Nchemba: Wahisani wamerejesha misaada

Nchemba: Wahisani wamerejesha misaada

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,423
Wizara ya Fedha imesema hatua za awali zilizoanza kuchukuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia maazimio ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow zimewezesha wahisani kuanza kutoa misaada waliyokuwa wamesitisha.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, alisema hayo jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One.

Nchemba alisema katika nusu ya mwaka wa kalenda wa fedha kulikuwa na changamoto nyingi ikiwamo wahisani kusitisha misaada yao kwa Tanzania kusubiri maamuzi yaliyotolewa na Bunge kuhusiana na sakata la Tegeta Escrow.

Alisema uamuzi uliochukuliwa na wahisani kusitisha misaada kwa Tanzania kwa muda ni fundisho kwamba kama nchi tunahitaji kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kuwa na kujenga misingi ya kujitegemea. "Kama Taifa tuanze misingi ya kujitegemea, tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo halafu unategemea fedha za wahisani ni tatizo," alisema.

Nchemba alisema kutegemea wahisani ni tatizo ambalo nchi inabidi kujipanga kuondokana nalo kwani hali hiyo inakwamisha miradi kuchelewa kutekelezwa wahisani wanaposhindwa kuleta fedha kwa wakati.

Wahisani wanaosaidia bajeti ya Tanzania ni pamoja na African Development Bank (AfDB), Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Germany, Ireland, Japan, Norway, Sweden, Uingereza na Benki ya Dunia. Benki ya Dunia na wahisani wengine kwa muda sasa wamekuwa wakisaidia katika miradi mingi ya ujenzi yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 230.

Mwishoni mwa mwaka jana, Marekani ilibainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Desemba mwaka jana na ubalozi wa Marekani nchini ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.


CHANZO:
NIPASHE
 
Wizaraya Fedha imesema hatua za awali zilizoanza kuchukuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia maazimio ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 3000 katika akaunti ya Tegeta Escrow zimewezesha wahisani kuanza kutoa misaada waliyokuwa wamesitisha.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, alisema hayo jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One. Nchemba alisema katika nusu ya mwaka wa kalenda wa fedha kulikuwa na changamoto nyingi ikiwamo wahisani kusitisha misaada yao kwa Tanzania kusubiri maamuzi yaliyotolewa na Bunge kuhusiana na sakata la Tegeta Escrow.

Alisema uamuzi uliochukuliwa na wahisani kusitisha misaada kwa Tanzania kwa muda ni fundisho kwamba kama nchi tunahitaji kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kuwa na kujenga misingi ya kujitegemea. "Kama Taifa tuanze misingi ya kujitegemea, tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo halafu unategemea fedha za wahisani ni tatizo," alisema.

Nchemba alisema kutegemea wahisani ni tatizo ambalo nchi inabidi kujipanga kuondokana nalo kwani hali hiyo inakwamisha miradi kuchelewa kutekelezwa wahisani wanaposhindwa kuleta fedha kwa wakati. Wahisani wanaosaidia bajeti ya Tanzania ni pamoja na African Development Bank (AfDB), Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Germany, Ireland, Japan, Norway, Sweden, Uingereza na Benki ya Dunia. Benki ya Dunia na wahisani wengine kwa muda sasa wamekuwa wakisaidia katika miradi mingi ya ujenzi yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 230.

Mwishoni mwa mwaka jana, Marekani ilibainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo. Taarifa iliyotolewa na Desemba mwaka jana na ubalozi wa Marekani nchini ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.

CHANZO: NIPASHE


[/QUOTE...akili ndongo!kila siku wanaota misaada tu.......hii shida itaondolewa na ukawa tu.......mwaisho wa vijimsaada vya kipumbavu ni october 2015
 
wametoa kiasi gani?ccm kwa uongo siwawezi...hakuna msaada wowote mpaka aseme ni nchi gani na kiasi gani kimetolewa,..nasubiri wafadhili wakanushe.
 
wametoa kiasi gani?ccm kwa uongo siwawezi...hakuna msaada wowote mpaka aseme ni nchi gani na kiasi gani kimetolewa,..nasubiri wafadhili wakanushe.
Wafadhili hawawezi kukanusha huu utumbo.
Waandishi wa habari nao ni shida ingine......kwanini hawakumuuliza specifically how much and from which countries/or institutions?

Takataka hizi tbu kweli.
 
akili ndongo!kila siku wanaota misaada tu.......hii shida itaondolewa na ukawa tu.......mwaisho wa vijimsaada vya kipumbavu ni october 2015

Chadema wameacha kupokea msaada kutoka chama cha siasa cha kikristo cha Ujerumani?
 
Chadema wameacha kupokea msaada kutoka chama cha siasa cha kikristo cha Ujerumani?
Mbona unashusha hadhi yako kiasi hicho! Hivi CDM ndiyo inayoiongoza serikali yako sikivu hadi iwe haki kwao kufanya kila lifanywalo na CDM?!
 

Alisema uamuzi uliochukuliwa na wahisani kusitisha misaada kwa Tanzania kwa muda ni
fundisho kwamba kama nchi tunahitaji kujenga misingi ya kujitegemea. "Kama Taifa tuanze misingi ya kujitegemea, tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo halafu unategemea fedha za wahisani ni tatizo," alisema.


