Nchemba: CCM haiwategemei walimu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,865
1,225
[h=2][/h]JUMANNE, MEI 22, 2012 05:42 NA ABDALLAH AMIRI, NZEGA

KATIBU wa Fedha na Uchumi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba, amesema CCM ni chama kikubwa hakiwezi kutetereka na kutegemea walimu ili kishinde chaguzi.

Nchemba aliyasema hayo jana wakati akitoa ushahidi wa upande wa mdaiwa katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM). Kesi hiyo ilifunguliwa na Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Kashindye.

Akitoa ushahidi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mjini Nzega, Nchemba ambaye pia Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), alikanusha tuhuma za kutoa rushwa kwa walimu katika eneo la Nkinga pamoja na kutoa lugha ya matusi katika baadhi ya mikutano ya kampeni.

Nchemba ambaye alikuwa Kiongozi Mkuu wa Kampeni za CCM, aliieleza Mahakama hiyo, kuwa chama hicho kilitenga Sh milioni 402 kwa ajili ya shughuli nzima ya kampeni.

Awali, Wakili wa Mlalamikaji, Profesa Abdallah Safari, alieleza Mahakama kuwa, September 16 mwaka jana, Nchemba alikutana na walimu na kuwashawishi waipigie kura CCM ili kukinusuru kisianguke pamoja na kuwagawia fedha walimu 70 katika eneo la Shule ya Msingi Nkinga iliyoko Igunga.

Akijibu hoja hiyo, Nchemba alikana kuhusika na utoaji wa pesa ndogo ndogo, kwa walimu hao na kusema kuwa yeye husaini hundi katika chama hicho.

“Mimi sihusiki na viji-petty cash, nahusika na kusaini akaunti kubwa, hivyo vijipetty cash vina wenyewe kama nilivyotaja hapo mwanzo,’’alisema Nchemba.

Kwa mujibu wa Nchemba, chama hicho hakiwezi kunusuliwa na kikundi cha walimu bali kinanusuliwa na wanachama wa CCM waliopo sehemu mbalimbali nchini wakiwamo wa Igunga.

‘’Huwezi kumpatia shetani neno la Mungu akahubiri, ni jambo ambalo ni gumu sana,” alisema Nchemba akiwalenga walimu kulingana na swali aliloulizwa na Profesa Safari.

Mwanzoni, Nchemba wakati akijitambulisha, alidai CCM ina fedha nyingi na yeye ni Bwana Fedha wa chama hicho, kauli ambayo ilisababisha wananchi waliofurika mahakamni hapo kuguna.

Hata hivyo, Jaji Mery Shangali anayesikiliza shauri hilo, alimtaka mbunge huyo kuheshimu Mahakama kwa kutotumia lugha zisizostahili.

Wakati huo huo Mahakama hiyo ilikataa ushahidi wa shahidi wa 18 ambaye ni Ofisa Mtendaji, Kata ya Igunga, Fedrick Magaka kutokana na shahidi huyo kuhudhuria baadhi ya vikao vya kesi hiyo. Kesi hiyo itaendelea leo.

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,865
1,225
Huyu Nchemba aliteuliwa Central Committee kuiua CCM? Chochote kinachotoka Mdomoni Mwake ni Utumbo na Matusi tu

Central Committee kutawaliwa na Vijana wasio na hekima ni hatari kweli kwa CCM; Waalimu Wawakosea Nini CCM?

Sababu ya Kudai Mishahara yao? Hapo ni Serikali ya CCM inatakiwa kujibu sio Chama cha CCM
 
agatony8l

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
453
170
Kwa kauli hizi, washangaa kama kuna umakini unachukuliwa wakati wa kuteua watu katika nafasi hizi muhimu. Kasha sahau kauli ya kutohitaji kura za wafanyakazi zilivyowaumiza mwaka 2010.
 
Lushinde

Member
Apr 25, 2012
11
0
Bahati yenu, siku ningeingia hapo kutoa ushahidi huyu Jaji angenitambua kuwa mimi ndio BAJAJI, kudadadeki.
 
samstevie

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
202
0
Walimu mpooo na mmesikia wwenyewe kwamba hawana mpango nanyi so hata wake zenu, waume zenu watoto na ngugu zenu wote hamuwezi kuimaliza ccm hamieni airtel shauriyenu siku nyingine watawakataa manesi na madaktari na kada nyinginezo watabaki polisi wao tu kwa lengo maalum.
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,768
2,000
Kauli hii ya Nchemba kwa walimu ni muhimu isambazwe kwa kasi ili waalimu wote wajue jinsi CCM inavyo "waheshimu" ili wachukue hatua muhimu.
 
Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,528
2,000
amuulize JK kauli yake kwa wafanyakazi kuwa hazitaki kura zao ilivomfanya 2010..
 
