Nchemba: Wahisani wamerejesha misaada

Nchemba: Wahisani wamerejesha misaada

Shida kubwa ni waandishi wa Tz, huwa hawaendi deep. Wao kazi yao kupokea taarifa yoyote bila kuhoji wala nini. Ndio maana rais Ben Mkapa alikuwa anawadharau sana..
ni kweli kabisa mwigulu anasema uwongo na wao wanaandika bila kumhoji huu ndo ujinga unawasumbua watu wengi habari nyingine wanazoziandika wanazitoa humu JF.
 
..mpaka sasa haijatoka hela....wacheni propaganda zisizoisaidia nchi....Taarifa ya mwisho toka washirika wa maendeleo kupitia mwenyekiti wao ambae ni balozi wa Finland TZ (bi Sinikka Antila) inasema kuwa bado wanasubiri hatua zaidi toka GoT dhidi ya wezi wa hela za escrow waliotajwa kwenye maazimio ya bunge....Taarifa hii ndio latest na imetoka hapo December 25th mwaka jana....

..Utaipata hapa Citizen: Donors insist on more escrow action

..Katika taarifa yake hii bi Antila anasema kwamba fedha iliyotoka ni asilimia 15% tu hadi sasa (dola mil.84$)..na hizi zilitoka kabla ya kashfa hii kujadiliwa bungeni....

..Habari zaidi juu ya msimamo wa wahisani hadi sasa juu ya suala hili utaupata hapa chini:

Home
Delays in resolving power deal hurts Tanzania
 
ni usiri wa kijinga au ndo uongo wa mwigulu mana huyu mheshimiwa naye ni muongo aliyebobea nikikumbuka ushaidi wa mbinguni aliousema bungen juu ya ugaid sina iman naye!!mambo magum majbu mepesi hajasema kiasi gan!!politics tu za kujifarij
 
Sikumsikia Radio one, but nilimsikia ITV kupitia kipindi chao baada ya magazeti on Sunday, maneno aliyokua akitumia si haya, "Kwa hatua zilizochukuliwa, naamini wahisani watarudisha misaada" na pia alisema hivi, "Waziri wa fedha atakua na mzungumzo na wahisani" Sikusikia kitu chenye uhakika kwamba wahisani wamerudisha misaada kwa nchi yetu.

Kitu kmojaambacho pia sikukipenda toka kwake ni hiki, Aliulizwa na Fatuma Almas Nyangasa kuhusu tamko lake ya bungeni kama wale wanufaika je, wamelipa kodi au laa? Jibu lake nalo hakua na uhakika, alianza kusingizia sikukuu n.k lakini akatoa tena ahadi nyingine ya kwenda TRA kufuatilia, hesabu yangu ya haraka haraka Tibaijuka na Chenge kila mtu kwa alitakiwa kulipa kodi Tsh 431,890,700/= Halafu hawa bado hawajalipa. Najiuliza, kwanini sisi masikini wenye viduka vya kuuza vibiriti tu, usipolipa hadi 31 December unakutana na kufuri la TRA dukani kwako? Mbona kwa hawa wateule hali ni tofauti?
 
kila nikimuona mugulu mchemba au nikimsikia nakumbuka bomu la soweto arusha kwa kweli aliyoyafanya mugulu lazima yatalipwa na serikali yeyote ile itakayochukua madaraka tofauti na ccm

umenikumbusha hili tukio huyu bwana hata akienda kusali marekani asipowaomba radhi wana arusha na familia zilizopatwa na zahma hii akika ataugulia moyo wake maisha yake yote
 
Chadema wameacha kupokea msaada kutoka chama cha siasa cha kikristo cha Ujerumani?

Wewe kila wakati na ukristo tuu huna jingine? Au ulishapata mkristo akakutumia kinyume na .. ? Ndio maana una chuki na wakristo wote? Chuki zako ni za wazi kabisa mpaka unakera!
 
Chadema wameacha kupokea msaada kutoka chama cha siasa cha kikristo cha Ujerumani?

Hapo tu ndio tunapishana wewe kila kitu udini yani ndio ninazidi kuamini chama tawala ndio kinazidi kuligawa taifa kwa misingi ya kidini.
 
Kama anayosema mwigulu ni kweli, basi sio bure, ni lazima hao wahisani wameshagewiwa asilimia zao za gesi na rasilimali nyingine. Si mnajua tena CCM kwa rushwa! Haina hofu yeyote, inaweza hata kuuhonga ulimwengu.
 
