Nchi hii imenichosha kabisa

Nipo uwanja wa ndege wa "kimataifa" wa JK Nyerere nikisubiri usafiri wa kwenda Kilimanjaro kwa ndege ya Precision Air,hali hapa uwanjani ni mbaya sana kuna mamia ya abiria wanasubiri kusafiri toka jana usiku,kinachonisikitisha na kilichonisukuma kuandika thread hii ni kuwa hakuna taarifa yeyote toka kwenye uongozi wa uwanja juu ya kinachoendelea,tumefuatilia na jibu tulilopewa ni kuwa eti **** timu toka JWTZ inasubiriwa ije ikague uwanja,nilitegemea hayo yangefanyika mapema sana ili kuondoa tafrani hii lakini hadi sasa haijulikani timu hiyo itafika saa ngapi.Watanzania tupunguze kufanya kazi kwa mazoea,tunatia aibu sana.
Ukitaka serikali na wahusika wa huo uwanja waje haraka hapo' piga simu na uwaambie kuwa kuna maandamano makubwa sana
ya wafuasi wa vyama vya upinzani na wanafunzi wa vyuo hapa ndani ya uwanja wa JK nyerere. utaona within 5 mns watakuwa
hapo na mabom,bunduki,maji ya kuwasha,virungu nk. Lakini zaidi ya hapo hesabuni imekula kwenu daima
 
Ndg zangu hapa ndipo CCM ilipoifikisha Nchi ye2. Unajua kwa Nchi yoyote ambayo Viongozi wake wa ngazi za juu, kama Rais na wasaidizi wake watakuwa hawana msimamo ni dhahiri nchi itayumba kwa kila eneo! Ndio maana umeona hata sisi wananchi tumelazimika kuharalisha Rushwa ili kurahisisha matakwa yetu, Viongozi wa chini mf. Watendaji wa kata na vjj kujifanya Miungu watu, Wakuu wa Idara mbalimbali za serikali kujiamini kupita kiasi hata kama wanakosea, Polisi kuua watu ovyo, nk, haya na mengine mengi ni matokeo ya Siasa mbovu. We unavyoona kwa nchi kama Tanzania 'nani anamwogopa nani?' Hii yote ni sababu ya serikali kukosa msimamo.
 
Hutakiwi kulalamika kana kwamba hujui hali halsi inavyoendelea hapa nchini. Nivizuri tukaacha tabia ya ubinafsi ambayo ndiyo imetufikisha katika matatizo tuliyonayo leo hii.

Kimsingi, suala la wewe kukosa ndege ya kusafiria kwetu halina nafasi sana kwani hayo ni mambo yako binafsi. Hivi sasa tumejikita macho na nguvu zetu kwa ndugu zetu, watanzania wenzetu ambao wamejeruhiwa kupoteza mali na maisha yao pasipo na hatia.

Shida ya watanzania ni ubinafsi, na kujali maslahi binafsi kama ambavo wewe unachanganya masuala yako binafsi wewe na mkeo/mumeo na masuala ya kitaifa.

Kama unaona hayo hayana msingi sana zaidi ya safari yako basi tutatilia shaka uwezo wako katika kufikiri na kuamua nini uongee, wapi na lini na kwanini. AU WEWE SIO MTZ MWENZETU?

''RAFIKI WA KWELI AKUFAAYE WAKATI WA DHIKI''

Inapotokea shida kama hiyo, kila mtu anatakiwa kuwajibika kutokana na nafasi yake na kazi yake. Ina maana kuwa hata abiria hao nao ni wahanga wa mabomu hayo kwa njia fulani. Kinachotakiwa kufanyika ni wao kupatiwa taarifa kamili kutoka kwa anayehusika na usafiri kuhusu hali hiyo. Kusingizia tu chanzo cha tatizo ndio mwanzo wa kutokuwajibika na uzembe kuenea.
 
<i>Hutakiwi kulalamika kana kwamba hujui hali halsi inavyoendelea hapa nchini. Nivizuri tukaacha tabia ya ubinafsi ambayo ndiyo imetufikisha katika matatizo tuliyonayo leo hii
Kimsingi, suala la wewe kukosa ndege ya kusafiria kwetu halina nafasi sana kwani hayo ni mambo yako binafsi. Hivi sasa tumejikita macho na nguvu zetu kwa ndugu zetu, watanzania wenzetu ambao wamejeruhiwa kupoteza mali na maisha yao pasipo na hatia.
Shida ya watanzania ni ubinafsi, na kujali maslahi binafsi kama ambavo wewe unachanganya masuala yako binafsi wewe na mkeo/mumeo na masuala ya kitaifa.
Kama unaona hayo hayana msingi sana zaidi ya safari yako basi tutatilia shaka uwezo wako katika kufikiri na kuamua nini uongee, wapi na lini na kwanini. AU WEWE SIO MTZ MWENZETU?
''RAFIKI WA KWELI AKUFAAYE WAKATI WA DHIKI

Nashukuru Mungu baada ya msukosuko wa zaidi ya masaa 7 pale Airport atlast nimefika nilipokuwa nakwenda,nawapa pole sana ndugu zetu wa Gongolamboto waliopatwa na yale matatizo ya jana.
Wewe mzee wa Inshu ni vyema siku nyingine uwe unasoma na kuelewa vizuri maudhui ya hoja iliyotolewa kabla ya kutoa comment zako,sometimes kama huna cha kuandika ni bora ukasoma na kupotezea kama walivyofanya wenzio wengi tu,kwa Comment yako hii naona huna tofauti na viongozi wa airport na viongozi wengine wazembe wa nchi hii
<br />
 
Back
Top Bottom