Tujifunze: Hii mikopo 'nafuu' toka China itauza nchi hapo baadae kama yanayotokea Malaysia na Zambia

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Ni ukweli usiopingika kuna kamsemo kanaenea sana toka kwa watawala wakidai mikopp ya riba nafuu na wanaongeza isiyo na masharti ila hiyo rina nafuu huwa haisemwi ni ngapi na masharti hayo hayawekwi wazi.

Tuliwacheka mababu zetu kuwa walisaini mikataba mibovu kama Mangungo wa musowero lakini nashangaa hii mikataba ya sasa ya madini na rasilimali inatofauti gani na hizo ya Karl Peters?

Kwa sasa Uchina ndio mkoloni mbaya zaidi ya mzungu wa ulaya na marekani na anataka kuitawala afrika kwa nguvu zote.

Kaanza kiuchumi, ameshawekeza kijeshi na kiutawala na majuzi kaja na donge nono kwa afrika kama kishika uchumba.

Ila kwa taarifa madeni hayo makubwa yasiyolipika yamepelekea nchi ya malesyia kuachia bandari yake kwa china na huku zambia wakijiandaa kichukuliwa kwa uwanja wa ndege wa lusaka ili wawe wanapokea mapato kama marejesho.

Sie awamu hii ya tano mikopo ni zaidi ya trilion 20 zishakopwa itafika kipindi bandari salama itakiwa sio yetu tena.

Tuendelee kuunga juhudi
 
Uzuzu wa CCM utatukosti.
Nchi masikini haiwezi kuendelea kwa kutegemea misaada kutoka nchi tajiri
 
Unamwangaliza Nani sasa? Nenda pale ikulu jichome Moto na sisi tutakuunga mkono.
 
Kama ulikuwa hujui ni kwamba deni la Tanzania % kubwa ni la wazungu yani IMF na world Bank... Kingine mradi uliogalamiwa na China ni bomba la Gesi la mtwara.miradi mingine yote yani barabara,airport,kinyerezi ni mikopo toka IMF na world na bank ya maendeleo Afrika...wachina wanapewa tenda ya kujenga c kugaramia miradi...
 
Unagombana na wawekezaji ambao ndo walipa kodi kisha mapato unakosa unaenda kukopa mikopo ya kimangungo alafu mnasema ya mashartì nafuu inayowezesha kulipa kwa miaka 40.

Wakoloni tuachieni nchi yetu jamani tupate uongozi wenye tija kwa wananchi wapate faidi keki ya taifa
 
rejea mikataba 21 ile aliyoingia wa msoga na wachina.
kiufupi nchi ishauzwa.bado mgawo wetu tu.
Nikipata naenda kuishi sauzi
 
Tatizo hakuna uwajibishwaji kwa wale wanaohusika kuingia hii mikataba inaposainiwa na mara nyingi athari zake huonekana wakiwa washaondoka madarakani. Hili la China likija kuleta madhara Jiwe bin Kichaa atakuwa Chattle anachunga mabata na atakaekuwa madarakani atasema mumuache mzee apumzike.
 
Kama ulikuwa hujui ni kwamba deni la Tanzania % kubwa ni la wazungu yani IMF na world Bank... Kingine mradi uliogalamiwa na China ni bomba la Gesi la mtwara.miradi mingine yote yani barabara,airport,kinyerezi ni mikopo toka IMF na world na bank ya maendeleo Afrika...wachina wanapewa tenda ya kujenga c kugaramia miradi...
Ufipa hawataki kuskia haya.
 
Tatizo hakuna uwajibishwaji kwa wale wanaohusika kuingia hii mikataba inaposainiwa na mara nyingi athari zake huonekana wakiwa washaondoka madarakani. Hili la China likija kuleta madhara Jiwe bin Kichaa atakuwa Chattle anachunga mabata na atakaekuwa madarakani atasema mumuache mzee apumzike.
Tatizo lenu nyie ufipa hata rais akiwawa jibisha bado mtasema kawaonea, au mtaanza kusema analipiza kisasi..
 
Again mwendelezo wa malalamiko mtandaoni. Si China, Europe wala US wenye nia njema na Afrika....yanayowakuta Zambia wakujilaumu ni wao wenyewe, rushwa, mismanagement, ubinafsi yanawapa walichokuwa wanastahili. China katumia fursa tu.
 
Unagombana na wawekezaji ambao ndo walipa kodi kisha mapato unakosa unaenda kukopa mikopo ya kimangungo alafu mnasema ya mashartì nafuu inayowezesha kulipa kwa miaka 40.

Wakoloni wa kijani tuachieni nchi yetu jamani tupate uongozi wenye tija kwa wananchi wapate faidi keki ya taifa
Hebu shusha line-up ya uongozi wenye tija tuuone!
 
Uzuzu wa CCM utatukosti.
Nchi masikini haiwezi kuendelea kwa kutegemea misaada kutoka nchi tajiri
Mikopo sio misaada, Najionea huruma kwa mikopo mingi isiyo na tija tumeingia kama taifa awamu za nyuma, Nionavyo mimi miradi mingi inayoanzishwa chini ya JPM ni miradi muhimu kuinua uchumi wetu siku za usoni.
 
Unagombana na wawekezaji ambao ndo walipa kodi kisha mapato unakosa unaenda kukopa mikopo ya kimangungo alafu mnasema ya mashartì nafuu inayowezesha kulipa kwa miaka 40.

Wakoloni wa kijani tuachieni nchi yetu jamani tupate uongozi wenye tija kwa wananchi wapate faidi keki ya taifa
Soma hii wilbert peter
 
Sie awamu hii ya tano mikopo ni zaidi ya trilion 20 zishakopwa itafika kipindi bandari salama itakiwa sio yetu tena.
Tunakopa na kujenga nchi na uchumi
Hao zambia walikopa wakafisadi nchi
Hivi unatarajia SGR haitapata faida ikisimamiwa vizuri?
Hivi unategemea Nyerere gorge haitashusha bei za umeme na kufanya uchumi ukue?
 
Back
Top Bottom