Sidhani kama fundisho hapa ni kujenga misingi ya kujitegemea...
Fundisho hapa ni viongozi wawe waadilifu na kuacha ufisadi... simple.

Ukiona mtu miaka yote anajifunza kiyu kile-kile na haelewi, jua kwamba mtu huyu ni mpumbavu. CCM kila siku inasema imepata fundisho katika jambo fulani lakini inarudia yaleyale kisha baada ya muda mambo yakishindikana tena inasema imepata fundisho! Mpaka lini? Tumechoka tunataka na wengine wapewe nafasi watende.
 
akili ndogo we mda wote unawaza uchonganishi wa dini tu ??

Hivhi uchanganishi uko wapi, jisomee;

Chama tawala nchini Ujerumani, Christian Democratic Union (CDU), ambacho ni chama rafiki na Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kimesema kitawapa nafasi za mafunzo nchini humo vijana viongozi wa Chadema, kusomea maadili na uongozi.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema hayo mwishoni mwa wiki baada ya mazungumzo ya faragha yaliyomshirikisha pia Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa na viongozi wengine wa juu, na ujumbe wa CDU, uliokuwa ukiongozwa na Rais wa zamani wa Ujerumani, Profesa Dk. Horst Kohler.
Alisema katika mazungumzo yao, Kohler alisema dhamira ya kuwapa nafasi za masomo vijana viongozi wa Chadema inalenga kuwafanya wawe viongozi wenye maadili mazuri kwa taifa lao.
"Tumekubaliana ambapo tutapata nafasi za masomo kwa vijana ambao ni viongozi wa Chadema kwenda kusomea uongozi na maadili nchini Ujerumani," alisema.

Chanzo: Vijana wa Chadema kupewa mafunzo Ujerumani - Jukwaa la Wananchi

Cha kushangaza, hawa CDU waliiona kuwa chadema haina maadili ndiyo wakawapa ofa ya kuwafunda maadili, badala ya chadema kupeleka Mwenyekiti na Katibu Mkuu wao kundwa maadili wao wanapeleka vijana, makubwa haya.
 
Alisema uamuzi uliochukuliwa na wahisani kusitisha misaada kwa Tanzania kwa muda ni fundisho kwamba kama nchi tunahitaji kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kuwa na kujenga misingi ya kujitegemea. "Kama Taifa tuanze misingi ya kujitegemea, tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo halafu unategemea fedha za wahisani ni tatizo," alisema.CHANZO: NIPASHE

Kuanza kuweka misingi ya kujitegemea bila kuwa na matumizi mazuri ya fedha is like putting the cart before the horse. Waswahili mnasema kuchota maji kwa kutumia tenga!

With all due respect Hon. Mwigulu inabidi kwanza kama nchi tuanze kuwa na nidhamu ya matumizi ya pesa this includes to fight grand corruption by teeth ana nails. THIS MUST BE FIRST PRIORITY

Lakini kuweka misingi ya kujitegemea KWANZA bila kuwa na misingi mizuri ya matumizi ya pesa ni kutwanga MAJI KWENYE KINU.

Kama hiyo ndiyo priority nambari ONE MoF, then you have inverted priority. Kuweka misingi mizuri ya matumizi ya pesa kunabidi kuje mwanzo na hakuhitaji Misaada ya nje ni UTASHI TU WA KISIASA. I know you can do that Mwigulu.
 
NARUDIA, Unaweza kusoma ulichoandika na kujitathmini kama mtazania ni namna gani usaidiwe ili uwe raia bora na timamu??

KUJIFUNZA MAADILI YA UONGOZI KUNA MAANA YA MTU HANA MAADILI????? HAPPY NEW YEAR!!!

Soma post #34 halafu ujibu na hilo, ushahidi kamili.
 
NARUDIA, Unaweza kusoma ulichoandika na kujitathmini kama mtazania ni namna gani usaidiwe ili uwe raia bora na timamu??

KUJIFUNZA MAADILI YA UONGOZI KUNA MAANA YA MTU HANA MAADILI????? HAPPY NEW YEAR!!!

Maadili huanzia nyumbani. Si mpaka mzungu wa chama cha kikristo cha Ujerumani akuone huna maadili akufundishe. Hukuwa na wazee wenye maadili mema wakakufunda?
 
Back
Top Bottom