likemike
Senior Member
- Mar 10, 2016
- 115
- 56
Habarini..
Jaman nchi hii inabidi hospitali za wagonjwa maalumu ziongezwe. Maana tunakoelekea sasa hapana kwa kweli.
Wakulima WANA-LAANI ardhi kuchukuliwa na wawekezaji. Jana wamewa-LAANI viongozi kwa kuuza ardhi kinyemela, tena wali-LAANI mauaji ya wenzao yanayofanywa na wafugaji. Na wafugaji nao wana-LAANI vivyo hivyo.
Tena mara utaskia jeshi la polisi lime-LAANI mauaji ya kibaka. Walo-LAANIWA kina nani? Wananchi wenye hasira kali. Na majuzi tu jeshi la polisi lika-LAANI utoroshwaji wa tumbili. Na majambaz nao hawako nyuma wakajipatia LAANA zao.
Huku na kule ukahawa waka-LAANI ubakaji wa demokrasia Zanzibar. Upande wa sikio la kufa waka-LAANI wasusia uchagizi.
Madaktar waka-LAANI mwenzao kupigwa. Ndugu nao waka-LAANI maiti kuombwa damu.
Watumishi hawako nyuma, nao waka-LAANI kufurushwa kazi. Wananchi wao waka-LAANI wafanyakazi misukule.
Utachoka kabisa ukiskia MCC ime-LAANI utoaji wa tr. 1. Na tena nchi washirika wa maendeleo toka bara Ulaya sijui kumi zime-LAANI misaada kwa Tz.
Mara ghafla mtu kaandika thread ndefu humu ana-LAANI viongozi kukosesha nchi fedha na misaada. Mwingine kamjibu huku povu likimtoka na LAANA tena kwanini tuwe tegemezi. Wachangiaji nao ni LAANA huku na kule. Basi ilimradi tu mtu kesha-LAANI na roho yake imesuuzika.
Wako tena wale wanao-LAANI wanaoshabikia kukosa misaada. Upande wa pili nao vivyo hivyo wana-LAANI kunyimwa.
Nchi hii jaman, kwa wepesi kabisa si kila mtu anae-LAANA yake apo ukubwa wa kizibo.
Tujiangalie jaman, tunakoelekea tutafika jaman maana kila mtu ana-LAANI
Kunae maneno yamezoeleka na si mazuri kwa kweli. Tujitafakari. Tofauti na hapo tutakuja kujikuta wote tumejazana hospital za vichaa kwa mi-LAANA isiyo mpango ...
Shukran
Likemikelove