Nchemba kupeleka hoja ya rushwa bungeni, je yeye ni msafi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchemba kupeleka hoja ya rushwa bungeni, je yeye ni msafi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGAMBA MATATU, Jun 8, 2012.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Na Jumbe Ismailly, Singida

  MBUNGE wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM) anatarajia kuwasilisha hoja binafsi katika Bunge lijalo la bajeti kupendekeza kuanzishwa kwa Baraza Maalumu la kushughulikia makosa ya rushwa na uhalifu uchumi.

  Nchemba alisema kumekuwepo wimbi kubwa la kushuka kwa maadili ya uongozi, hali inayochangia kwa namna moja au nyingine wananchi kupinga vitendo vya rushwa na hujuma nyingine zinazohusiana na mali za umma.

  Alisema kutokana na ukubwa wa wimbi hilo, ameona ni vema likaanzishwa baraza hilo ambalo litashughulikia kesi za aina hiyo.

  Nchemba ambaye pia ni Katibu wa Uchumi wa CCM Taifa, alibainisha sababu za mapendekezo hayo kuwa ni mazingira ya kusikiliza kesi hizo, kukwamisha ufanisi katika kuzishughulikia kesi hizo.

  Alivitaja baadhi ya vitu vinavyokwamisha kuwa ni msongamano wa kesi mahakamani zinazohusu rushwa na uhujumu uchumi, kwani huchangia pia hata kesi za kitaifa kupangiwa sawa na kesi nyingine kitendo kinachochelewesha kumalizika kwake.


  Je Nchemba yeye ni safi? Ule uchaguzi wa Igunga je, atabaki kama hoja ikipitishwa na ikafanya kazi bila zengwe?
   
 2. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Du..........! Hivi huyu mnyiramba mbona ana vituko sana? Yy mwenyewe ni mla rushwa za kampeni alafu apeleke hii hoja bungeni?
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Si mbaya kama tukielewa kwa undani msingi na namna anavyopendekeza baraza hilo litakavyojengwa
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Rushwa zake za ngono pia zitaundiwa baraza? Au ni hilohilo? Kamtia mimba mwandishi mmoja Meru halafu kaikataa bazazi huyu
   
 5. g

  greenstar JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mtoa maada unaonekana wewe ni shabiki wa chama cha upinzani usiye na mtazamo chanya...kwani wabunge wa CCM hawanauwezo wakufanya mema?

  kumbuka kamati teule zote zimekuwa zikiongozwa na wabunge wa CCM na kufanikiwa kuiwajibisha serikali pale inapokosea......Kama wewe unamawazo finyu usiingie na sera zako za kishabiki kama wanaCHADEMA....CCM ni chama chenye mtazamo na malengo ya dhati kuleta maisha bora na kuinua uchumi wetu....Mafisadi watang'olewa,magamba watahamia CHADEMA ,CCM safi itadumu na kuimarika kila siku.

  Opereshini za CHADEMA ndizo zitatuinua zaidi katika kuwawajibisha mafisadi na magamba
   
 6. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hivi kwa sasa tuna mabaraza mangapi? Je yanatusaidia nini? Pamoja na hayo, Raisi ana mamlaka gani na kwa nini hayatumii hapa? Kama tunataka kuanzisha baraza je bajeti itatoka wapi? Naulizi hivi kwa sababu kinachofanya mahakama ishindwe kufanya kazi kwa wakati ni kutokana na ufinyu wa bajeti. Sasa hilo baraza litaongozwa na volunteers siyo? Kwa nini tunafikiri kama tuna nazi vile? Hivi kama unakwenda Dar ukitokea Dodoma na umeishiwa na mafuta Dakawa, utakwenda kununua gari jingine au kununua mafuta ya kuliwezesha hilo lililoishiwa mafuta Dakawa?
  Nchemba akisema kuna mtu kamwambia waanzishe baraza ili apate ulaji hapo sawa. Lakini hoja hii haina mashiko na haina tija kwa taifa. CCM ni sifuri yaani "O" hapa duniani mpaka mbinguni!
   
 7. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe ndo huyu mzinzi mwenyewe au wewe ni id nyingine ya nape?
   
 8. josam

  josam JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 1,754
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Mlangaja, naunga mkono 500% maoni yako!
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kesi nyingi zinalundikana mahakamani kwa sababu Mahakama kama mhimili mmojawapo wa dola haina fedha. Wana madeni makubwa na kila wakiomba fedha serikalini wanapata pungufu. Sasa kama serikali inashindwa kuhudumia mahakama kwa sasa watawezaje kuhudumia hili baraza analopendekeza Nchemba?

  Huku ni kupoteza hela za walipa kodi.
   
 10. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ile haliyowasilisha Makamba kuhusu Nyumba za kupanga ilifikia wapi?isije ikawa ni kutangaza nia kila siku Sendeka naye alisema atawasilisha kuhusu Nyumba za Serikali zilizouzwa.!

  Mytake: Naona imekuwa Fashion sasa unapokuwa ujasikika muda mrefu au unataka umaarufu kupeleka hoja binafsi bungeni.
   
