Nchemba: Wahisani wamerejesha misaada

Nchemba: Wahisani wamerejesha misaada

Chadema wameacha kupokea msaada kutoka chama cha siasa cha kikristo cha Ujerumani?

Kiukweli dada angu huwa sikuelewi kabisa, chadema imeingia vp kwenye misaaada ya MCC?
 
quote_icon.png
By idoyo

Alisema uamuzi uliochukuliwa na wahisani kusitisha misaada kwa Tanzania kwa muda ni
fundisho kwamba kama nchi tunahitaji kujenga misingi ya kujitegemea. “Kama Taifa tuanze misingi ya kujitegemea, tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo halafu unategemea fedha za wahisani ni tatizo,” alisema.

Sidhani kama fundisho hapa ni kujenga misingi ya kujitegemea...
Fundisho hapa ni viongozi wawe waadilifu na kuacha ufisadi... simple.

Kama nia yao ni kuwa TUWEZE KUJITEGEMEA ILI WAWEZE KUIBA VIZURI WAKIJUA HAKUNA ATAKAYETUWAJIBISHA. Ninaomba Mungu ni bora atuache tu hivi hivi tegemezi kwa hao wazungu ili viongozi wetu wasipate pa kuibia mpaka CCM itakapotoka rasmi madarakani
 
HAIJALISHI NI WAPI, HATA NYUMBANI BADO NI TENDO LILE LILE LA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHA. KWA MJIBU WA FIKRA ZAKO NI KAMA ANAYEJIFUNZA MAADILI NI YULE AMBAYE HANA SASA CJUI YATAANZIAJE NYUMBANI BILA KUMFUNDISHA MTU. PILI MAADILI YA UONGOZI NI ZAIDI YA KUONGOZA FAMILIA YAKO NA NI SOMO PANA NA ENDELEVU KWA KIONGOZI MKOMAVU. HATA BABA AU MAMA KATIKA FAMILIA HAKOMI KUJIFUNZA MAADILI, MAKANISANI AU MISKITINI HATUKOMI KUJIFUNZA MAADILI. NA MIONGONI MWAKE MWAKE NI KUTOKUMBAGUA MTU KWA DINI YAKE WALA RANGI YAKE (HUU NDO MSINGI WA KWANZA WA MAADILI KUANZIA KWENYE FAMILIA, CJUI WEWE KWENYE FAMILIA UMEFUNZWA NINI). KUJIFUNZA MAADILI KWA MTU MZIMA HASA KIONGOZI NI MUHIMU SANA NA TOFAUTI NA KUMFUNDISHA MTOTO a,e,i,o,u. KWA MTU MZIMA NI KUSHIRIKISHANA UJUZI, UZOEFU, HULKA ZA WATU NA NAMNA UNAVYOWEZA KUWATUMIA WOTE KULETA MAENDELEO YENYE TIJA KWAO, KUTOKUWAKUMBATIA MAFISADI NA WALA RUSHWA n.k.

USHIRIKISHANAJI MAWAZO UNAWEZA KUFANYIKA NA MTU YEYOTE MWENYE UJUZI HUO SI TATIZO AKIWA MZUNGU, MHINDI, MWAARABU, MUISLAM, MKRISTO, MBUDHA, WAZEE WA KIMILA n.k. ILA UKIWA HAUNA MAADILI UTAWATAZAMA KWA MATABAKA YAO, DINI ZAO RANGI ZAO, MAVAZI YAO, LUGHA ZAO n.k.

KARIBU CDM NA WEWE UJIFUNZE KUWA KUJIFUNZA MAADILI NI JAMBO LILO BORA KWAKO, JIRANI YAKO, NDUGU YAKO NA VIONGOZI WAKO WA NCHI, DINI, VIKUNDI MABALI MBALI n.k.

=FaizaFoxy;11583931]Maadili huanzia nyumbani. Si mpaka mzungu wa chama cha kikristo cha Ujerumani akuone huna maadili akufundishe. Hukuwa na wazee wenye maadili mema wakakufunda?[/QUOTE]
 
Tatizo lako ni moja na litakupa kiholo sana hadi utaugua magonjwa ya ajabu, unapenda sana kuwaangalia watu kwa macho ya kidini. Halina tija hili ni upuuzi mtupu, achana nalo, wa dini au imani yako anaweza akawa mwizi, msaliti, mwongo, mzinzi, muuaji, jambazi, na akakudhuru na wewe pia kinyume na mwenye maadili japo si lazima awe wa dini au imani unayoamini wewe. Kwa hiyo una wajibu wa kujifunza maadili sana sana ili upone kifkra
 
= kihoro

Unayosema ni kweli kabisa wala sikatai, jee wewe kwanini unakataa kuwa chaadema wana uhusiano na chama CDU ya Ujerumani? hebu niandikie kireuf cha CDU.
 
