Nchemba: CCM haiwategemei walimu

Nchemba: CCM haiwategemei walimu

Mtukufu Rais alishasema hategemei kura za Wafanyakazi

Mjumbe wa CC, Mbunge wa Kuchaguliwa, Kijana, Msomi Pass with distinction Yeye kasema CCM haitegemie kura za Walimu

Sasa Waliobaki wanaomba Kura za Vijana, Wakulima Vijijini na Wafanya - biashara Wengi Wao Ni Fisadis
 
Hajui anasema nini.Masikitiko makubwa kwa CCM kuharibu ni rahisi lakini kukarabati ni ngumu.Tamko la Bw Fedha litawagharimu.
 
JUMANNE, MEI 22, 2012 05:42 NA ABDALLAH AMIRI, NZEGA


KATIBU wa Fedha na Uchumi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba, amesema CCM ni chama kikubwa hakiwezi kutetereka na kutegemea walimu ili kishinde chaguzi.

Nchemba aliyasema hayo jana wakati akitoa ushahidi wa upande wa mdaiwa katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM). Kesi hiyo ilifunguliwa na Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Kashindye.

Akitoa ushahidi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mjini Nzega, Nchemba ambaye pia Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), alikanusha tuhuma za kutoa rushwa kwa walimu katika eneo la Nkinga pamoja na kutoa lugha ya matusi katika baadhi ya mikutano ya kampeni.

Nchemba ambaye alikuwa Kiongozi Mkuu wa Kampeni za CCM, aliieleza Mahakama hiyo, kuwa chama hicho kilitenga Sh milioni 402 kwa ajili ya shughuli nzima ya kampeni.

Awali, Wakili wa Mlalamikaji, Profesa Abdallah Safari, alieleza Mahakama kuwa, September 16 mwaka jana, Nchemba alikutana na walimu na kuwashawishi waipigie kura CCM ili kukinusuru kisianguke pamoja na kuwagawia fedha walimu 70 katika eneo la Shule ya Msingi Nkinga iliyoko Igunga.

Akijibu hoja hiyo, Nchemba alikana kuhusika na utoaji wa pesa ndogo ndogo, kwa walimu hao na kusema kuwa yeye husaini hundi katika chama hicho.

“Mimi sihusiki na viji-petty cash, nahusika na kusaini akaunti kubwa, hivyo vijipetty cash vina wenyewe kama nilivyotaja hapo mwanzo,’’alisema Nchemba.

Kwa mujibu wa Nchemba, chama hicho hakiwezi kunusuliwa na kikundi cha walimu bali kinanusuliwa na wanachama wa CCM waliopo sehemu mbalimbali nchini wakiwamo wa Igunga.

‘’
Huwezi kumpatia shetani(WALIMU) neno la Mungu akahubiri, ni jambo ambalo ni gumu sana,” alisema Nchemba akiwalenga walimu kulingana na swali aliloulizwa na Profesa Safari.

Mwanzoni, Nchemba wakati akijitambulisha, alidai CCM ina fedha nyingi na yeye ni Bwana Fedha wa chama hicho, kauli ambayo ilisababisha wananchi waliofurika mahakamni hapo kuguna.

Hata hivyo, Jaji Mery Shangali anayesikiliza shauri hilo, alimtaka mbunge huyo kuheshimu Mahakama kwa kutotumia lugha zisizostahili.

Wakati huo huo Mahakama hiyo ilikataa ushahidi wa shahidi wa 18 ambaye ni Ofisa Mtendaji, Kata ya Igunga, Fedrick Magaka kutokana na shahidi huyo kuhudhuria baadhi ya vikao vya kesi hiyo. Kesi hiyo itaendelea leo.


Kweli ccm imeishiwa! Yaani waalimu ambao wamekuwa wakitumika kuwasaidia leo anawafananisha na shetani!? Kaazi kweli kweli! Naona wokovu umeingia sasa mapepo yanapagawa!
 
Hata JK aliwahi kutamka kauli kama hiyo kuwa haitaji kura za wafanyakazi wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi Mkuu 2010. Baada ya siku kadhaa akaja kuwaangukia wafanyakazi kuwa hawakumuelewa....really? Haya this time napo watakuja na press release kuwa Mchemba hakueleweka....NAPE kazi unayo mdogo wangu.
 
Yale yaleee ya mbayuwayu. Nchemba anajua madhara ya hayo matamshi?
 