 11. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Huyu Jamaa Mwigulu ni Kama tu anatupumbaza sisi wananchi.Kama ni maadili ya uongozi yeye ni mchafu,mnakumbuka alivyoshirikiana na Lusinde a.k.a kibajaji kuporomosha matusi ktk uchaguzi wa Arumeru Mashariki!!?
   
 12. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Kamata mwizi men!hivi kesi yake ya kugawa rushwa kanisani kwenye uchaguzi wa arumeru iliishaje?shetani kweli kaamua huu mwaka tutashuudia vituko vingi sana
   
 13. Mwigulu Nchemba

  Mwigulu Nchemba Verified User

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 756
  Trophy Points: 180
  Greenstar siku chadema wakinisifia na shetani atamsifu mungu wala usihangaike nawo
   
 14. fige

  fige JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2012
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku zote nawashangaa sana ccm kwani ajenda yenu ni cdm na si vita dhidi ya ufisadi.Kumbukeni kuwa vyama vinaweza kufa lakini harakati za ukombozi haziwezi kukoma.
  CCM na ife tu
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mwigulu mwana wa nchemba unataka kusifiwa?
  ULIOMBA KAZI ILI USIFIWE AU UTIMIZE WAJIBU WAKO?
  KWA ULIYOFANYA IGUNGA NA ARUMERU MASHARIKI WOTE TUMEYAONA NA KUYASIKIA.
  MIMI NITAKUSIFU SIKU HUKUMU YA UBUNGE WA IGUNGA IKIAMULIWA.
   
 16. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  Duh, ndugu yangu naona una hasira kwelikweli....Kimsingi kama anakusudia kuleta hoja hiyo ni sawa, wacha tuisubiri kwa kuwa pengine itatoa unafuu kwa mahakama zetu kupunguza rundo la kesi. Lakini sina hakika kama uchambuzi wa kwa nini baraza lisikilize kesi hizo badala ya mahakama utakaa sawasawa. Pili sina hakika kama Nchemba amelenga rushwa ya fedha akaacha nyingine kama ngono, vito vya thamani, magari nk. Ila umeniacha hoi hapo kwenye red.
   
 17. Mwigulu Nchemba

  Mwigulu Nchemba Verified User

  #17
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 756
  Trophy Points: 180
  Ringo sijataka kusifiwa ila nilitegemea ambaye hajeelewa aulize. Hilo la wajibu ndio ninalofanya badala ya kulenga kwenye hilo unasema mara meru mara igunga. Igunga hakuna jipya hapo Dr kafum ndiye mbunge wa igunga. Hayo ya kusikia utasikia sana na haya hayakuwa ya kwanza. Hata kwetu yapo
   
 18. d

  dguyana JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juz tulisikia ritz kuwa yupo tayari PCCB kumchunguza. Leo mwigulu Du!! Kuna kitu nyuma ya hili.

  M4C kweli kiboko.
   
 19. F

  FJM JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuna tofauti kubwa sana kati ya kupiga kelele na kuwajibisha. Kwa muda mrefu wabunge wa CCM wamekuwa wanapiga kelele na hata wao wenyewe wamekiri hivyo (pitia HANSARD za bunge), lakini mambo bado yamebakia kuwa vile vile. Na hili limewezekana tu kwa sababu serikali ya CCM ilijuwa udhaifu wa wabunge wake.

  Kwa sasa wabunge hao wamepatwa na hofu, wamekumbana na hasira za wananchi ambao kwa miaka nenda miaka rudi wamekuwa wakiangalia sinema za kupiga kelele bungeni. Ni kwa sababu hiyo tumeona wabunge wa CCM wakikesha kwenye vikao vya ndani (party caucuses) wakifukuzana maana wamejua waangalia sinema wamechoka.

  Anachofanya Nchemba ni juhudi ya kuokoa chama chake cha CCM. Ni jambo jema lakini kama nilivyosema, kama serikali inashindwa kutoa hela ya kutosha kuendesha mahakama, watapata wapi hela kwa hiki chombo cha nyongeza anachopendekeza Nchemba? Mimi nilidhani badala ya kuwa na chombo kingine, Nchemba angepeleka hoja binafsi inayoweka muda maalum wa kushughulikia kesi ya rushwa. Sheria iseme kabisa kesi ya rushwa lazima imalizike within x number of weeks, or months etc lakini sio kuwana kesi za miaka kama ile ya Prof Mahalu. Kwa mtindo huo lazima tutakuwa na mlundikano wa kesi.

  Pia Nchemba angependekeza kuwe na mfuko maalum wa kushughulikia gharama za kesi za rushwa. Na mwisho TAKUKURU ifumuliwe na kuundwa upya.
   
 20. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CCM ndio wala rushwa na ushahidi mmoja wao kakamatwa Live anachukua mlungula. Leo hii Mwigulu aliyekutwa anahonga kanisani Arumeru aje na hoja ya kuzuia rushwa!! Labda kama ni kuipamba rushwa...
   
Loading...