Nchi hii imenichosha kabisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi hii imenichosha kabisa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by M-bongotz, Feb 17, 2011.

 1. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Nipo uwanja wa ndege wa "kimataifa" wa JK Nyerere nikisubiri usafiri wa kwenda Kilimanjaro kwa ndege ya Precision Air,hali hapa uwanjani ni mbaya sana kuna mamia ya abiria wanasubiri kusafiri toka jana usiku,kinachonisikitisha na kilichonisukuma kuandika thread hii ni kuwa hakuna taarifa yeyote toka kwenye uongozi wa uwanja juu ya kinachoendelea,tumefuatilia na jibu tulilopewa ni kuwa eti **** timu toka JWTZ inasubiriwa ije ikague uwanja,nilitegemea hayo yangefanyika mapema sana ili kuondoa tafrani hii lakini hadi sasa haijulikani timu hiyo itafika saa ngapi.Watanzania tupunguze kufanya kazi kwa mazoea,tunatia aibu sana.
   
 2. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,659
  Likes Received: 940
  Trophy Points: 280
  Kama safari yako ni ya muhimu kuliko majeruhi unaweza kukodi helikopta
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mh!no comment sometimes is better than non sense comment!!
   
 4. m

  mwanafyale JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mwanamke halisi hachoki ! anakomaa mpaka mwenzake ashindwe !
   
 5. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Pole sana mkuu kwa matatizo yaliyokukuta,hii ndiyo Tanzania yetu,tuwe wavumilivu!!
   
 6. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Madams will remain madams ....... Kutotatua tatuzi lililokuwepo hilo la mabomu ni tatizo japo ilibidi lisitokee au lidhibitiwe...... Lakini kuzidi kuleta matatizo kwa kigezo au kwa sababu ya tatizo lililopo napo ni tatizo mno? Huyo mtu hujui anaenda fanya nn Moshi...... akifukuzwa kazi, kama kuna mgonjwa etc? Kwahiyo uzembe wa mtu/kikundi/serikali ki-ujumla kutodhibiti mabomu na majanga mengine isiwe sababu ya Madam kuona lililo at hand ni muhimu zaidi..... Umuhimu has to be equally weighed..... Na kwa taarifa yako serikali makini ni ile kwenye tatizo inatatua tatizo husika faster while ensuring the other related probs are contained smoothly (bila kuanzisha tatizo lingine).....
   
 7. M

  MAINA Member

  #7
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole kwa kukatizwa safari
  hayo nimatokeo ya uongozi mbaya wa kikwete
  huku kilimanjaro ndge zimepaki hazina pakwennda iliyokuja jana uck kutokea ams jro dar imeshindwa na abiria wote wako hotelini
  huu upuuzi wa serikali yetu utaisha lini?
   
 8. M

  Mgalatia JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tatizo siyo serkali bali watu waliopewa dhamana ya kazi. Hivi JK aende jeshini na kiwaambia askari waende wakacomb runways za airport Dsm na maeneo jirani ili kuondoa vyuma au mabomu ambayo hayakulipuka ili kuruhusu ndege kutua na kupaa hapo?
  Sasa tukio moja linatushinda kurudisha haraka Hali ya kawaida itakuwaje Kama inazuka vita?
   
 9. Rural Swagga

  Rural Swagga JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu mbongo pole sana mm mwenyewe nimekwama mwanza Airport toka jana ucku
   
 10. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Bora Ungelamba Dar express saizi ungekuwa umefika tayarri
   
 11. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Madam T hujui unachokisema,kama ungekuwa hapa airport ndio ungeona adha iliyopo,hatukatai dharura kama hizi kutokea lakini kilichonikwaza ni uongozi wa uwanja kukaa kimya wakati watu wamelala uwanjani toka jana usiku,sidhani kama ilikuwa ngumu sana kuwapa taarifa wasafiri ya ni nini kinachoendelea na watarajie hali kutengemaa baada ya muda gani.,information is power remember.
   
 12. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Ingekuwa vizuri kama tungekuwa tunasoma post na kuelewa maana yake na si kukurupuka ku-comment tu!!
   
 13. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mijiti mingine Bwana haina adabu kabisa, wala sitaha.
   
 14. d

  dorry Senior Member

  #14
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  sikutegemea madam uwe na comment za kihivi. Nadhani concern ya mwenzio sio kwa ajili yake tu. Ina maana wanajeshi wote wanatibu au kuhudumia majeruhi? Kubadilika ni muhimu tusiwaongezee ukubwa wa mabichwa wazembe watatumaliza hawa. pole madam kama nitakuwa nimekukwaza.
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Pole sana kwa yaliyokukuta ndiyo Tanzania yetu hiyo
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Uongozi wa juu wa nchi umeshindwa kabisa kufanya kazi ndiyo maana madudu yanaongezeka kila mahali. Ingekuwa hawa wanaojiita viongozi wanaweka mbele maslahi ya nchi Serikali yote ingejiuzulu ili iundwe Serikali mpya na kuitisha uchaguzi haraka sana, lakini hawa mafisadi wataendelea kubaki madarakani kwa miaka mitano mingine hata kama nchi inadorora kiasi gani katika mambo mbali mbali ikiwemo uchumi. Dr Slaa hakukosea kabisa aliposema kumpigia kura Kikwete ni sawa na kuitakia nchi yetu maafa makubwa.
   
 17. m

  mzee wa inshu Member

  #17
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hutakiwi kulalamika kana kwamba hujui hali halsi inavyoendelea hapa nchini. Nivizuri tukaacha tabia ya ubinafsi ambayo ndiyo imetufikisha katika matatizo tuliyonayo leo hii.

  Kimsingi, suala la wewe kukosa ndege ya kusafiria kwetu halina nafasi sana kwani hayo ni mambo yako binafsi. Hivi sasa tumejikita macho na nguvu zetu kwa ndugu zetu, watanzania wenzetu ambao wamejeruhiwa kupoteza mali na maisha yao pasipo na hatia.

  Shida ya watanzania ni ubinafsi, na kujali maslahi binafsi kama ambavo wewe unachanganya masuala yako binafsi wewe na mkeo/mumeo na masuala ya kitaifa.

  Kama unaona hayo hayana msingi sana zaidi ya safari yako basi tutatilia shaka uwezo wako katika kufikiri na kuamua nini uongee, wapi na lini na kwanini. AU WEWE SIO MTZ MWENZETU?

  ''RAFIKI WA KWELI AKUFAAYE WAKATI WA DHIKI''

   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,957
  Likes Received: 23,632
  Trophy Points: 280
  Angefika salama kama yale makombora yaliyokuwa yanaelekea kimara yasingekutana na Dar Express.
   
 19. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  bunge limesimamishwa, hayo tu yaliyobaki bado ni kitendawili unataka waje aport, namsaport madam t kodi helkopter brother
   
 20. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mijadala mingine watu wanacomment tu bila kufikiria side effects ya tatizo lenyewe.
  Sasa hivi viongozi wote wanakimbilia kuokoa majeruhi na kutafuta yale ambayo bado hayajalipuka
  bila kujali kwamba kuna order walizozitoa ambazo zina madhara pia kwa upande mwingine wa system.
  Lazima ukabiliane na tatizo accordingly mfano airport wana security sysems ambazo lazima zitaonyesha kama
  kuna kitu chochote kiiliingia ndani ya uwanja.
  Kataeni mkubali hatuna viongozi tuna wasimamizi.
   
Loading...