Nchemba: Wahisani wamerejesha misaada

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,423
Wizara ya Fedha imesema hatua za awali zilizoanza kuchukuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia maazimio ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow zimewezesha wahisani kuanza kutoa misaada waliyokuwa wamesitisha.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, alisema hayo jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One.

Nchemba alisema katika nusu ya mwaka wa kalenda wa fedha kulikuwa na changamoto nyingi ikiwamo wahisani kusitisha misaada yao kwa Tanzania kusubiri maamuzi yaliyotolewa na Bunge kuhusiana na sakata la Tegeta Escrow.

Alisema uamuzi uliochukuliwa na wahisani kusitisha misaada kwa Tanzania kwa muda ni fundisho kwamba kama nchi tunahitaji kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kuwa na kujenga misingi ya kujitegemea. "Kama Taifa tuanze misingi ya kujitegemea, tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo halafu unategemea fedha za wahisani ni tatizo," alisema.

Nchemba alisema kutegemea wahisani ni tatizo ambalo nchi inabidi kujipanga kuondokana nalo kwani hali hiyo inakwamisha miradi kuchelewa kutekelezwa wahisani wanaposhindwa kuleta fedha kwa wakati.

Wahisani wanaosaidia bajeti ya Tanzania ni pamoja na African Development Bank (AfDB), Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Germany, Ireland, Japan, Norway, Sweden, Uingereza na Benki ya Dunia. Benki ya Dunia na wahisani wengine kwa muda sasa wamekuwa wakisaidia katika miradi mingi ya ujenzi yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 230.

Mwishoni mwa mwaka jana, Marekani ilibainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Desemba mwaka jana na ubalozi wa Marekani nchini ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.


CHANZO:
NIPASHE
 
 
wametoa kiasi gani?ccm kwa uongo siwawezi...hakuna msaada wowote mpaka aseme ni nchi gani na kiasi gani kimetolewa,..nasubiri wafadhili wakanushe.
 
wametoa kiasi gani?ccm kwa uongo siwawezi...hakuna msaada wowote mpaka aseme ni nchi gani na kiasi gani kimetolewa,..nasubiri wafadhili wakanushe.
Wafadhili hawawezi kukanusha huu utumbo.
Waandishi wa habari nao ni shida ingine......kwanini hawakumuuliza specifically how much and from which countries/or institutions?

Takataka hizi tbu kweli.
 
akili ndongo!kila siku wanaota misaada tu.......hii shida itaondolewa na ukawa tu.......mwaisho wa vijimsaada vya kipumbavu ni october 2015

Chadema wameacha kupokea msaada kutoka chama cha siasa cha kikristo cha Ujerumani?
 
Chadema wameacha kupokea msaada kutoka chama cha siasa cha kikristo cha Ujerumani?
Mbona unashusha hadhi yako kiasi hicho! Hivi CDM ndiyo inayoiongoza serikali yako sikivu hadi iwe haki kwao kufanya kila lifanywalo na CDM?!
 

Sidhani kama fundisho hapa ni kujenga misingi ya kujitegemea...
Fundisho hapa ni viongozi wawe waadilifu na kuacha ufisadi... simple.
 
kila nikimuona Mugulu mchemba au nikimsikia nakumbuka bomu la soweto Arusha kwa kweli aliyoyafanya Mugulu lazima yatalipwa na serikali yeyote ile itakayochukua madaraka tofauti na ccm
 
Mkuu salama hupatikani kwa simu
Ushauri wako tumeusikia ila maagizo yako tumeyakataa
 
Hii habari si ya kweli kwani hakuna habari yeyote ile kutoka kwa wafadhili kwamba wameamua kutoa misaada tena. Hii ni tofauti na pale walipositisha misaada ambapo walitoa habari hizo kwenye vyombo vya habari.

UK and international donors suspend Tanzania aid after corruption claims | Global development | The Guardian

Tanzania May Delay Development Projects as Donors Withhold Aid - Bloomberg

Corruption in Tanzania: President's men took over, Norwegian aid money disappeared | REDD-Monitor

Hebu jaribu kutafuta kwenye google 'international donors resume aid to Tanzania' kama utapata jibu!
 
Shida kubwa ni waandishi wa Tz, huwa hawaendi deep. Wao kazi yao kupokea taarifa yoyote bila kuhoji wala nini. Ndio maana rais Ben Mkapa alikuwa anawadharau sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…