Si amesema CCM wana hela nyingi, mwashangaa nini. Wanakwiba hazina wanahamishia CCM.
 
Nchemba amepotoka. Anatafuta suluhisho la sasa kwa kutumia njia yoyote bila kufikiria madhara yake baadae. Hawa watu wanatakiwa kufukuzwa CCM bila notice. Sijui kurugenzi ya Uenezi ya chama iko wapi.
 
hivi lini haya matusi yataisha aki ya mama wananchi itafika mahala tutawapiga mawe kama huko viongozi wa hii nchi,we umefundishwa na nani!mi nauliza wanajf hv hizi dharau na matusi hadi lini?
 
Ndio waalimu wajifunze sasa! Kumbe wanaonekanaga hawana maana baada ya kutumiwa! Kazi kwao!
 
Halafu bado walimu hao hao wanadanganywa wakati wa uchaguzi wanaisaidia ccm
 
Eee Mungu muumba wa mbingu na nchi, umewaumba watu kwa vipaji tofauti, miongoni mwetu umeweka waalimu, wahandisi, makasisi, wanasheria madaktari n.k. Sote nia yetu ni moja tu ya kupafanya duniani kuwa mahali pazuri kama mji uliotuandalia, kwa ajili ya utukufu wako.

Tunakushukuru sana sisi waalim ambao, uliona umuhimu wetu ukatupa kazi aliyoifanya bwana wetu Yesu kristo na baadae akamwachia Roho mtakatifu. Tunakuomba utupe moyo wa kusamehe pia na wewe uwasanehe hawa wanao tutukana pasi kujua kuwa sisi tunafanya kazi uliyotuitia. Tupe moyo wa kuipenda kazi yetu, na wala hawa wanasiasa ambao sisi tumewafundisha na bado tunaendelea kuwafundisha lakin bado wanatutukana tusiwajali na tuwadharau ili tuweze kuifanya kazi hii kwa bidii na kwa uaminifu ili tukuzalie matunda ema si tu kwa ajili ya watu binafsi bali kwajili ya taifa hili na dunia hii kwa ujumla. Tupe moyo wa ustahimilivu kama Kristo alivyokuwa nao. Tunaomba hayo kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

AMEN...
 
Nchi hii walimu wanadharauliwa sana lakini wao ndio walio tufikisha hapa tulipo .mchemba umechemsha
 
Bahati yenu, siku ningeingia hapo kutoa ushahidi huyu Jaji angenitambua kuwa mimi ndio BAJAJI, kudadadeki.
Ni kweli bahati yetu mana ungemwaga mitusi ukachafua hali ya hewa hapo mahakamani.
 
tatizo la dying party aka CCM, kila mmoja ni msemaji.
 
walimu poleni zenu! Endeleeni tu kujipendekeza magambani wenzenu wanawaona nyie mashetani. Khaaa hivi hii ndo ile ccm ya jembe na nyundo? Hapana hii itakuwa ccm ya uma na kijiko wanakula tuu
 
Wakipewa fulana na kofia Bila viatu! aaaaa wanasahau shida.

Acha kuwadhalilisha walimu bila walimu usingeweza hata kuposti mawazo yako.Walimu hawana mpango na CCM tofauti na dhana potofu za watu. Walimu wametoa elimu wanashangaa hata wanaojua kusoma kupigia CCM. Walimu hufanya kazi ya kusimamia uchaguzi na si kupiga kula. Endelea kuwaelimisha wazazi wako vjijini siyo kuelekeza shutuma kwa walimu. Kumbuka nchi hii ilikombolewa na mwalimu.Tuungane pamoja kuitokomeza CCM
 
Hivi Nchemba amefikiria madhala ya kauli aliyoitoa? Yaani leo anawaita walimu SHETANI wakati hawa ndio wasimamizi wa chaguzi zote?

Leo anaserma kwamba CCM haitegemei walimu kushinda wakati tunafahamu ndiyo huwa wanaisadia CCM (halali na isivyo halali) kushinda.

Nitashangaa sana kama CWT haitatoa tamko KALI kulaani udhalilishaji wa huyu Mh. Nchemba.

Kweli fedha fedheha yaani leo Nchemba kuwa mweka hazina wa CCM tayari amewaona walimu waliomfikisha hapo alipo kuwa ni MASHETANI?! Baba wa Taifa JK wa ukweli alipendelea kuitwa kwa jina la MWALIMU. Sasa sijui kwa Nchemba Nyerere ni SHETANI WA TAIFA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom