Nchi gani ina viongozi maprofesa wengi zaidi duniani?

Nchi gani ina viongozi maprofesa wengi zaidi duniani?

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2013
Posts
2,007
Reaction score
1,898
hivi ni nchi gani inaongoza duniani kuwa na viongozi wengi ambao ni maprofesa, na tukipima mafanikio waliyoyaleta ni yepi?

hapohapo, hivi tukichukua maprof kuwa viongozi, vyuo vikuu anabaki kufundisha phd holder na Masters pekee, rating ya vyuo vyetu kidunia inakuwa katika hali gani?

ni fikra tu. hivi prof ambaya ana uzoefu wa kufundisha tu, pia amejaa theories hakuna uzoefu wa practice anao uwezo kuongoza kuliko mtu mwenye degree moja aliyekaa kwenye sector fulani kwa miaka hata kumi au zaidi ana uzoefu wa kutosha kwenye eneo hilo?

ni bora kuteua watu wasio na uzoefu kuwaongoza wenye uzoefu kwa kigezo cha uwingi wa degree?
kipi bora wakuu?
 
Ni Tanzania tu watu wanadhani kua prof ndio kujua kila kitu.

Kama maprofesa wangekua ndio kila kitu basi nchi kama Marekani au Ugiriki ambayo demokrasia na utaalam umezaliwa wangekua wanaongozwa na maprof tu.
 
lakini tuseme ukweli, kati ya uzoefu wa mtu mwenye elimu ya kawaida, na kukosa uzoefu (mtu amejaa theories) kwa mtu mwenye degree nyingi, kipi bora? Kagame nadhani kama atakuwa amejitahidi sana ana degree moja, lakini kichwani yupo smart na amewazidi maprof wengi tu. kwa mawazo ya kawadia, maprof wengi wakiwa kwenye nchi maendeleo yataenda fasta sana. Malawi ni nchi masikini mno na inaongozwa na profesa, na tangu prof aingie madarakani hakuna nafuu yeyote substantial inayoonekana....tunajifunza nini hapo?
 
hivi ni nchi gani inaongoza duniani kuwa na viongozi wengi ambao ni maprofesa, na tukipima mafanikio waliyoyaleta ni yepi?

hapohapo, hivi tukichukua maprof kuwa viongozi, vyuo vikuu anabaki kufundisha phd holder na Masters pekee, rating ya vyuo vyetu kidunia inakuwa katika hali gani?

ni fikra tu. hivi prof ambaya ana uzoefu wa kufundisha tu, pia amejaa theories hakuna uzoefu wa practice anao uwezo kuongoza kuliko mtu mwenye degree moja aliyekaa kwenye sector fulani kwa miaka hata kumi au zaidi ana uzoefu wa kutosha kwenye eneo hilo?

ni bora kuteua watu wasio na uzoefu kuwaongoza wenye uzoefu kwa kigezo cha uwingi wa degree?
kipi bora wakuu?
Ni Tanzania ndo inao maprofesa wengi viongozi Serikalini lakini ndo wanaongoza kwa umbumbumbu,wameshindwa kabisa kumsaidia nambari moja maana walizoea darasani kwa hiyo wanapoingia kwenye field wanachemka vibaya,vichwa vyao vimeshajichokea. Rais anapaswa kulitambua hilo kwamba asitegemee msaada wowote kutoka kwa hao maprofesa wake maana huku makazini ni zero brain wanachekwa hadi na wale wafanyakazi wa darasa la saba. Kama Rais kadhamiria kuitengeneza Tanzania mpya aachane na maprofesa badala yake adeal na watu wenye uzoefu mkubwa na kazi hakika hao watamsaidia
 
Wengi wa maprofesa wenye ufanisi ni wale ambao zaidi ya kufundisha na kuandika huwa wanajishughulisha na kazi zingine zinazoendana na taaluma zao

Kwamfano, profesa wa mambo ya jeolojia ajishughulishe na mambo ya jeolojia, kwa kufanya hizo shughuli na mambo mengine yanayohusu jeolojia. Anatakiwa awe anaenda huko huko maporini etc