Eyoma

Senior Member
Sep 9, 2011
166
0
ama kweli.yaani leo hii walimu wamekuwa wakuwananga hivyo eti jamani,ebu walimu amkeni sasa kutoka usingizini.ukifika wakati wa uchaguzi mnakuwa almasi lakini kabla ya hapo hamna lolote hayaa.uliyemtoa tongotongo leo anakuzodoa.ngoja tusubiri tamko kla CWT taifa.
 
buyegiboseba

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
535
0
Waalimu kwa miaka mingi wamefanywa shamba la bibi,kutumika wakati wa kampeni,jamaa wakishinda wanawatosa hata madai yao ya msingi,lakini naamini walimu wanafikiri sawasawa hasa wale wa msingi wataamka usingizini.
 
andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
1,500
Hi tena kali, waalimu ni mashetani tena? hivi humu jamvini hakua mtu mwenye baba,mama,kaka,dada,shakazi, mjomba.nk ambaye ni mwalimu kwa sasa?
 
UNIQUE

Senior Member
Mar 31, 2011
180
0
Hata arumeru alikuwa anatukana. Lakini kama unavyojua arumeru siyo kama igunga waliwaonyesha. Hawa watoto hawana adabu hawajajua hata kunawa watakulaje meza kuu. Jk hivi jamani unashida gani? Kila unayemchagua feki
 
kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
17,498
2,000
CCM inawaonea sana waalim sijui kwa nini?yaani waalimu wa Tanzania ni kama kinda la kuku lililokosa mama,na CCM ni kama mwewe anawanyanya sana waaimu,
Nadhani sasa ni muda mwafaka wa kumkimbia mwewe CCM.
 
samora10

JF-Expert Member
Jul 21, 2010
7,569
2,000
ha ha ha haaaa CCM Bana wana maneno kweli sasa hivi kuna "Vijipetty cash" sio "vijisent" tena? kweli wamelewa madaraka hawa watu
 
AlamaZA NYAKATI

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
274
0
huyu fataki mwache tu aringe na kodi za watz kwa kuita vijipety cash kama mwenzake chenge siku si nyingi vitawatokea puani.....siku zao zinahesabika mbona...........M4C is near.
 
MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
620
1,000
JUMANNE, MEI 22, 2012 05:42 NA ABDALLAH AMIRI, NZEGA

KATIBU wa Fedha na Uchumi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba, amesema CCM ni chama kikubwa hakiwezi kutetereka na kutegemea walimu ili kishinde chaguzi.

Nchemba aliyasema hayo jana wakati akitoa ushahidi wa upande wa mdaiwa katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM). Kesi hiyo ilifunguliwa na Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Kashindye.

Akitoa ushahidi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mjini Nzega, Nchemba ambaye pia Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), alikanusha tuhuma za kutoa rushwa kwa walimu katika eneo la Nkinga pamoja na kutoa lugha ya matusi katika baadhi ya mikutano ya kampeni.

Nchemba ambaye alikuwa Kiongozi Mkuu wa Kampeni za CCM, aliieleza Mahakama hiyo, kuwa chama hicho kilitenga Sh milioni 402 kwa ajili ya shughuli nzima ya kampeni.

Awali, Wakili wa Mlalamikaji, Profesa Abdallah Safari, alieleza Mahakama kuwa, September 16 mwaka jana, Nchemba alikutana na walimu na kuwashawishi waipigie kura CCM ili kukinusuru kisianguke pamoja na kuwagawia fedha walimu 70 katika eneo la Shule ya Msingi Nkinga iliyoko Igunga.

Akijibu hoja hiyo, Nchemba alikana kuhusika na utoaji wa pesa ndogo ndogo, kwa walimu hao na kusema kuwa yeye husaini hundi katika chama hicho.

“Mimi sihusiki na viji-petty cash, nahusika na kusaini akaunti kubwa, hivyo vijipetty cash vina wenyewe kama nilivyotaja hapo mwanzo,’’alisema Nchemba.

Kwa mujibu wa Nchemba, chama hicho hakiwezi kunusuliwa na kikundi cha walimu bali kinanusuliwa na wanachama wa CCM waliopo sehemu mbalimbali nchini wakiwamo wa Igunga.

‘’
Huwezi kumpatia shetani(WALIMU) neno la Mungu akahubiri, ni jambo ambalo ni gumu sana,” alisema Nchemba akiwalenga walimu kulingana na swali aliloulizwa na Profesa Safari.

Mwanzoni, Nchemba wakati akijitambulisha, alidai CCM ina fedha nyingi na yeye ni Bwana Fedha wa chama hicho, kauli ambayo ilisababisha wananchi waliofurika mahakamni hapo kuguna.

Hata hivyo, Jaji Mery Shangali anayesikiliza shauri hilo, alimtaka mbunge huyo kuheshimu Mahakama kwa kutotumia lugha zisizostahili.

Wakati huo huo Mahakama hiyo ilikataa ushahidi wa shahidi wa 18 ambaye ni Ofisa Mtendaji, Kata ya Igunga, Fedrick Magaka kutokana na shahidi huyo kuhudhuria baadhi ya vikao vya kesi hiyo. Kesi hiyo itaendelea leo.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom