tu na unaofahamiana nao na umuhimu wako kwa watu wanaoweza kukupa hizo fursa. Nchi hii ukiwa wa kulalamika na kutaka wengine wafanye kwa niaba yako unapoteza sana.
Ndo tuanzie hapa, wewe uwe ndo connector wng unisaidie usafir wa bure na soko la mahind Au unga Dar.
 
Ndo tuanzie hapa, wewe uwe ndo connector wng unisaidie usafir wa bure na soko la mahind Au unga Dar.
Sawa..... sasa uniambie wewe una umuhimu gani kwangu? Kwann nikupe hiyo connection? Una mzigo kiasi gani? Kama upo wa kutosha hakuna haja ya kupeleka dar. Hamna ela pale sokoni.
 
Any strong Economy inahitaji private business and enterprises ambao ndio walipa kodi na waajiri wakubwa katika jamii, lakini bila cheap credit, strong/non corrupt regulatory bodies, trust (insurance) na low taxes itakuwa ngumu sana kuwa nao kwenye jamii na ndio mwanzo wa umaskini mwingi kwenye jamii, huwezi kuwa na bank zinazotoa mikopo kwa 17% na mikodi kama ya kina Mwigulu then ukategemea uchumi ukue
 
Back
Top Bottom