MAGAMBA MATATU
JF-Expert Member
- Jul 2, 2011
- 646
- 1,174
Na Jumbe Ismailly, Singida
MBUNGE wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM) anatarajia kuwasilisha hoja binafsi katika Bunge lijalo la bajeti kupendekeza kuanzishwa kwa Baraza Maalumu la kushughulikia makosa ya rushwa na uhalifu uchumi.
Nchemba alisema kumekuwepo wimbi kubwa la kushuka kwa maadili ya uongozi, hali inayochangia kwa namna moja au nyingine wananchi kupinga vitendo vya rushwa na hujuma nyingine zinazohusiana na mali za umma.
Alisema kutokana na ukubwa wa wimbi hilo, ameona ni vema likaanzishwa baraza hilo ambalo litashughulikia kesi za aina hiyo.
Nchemba ambaye pia ni Katibu wa Uchumi wa CCM Taifa, alibainisha sababu za mapendekezo hayo kuwa ni mazingira ya kusikiliza kesi hizo, kukwamisha ufanisi katika kuzishughulikia kesi hizo.
Alivitaja baadhi ya vitu vinavyokwamisha kuwa ni msongamano wa kesi mahakamani zinazohusu rushwa na uhujumu uchumi, kwani huchangia pia hata kesi za kitaifa kupangiwa sawa na kesi nyingine kitendo kinachochelewesha kumalizika kwake.
Je Nchemba yeye ni safi? Ule uchaguzi wa Igunga je, atabaki kama hoja ikipitishwa na ikafanya kazi bila zengwe?