Sio kukaa ofisini tu na kusoma na kuandika majarida na kwenda kufundisha . anatakiwa awe MTU wa field, huko kazi husika zinakofanyika

Maprofesa wetu wengi hawako hivyo. Hawavifanyi wanavyofundisha. Ni full theories

Halafu huyu unafanya anakuwa bosi wa mambo ya madini, kisa ni profesa. Uzoefu wa kivitendo kwenye fani husika ni jambo la maana sana
 
Watu hawana jema Magufuli kaamua kuwatumia wasomi kuleta tija mwalalama

Akiteua tena wasio na elimu mnataka cv iwekwe muona, ikiwa ni mchele mchele mnadai kateua mtoto wa dada yake?
 
Elimu itakusaidia kama utakua una talent ya uongozi otherwise elimu ya theory si kipimo cha kuwa kiongoz bora
 
Watu hawana jema Magufuli kaamua kuwatumia wasomi kuleta tija mwalalama

Akiteua tena wasio na elimu mnataka cv iwekwe muona, ikiwa ni mchele mchele mnadai kateua mtoto wa dada yake?
kutumia wasomi maprofesa halafu vyuoni afundishe nini?
 
Watu hawana jema Magufuli kaamua kuwatumia wasomi kuleta tija mwalalama

Akiteua tena wasio na elimu mnataka cv iwekwe muona, ikiwa ni mchele mchele mnadai kateua mtoto wa dada yake?
watu hawalaumu kwakuteuliwa wasomi mkuu
Bali wanasikitika kwakuona kuwa wasomi walioteuliwa wanamuangusha aliowateua kwakushindwa kwao kukaimu vyema sekta zao walizopewa
usiwe unakarili maisha tu nakudhani kila wakati niwakumzungumzia vibaya mh.Raisi
hapa watu wanajadili mambo nyeti kabisa kwaajili ya mkabala wa nchi yao

kama maproffesor wanashindwa kutatua changamoto mbali mbali zilizopo nchini ..so nikipi kifanyike
ndio ilikuwa naviongozi timamu kiutendaji ambao utafanana na level ya elimu yao.

hvyo ndio vitu ambavyo vimetufanya tutege macho yetu na fahamu tulizonazo dhidi ya wachambuzi wetu ili nasisi tuweze kung'amua jambo

maana kwanza yatakiwa utambue kuwa ni aibu kwa mtu anayeonekana amebobea katika usomi kisha akawa na utendaji uliokonda ambao unafanana nayule ambaye hana lundo la degree's
 
Nchi ya ITALY kuna serikali flani iliyokuwa madarakani iliamuwa kutea mawaziri na viongozi mbali mbali PHD, maprofesa, kwa ujumla Watu waliosoma. Sijajua ile serikali iliiishia vp kuhusu mafanikio
 
Wengi wa maprofesa wenye ufanisi ni wale ambao zaidi ya kufundisha na kuandika huwa wanajishughulisha na kazi zingine zinazoendana na taaluma zao

Kwamfano, profesa wa mambo ya jeolojia ajishughulishe na mambo ya jeolojia, kwa kufanya hizo shughuli na mambo mengine yanayohusu jeolojia. Anatakiwa awe anaenda huko huko maporini etc

Sio kukaa ofisini tu na kusoma na kuandika majarida na kwenda kufundisha . anatakiwa awe MTU wa field, huko kazi husika zinakofanyika

Maprofesa wetu wengi hawako hivyo. Hawavifanyi wanavyofundisha. Ni full theories

Halafu huyu unafanya anakuwa bosi wa mambo ya madini, kisa ni profesa. Uzoefu wa kivitendo kwenye fani husika ni jambo la maana sana
Tunao Maprofessor wachapakazi na wenye practical experience Serikalini.....Mfano mzuri ni Muheshimiwa Professor Maji Marefu Sometimes huacha shughuli za kibunge na kusaidia wananchi wa jimboni kwake Kutoa wachawi......
 
Back
Top Bottom