Sidhani kama fundisho hapa ni kujenga misingi ya kujitegemea...
Fundisho hapa ni viongozi wawe waadilifu na kuacha ufisadi... simple.
 
kila nikimuona Mugulu mchemba au nikimsikia nakumbuka bomu la soweto Arusha kwa kweli aliyoyafanya Mugulu lazima yatalipwa na serikali yeyote ile itakayochukua madaraka tofauti na ccm
 
Mkuu salama hupatikani kwa simu
Naleta uzi jukwaani baada ya kuona uzi wa MwanaDiwani jana (https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=784297) ukieleza jinsi umatu wa wanabumbuli huko Tanga walivyojitokeza katika mkutano.
Nimpongeze Nape na Kinana kwa ziara nzuri zinazoitwa za kujenga chama vijijini ( Japo mimi naamini ni za kukiua chama - nitaeleza sababu).
Pili Nimekuwa nikijiuliza JE NI KWELI NAPE NA KINANA HAWAJAJUA SABABU ZA WANANCHI WENGI KUHUDHURIA MIKUTANO YAO AU WANATUZUGA? NA KAMA WANATUZUGA - JE WANAMFARIJI NANI JUU JA HILI?
Sababu zinazowafanya watanzania kuhushuri mikutano zilizo wazi ni
1) Viongozi wa chama ni lazima wahudhurie. Hawana option ya kuchagua hata kama hawako tayari. Tumeona mpaka ma DC na DED wakilazimika kuambatana na ziara. Hivyo hili Nape / Kinana halijui?
2. Wenye shida mbalimbali kuja kusikiliza kuna nini kipya cha kutatua shida zao? Huu ni mfano wa wahudhuriaji wengi waliojitokeza Huko Bumbuli kujua msimamo juu ya kiwanda na chai zao, Mtwara mjini kujua uhalisia wa gesi inavyotoka, Singida mashariki (Kwa Lissu) kujua hatima ya mgodi wa sagharu, Mwanza - kujuona ahadi ya meli kubwa iliyoahidiwa na JK. n.k. wengine mtasaidia kuainisha maeneo na sababu.
3) Masikini wanaofuata mgao wa kanga, T shirt, mafuta ya bodaboda / bajaji, ubwabwa n.k ambo husombwa na malori. Ifahamike kuwa wahudhuriaji hawa wengi huwa hawana dhamira za zati kuja kusikiliza ndio maana bila usafiri hawaji au hivyo vitakrima hawaji.
Hapa unaweza tofautisha na wahudhuriaji wa mikutano ya vyama pinzani. Hakuna mtu hata mmoja anaegharamiwa usafiri ili kufika uwanjani bali wanaenda kwa nia ya kusikiliza sera na mikakati ya wapinzani.
4) Uhamasishwaji wa wanachama na wananchi juu ya kuhudhuria mikutano unaofanywa mtaa kwa mtaa. Hivyo wengi wanakuja kwa kuwa wainekane na kiongozi wao wa mtaa kuwa walihudhuria na si matakwa yao toka moyoni kuhudhuria.
5) kundi kubwa la wafanyabiashara na baadhi ya viongozi/ watumishi wa umma kufika kwa ajili ya kulinda maslahi binafi katika kazi zao. Kama inavyofahamika kuwa ukijiweka wazi wazi kuwa uko uponzani basi hata kabiashara kako kataandamwa, kila kukicha polisi wako na wewe na makosa ya kubambikwa. Hivyo kinafiki lazima walete nyuso ila ktk nafsi sio.
Sasa hizi sababu zote ina maana Nape na Kinana hawazijui au wanatuzuga? Je wanatudanganya sisi wananchi au wanajidanganya nafsi zai?

Pia nilisemaziara ni za kukiuwa chama sababu
1. Wananchi wanaenda kusikiliza nini chama kinataka kusema juu ya shida zao. Hotuba hujikita kulaumu zaidi utendaji mbovu wa serikali ambayo ni ya CCM, kuponda wapinzani kuwa hawataleta maendeleo hali ya kuwa CCM ina miaka zaidi ya 50 ikiwa hijafanya vya kutosha kushawishi wananchi. Upinzani kuleta machafuko hali ya kuwa wananchi wanashuhudia machafuko yakianzishwa na aidha vyombo vya dola au na wanaCCM mbele ya vyombo vya dola bila hatua stahiki kuchukuliwa.
2. Wananchi wanahitaji kuambiwa ni hatua gani zimechukuliwa na chama juu ya wafuja uchumi. Kitu ambacho chama chenyewe kuonyesha kimeshindwa kuwawajibisha wahisika na kimeamua kujiunga nao kuendeleza uhujumu.
Hivyo kwa hotuba hizi chama kitazidi kudidimia tu ikilinganishwa na kabla ya ziara ambapo wananchi8 walikuwa "undecided"
Niishie kwa kusema CCM inajichimbia kaburi lake kwa ziara zake.

Ushauri wako tumeusikia ila maagizo yako tumeyakataa
 
Hii habari si ya kweli kwani hakuna habari yeyote ile kutoka kwa wafadhili kwamba wameamua kutoa misaada tena. Hii ni tofauti na pale walipositisha misaada ambapo walitoa habari hizo kwenye vyombo vya habari.

UK and international donors suspend Tanzania aid after corruption claims | Global development | The Guardian

Tanzania May Delay Development Projects as Donors Withhold Aid - Bloomberg

Corruption in Tanzania: President's men took over, Norwegian aid money disappeared | REDD-Monitor

Hebu jaribu kutafuta kwenye google 'international donors resume aid to Tanzania' kama utapata jibu!
 
Shida kubwa ni waandishi wa Tz, huwa hawaendi deep. Wao kazi yao kupokea taarifa yoyote bila kuhoji wala nini. Ndio maana rais Ben Mkapa alikuwa anawadharau sana..
 
Back
Top Bottom