Mmmmmmmm....!! Hapo penkundu hapakuhusu kweli, ila pia unaweza usilelewe kuwa panakuhusu.....!!

Naona umekuja na povu, punguza kiherehere. Jisomee kama huna uelewa huo:

...............................................
 
Tatizo lako ni moja na litakupa kiholo sana hadi utaugua magonjwa ya ajabu, unapenda sana kuwaangalia watu kwa macho ya kidini. Halina tija hili ni upuuzi mtupu, achana nalo, wa dini au imani yako anaweza akawa mwizi, msaliti, mwongo, mzinzi, muuaji, jambazi, na akakudhuru na wewe pia kinyume na mwenye maadili japo si lazima awe wa dini au imani unayoamini wewe. Kwa hiyo una wajibu wa kujifunza maadili sana sana ili upone kifkra

Achana na hao Agents of Devils...thread haihusu uislam wala ukristo..
 
= kihoro

Unayosema ni kweli kabisa wala sikatai, jee wewe kwanini unakataa kuwa chaadema wana uhusiano na chama CDU ya Ujerumani? hebu niandikie kireuf cha CDU.

=je
=chadema
=ebu
=kirefu
=chama cha CDU

Hivi yangu yalikuwa mangapi vile??

Pia, unaweza kunikumbusha ni wapi nimekataa kuwa chaadema wana uhusiano na chama CDU ya Ujerumani? Japo sina hakika sana kama chaadema ndo ile ninayoifahamu mimi kama chadema.
 
ni usiri wa kijinga au ndo uongo wa mwigulu mana huyu mheshimiwa naye ni muongo aliyebobea nikikumbuka ushaidi wa mbinguni aliousema bungen juu ya ugaid sina iman naye!!mambo magum majbu mepesi hajasema kiasi gan!!politics tu za kujifarij

Juzi katoka kwa nabii tb Joshua huo uongo mnamsingizia wajemeni
 
Hawa wahisani wapuuzi na gazeti la nipashe na kipuuzi hatutaki misaada ya wahisani tunajiweza.
 
Si umeshajaza mabox ya hela kwako halafu unatibiwa india pia na watoto wako wanasomea huko huko kwa wahisani sasa huwezi wahitaji wewe ila sisi tunaotibiwa mwananyamala tunawahitaji sana...
 
Chadema wameacha kupokea msaada kutoka chama cha siasa cha kikristo cha Ujerumani?

Hiyo post haina uhusiano na mada iliyopo mezani. Tunazungumzia misaada ya wafadhiri inayochangia katika bajeti siyo misaada ya chama kimoja kimoja ambayo haina mchango wowote katika bajeti ya taifa
 
Si umeshajaza mabox ya hela kwako halafu unatibiwa india pia na watoto wako wanasomea huko huko kwa wahisani sasa huwezi wahitaji wewe ila sisi tunaotibiwa mwananyamala tunawahitaji sana...
Mkuu fisadi ni mengi alikuwa anagawa pesa huwahonga wabunge kumkomoa muhongo lakini tushamjua kuwa mengi ni tapeli pamoja na nyie vibaraka wake mafisadi nyie.
 
Shida sio kutegemea misaada, shida ni namna tunavyotumia pesa zetu na uwajibikaji wa watumishi wetu. Kulaumu wahisani nadhani ni upungufu wa uchambuzi wa kiini cha tatizo. Kwa maelezo na mtazamo wa Nchemba ni kama tatizo ni kustisha misaada kulikofanywa na wahisani na sio vitendo vya ufisadi vilivyofanywa na maafisa wa serikali na hatua legelege zinazochukuliwa na serikali ili kuwawajibisha wahusika.
Nchi wahisani, serikali zao, afisa akituhumiwa tu huchukuliwa hatua mara moja bila hata kusubiri Bunge kuilazimisha serikali. Hii ndiyo sababu mojawapo ya kuwa na maendeleo yayoziwezesha serikali hizi kuwa na pesa za kutupatia misaada. Sisi masikini tunaacha kusimamia vizuri rasilimali zetu huku tukitembeza bakuli na kuwalaumu wahisani. Ingalikuwa busara kama angesema serikali yetu inapaswa kusimamia vizuri rasilimali zetu ili tuweze kuwa fedha za maendeleo, kigezo kisiwe kwa sababu wahisani hawatupi misaada, kiigezo kiwe ni kiu ya maendeleo, uadilifu na uwajibikaji. Kazi kuwabana watumishi mafisadi ilipaswa kufanywa na wananchi wenyewe kupitia sanduku la kura. Inashangaza watu na akili zetu tunawachekea mafisadi na kuwachukia wahisani wanaosaidia kufanya kazi iliyopaswa kufanywa serikali, Bunge na wananchi. Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha ana akili finyu na uchambuzi finyu wa kujua kiini cha tatizo. Wahisani wanajua washike wapi ili serikali iwajibike, sisi hatujui penye shida ni wapi
Wizaraya Fedha imesema hatua za awali zilizoanza kuchukuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia maazimio ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 3000 katika akaunti ya Tegeta Escrow zimewezesha wahisani kuanza kutoa misaada waliyokuwa wamesitisha.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, alisema hayo jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One. Nchemba alisema katika nusu ya mwaka wa kalenda wa fedha kulikuwa na changamoto nyingi ikiwamo wahisani kusitisha misaada yao kwa Tanzania kusubiri maamuzi yaliyotolewa na Bunge kuhusiana na sakata la Tegeta Escrow.

