Nchi Hii Haijawai Kuishiwa Na Vituko

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
1,914
1,977
JPM: "Katika utawala wangu hakuna atakayepata mimba na kurudi shule. .., ni bora wakalime ili ile nguvu waliyoitumia kujifungua waitumie kulima."

Naibu Waziri TAMISEMI; "Ni marufuku mtoto wa kike kuolewa (Kufunga Ndoa) kama hana Cheti cha kidato cha nne"
_________________________________

Watoto wa kike msaada pekee ambao naweza kuwapa kwa sasa ni msaada wa maneno makavu kwamba; MTALIMA NA KUPIGA MBIZI KWENYE LAMI round hii..

Vituko vya nchi yenu; ili kuwa mbunge, RC, DC sifa ni ujue kusoma na kuandika tu, lakini binti ili ufanikiwe kuolewa lazima uwe na cheti cha kidato cha nne, (wonderful)

nchi haijawahi kuishiwa vituko hii.., hatujawahi kuacha kujishangaza..,we're the core authors of our very own misfortunes.

MMM
 
Vituko vya nchi yenu; ili kuwa mbunge, RC, DC sifa ni ujue kusoma na kuandika tu, lakini binti ili ufanikiwe kuolewa lazima uwe na cheti cha kidato cha nne, (wonderful)

Aisee
 
Vituko vya nchi yenu; ili kuwa mbunge, RC, DC sifa ni ujue kusoma na kuandika tu, lakini binti ili ufanikiwe kuolewa lazima uwe na cheti cha kidato cha nne, (wonderful)

Aisee
hii ndo kali kuliko
 
Kuna wakati nguri wa sheria nchini africa mashariki almaarufu kama prof Mwakyembe aliwahasa wana habari waende shule nadhani alikua sahii,mambo ya msingi awatilii maanani zaidi ya ku-quote mizaa na utani ili waendeshe vyanzo vyao vya mapato mitandaoni mwisho wasiku jamii inakumbwa na taharuki
 
Nchi hii inaharibiwa na wachache wanaofahamika. Halafu baadaye utasikia... "jamani tulikosea sana wote tujisahihishe na sisi mtuamini kwa kutupa uongozi..." Dammit!
 
Back
Top Bottom