Alisema uamuzi uliochukuliwa na wahisani kusitisha misaada kwa Tanzania kwa muda ni fundisho kwamba kama nchi tunahitaji kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kuwa na kujenga misingi ya kujitegemea. “Kama Taifa tuanze misingi ya kujitegemea, tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo halafu unategemea fedha za wahisani ni tatizo,” alisema.

Nchemba alisema kutegemea wahisani ni tatizo ambalo nchi inabidi kujipanga kuondokana nalo kwani hali hiyo inakwamisha miradi kuchelewa kutekelezwa wahisani wanaposhindwa kuleta fedha kwa wakati. Wahisani wanaosaidia bajeti ya Tanzania ni pamoja na African Development Bank (AfDB), Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Germany, Ireland, Japan, Norway, Sweden, Uingereza na Benki ya Dunia. Benki ya Dunia na wahisani wengine kwa muda sasa wamekuwa wakisaidia katika miradi mingi ya ujenzi yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 230.

Mwishoni mwa mwaka jana, Marekani ilibainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo. Taarifa iliyotolewa na Desemba mwaka jana na ubalozi wa Marekani nchini ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.

CHANZO: NIPASHE

[/QUOTE...akili ndongo!kila siku wanaota misaada tu.......hii shida itaondolewa na ukawa tu.......mwaisho wa vijimsaada vya kipumbavu ni october 2015
 
Masikini hata raisi Mhe. Prof Dkt. Jakaya Kikwete hajui ni kwanini nchi yetu ni masikini hata baada ya Kuwa na rasilimali za kutosha.
 
Hiyo post haina uhusiano na mada iliyopo mezani. Tunazungumzia misaada ya wafadhiri inayochangia katika bajeti siyo misaada ya chama kimoja kimoja ambayo haina mchango wowote katika bajeti ya taifa

= wafadhili

Hivi hujuwi kuwa hata Serikali ya Ujerumani inayoongozwa na chama hicho hicho cha Kikristo inachangia bajeti ya Tanzania? kafanye homework yako.
 
Wizaraya Fedha imesema hatua za awali zilizoanza kuchukuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia maazimio ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 3000 katika akaunti ya Tegeta Escrow zimewezesha wahisani kuanza kutoa misaada waliyokuwa wamesitisha.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, alisema hayo jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One. Nchemba alisema katika nusu ya mwaka wa kalenda wa fedha kulikuwa na changamoto nyingi ikiwamo wahisani kusitisha misaada yao kwa Tanzania kusubiri maamuzi yaliyotolewa na Bunge kuhusiana na sakata la Tegeta Escrow.

Alisema uamuzi uliochukuliwa na wahisani kusitisha misaada kwa Tanzania kwa muda ni fundisho kwamba kama nchi tunahitaji kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kuwa na kujenga misingi ya kujitegemea. “Kama Taifa tuanze misingi ya kujitegemea, tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo halafu unategemea fedha za wahisani ni tatizo,” alisema.

Nchemba alisema kutegemea wahisani ni tatizo ambalo nchi inabidi kujipanga kuondokana nalo kwani hali hiyo inakwamisha miradi kuchelewa kutekelezwa wahisani wanaposhindwa kuleta fedha kwa wakati. Wahisani wanaosaidia bajeti ya Tanzania ni pamoja na African Development Bank (AfDB), Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Germany, Ireland, Japan, Norway, Sweden, Uingereza na Benki ya Dunia. Benki ya Dunia na wahisani wengine kwa muda sasa wamekuwa wakisaidia katika miradi mingi ya ujenzi yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 230.

Mwishoni mwa mwaka jana, Marekani ilibainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo. Taarifa iliyotolewa na Desemba mwaka jana na ubalozi wa Marekani nchini ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.

CHANZO: NIPASHE

[/QUOTE...akili ndongo!kila siku wanaota misaada tu.......hii shida itaondolewa na ukawa tu.......mwaisho wa vijimsaada vya kipumbavu ni october 2015

Kaangalie karatu, jimbo la cdm. Jinsi wanavyofisadi! Wote walewale tu, mama yao mmoja matumbo mbalimbali.
 
Back
Top Bottom