NCCR na MASLAHI YA TAIFA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR na MASLAHI YA TAIFA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by George Kahangwa, Oct 27, 2008.

 1. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #1
  Oct 27, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  NATIONAL CONVENTION FOR CONSTRUCTION AND REFORM –MAGEUZI
  (NCCR-MAGEUZI)

  TAMKO LA CHAMA KUHUSU MASLAHI YA TAIFA LETU LA TANZANIA

  Ndugu wananchi,

  Baada ya kutafakari kwa kina mambo kadhaa yaliyojiri katika taifa letu hivi karibuni na yanayoendelea kutokea hapa nchini na kwingineko tumeona ipo haja ya watanzania kuwa makini sana ili taifa letu lisije likakosa mwelekeo kabisa, tusije kufika mahali tukapoteza yale yaliyo ya thamani kwetu tukaingia katika mvurugano, machafuko na hatimaye kuangamiza taifa letu sisi wenyewe. Hivi sasa kwa mfano kuna ongezeko wa utoaji wa kauli zenye shari katika majukwaa ya kisiasa, ongezeko la migogoro/migomo ya wafanayakazi, kadhalika mzozo unaoibuka kuhusu mpango wa serikali kuitafutia nchi yetu uanachama wa jumuiya ya Organization of Islamic Conference (OIC)

  Ni kutokana na tafakuri yetu juu ya yote hayo, tumeonelea ni vyema tukatoa wito kwa kila mwananchi wa Tanzania kuitambua hatari hii na kuchukua hatua za maksudi la kulinusuru taifa. Hatua za kuchukuliwa na kila mmoja wetu ni pamoja na kuhakikisha kwamba kwa mawazo yetu, matendo yetu, kauli zetu zote tangia sasa zizingatie kwa dhati kabisa MASLAHI YA TAIFA.

  Ndugu wananchi, kinachoendelea katika taifa letu kisiasa, kiuchumi na kijamii kinaashiria ongezeko la watu kutojali maslahi ya taifa badala yake kuzidisha umimi na uendekezaji wa maslahi binafsi na au maslahi ya wachache.

  Uendekezaji huu wa maslahi binafsi una na utaendelea kutengeneza nyufa zitakazolibomoa na kulisambaratisha taifa letu. Hatuna budi basi kujisahihisha na kuamua kurejea sote kwa pamoja katika uzingativu wa MASLAHI YA TAIFA.

  Ndugu wananchi, ili tuweze kuyazingatia vema maslahi hayo ya taifa hatuna budi kwanza kuyatambua ni yapi. Yamkini orodha yaweza kuwa ndefu, lakini sisi katika chama chetu cha NCCR-Mageuzi tunayatambua maslahi ya taifa kuwa ni pamoja na yafuatayo.

  • Amani
  • Umoja wa kitaifa
  • Haki za kisheria, kijamii na uchumi
  • Ustawi wa jamii
  • Ulinzi na uvunaji wa rasilmali za nchi kwa manufaa ya wananchi wote
  • Maendeleo ya kijamii na kiuchumi
  • Usalama wa nchi

  Ndugu wananchi, suala la uwepo wa amani na utunzaji wake ni la maslahi ya taifa yaliyo bayana. Hivyo mtu yeyote anayewaza na kutoa kauli zozote zinozoashiria uvunjifu wa amani, yatupasa tumtambue kuwa kwanza ni mbinafsi na tena ni mtu hatari asiyelitakia taifa letu mema. Mtu au kundi la watu wa namna hii tusiwaache wakaendelea kulihatarisha taifa letu. Hatuna budi kuwakemea watu wa namna hii na kujiepusha kuwaunga mkono kwa namna yoyote ile. Hatutakiwi tena kuendelea kuwapa fursa baadhi ya watu wanaoufanya vitendo ambavyo vina mwelekeo wa kutuondolea amani yetu.

  Katika hili tunatoa wito kwa kila mtanzania kuitetea na kuilinda amani ya nchi yetu. Tunawaomba sana walioko katika vyama vya siasa na vikundi vingine vyenye fursa za kuielimisha jamii hususan katika mikusanyiko ya hadhara, wajiepushe (kwa asilimia 100) kujihusisha na jambo lolote lililo kinyume na utunzaji wa amani.

  Tunatoa pia wito kwa vyombo vya habari vyote nchini, vinapoendelea kufanya kazi yenye heshima ya kuihabarisha jamii vizingatie kujiepusha na utoaji, utangazaji au uandishi wa habari zozote zinazochochea uvunjifu wa amani. Kwa mantiki hiyo habari zote wanazopatiwa watanzania hazina budi kuzingatia MASLAHI YA TAIFA.

  Umoja wa kitaifa ni jambo ambalo taifa letu linauhitaji sana husuan katika kipindi hiki tulichonacho kilichogubikwa na mabadiliko mengi sana yanayoikumba dunia. Tunapaswa kwa maslahi ya taifa kudumisha umoja wa Taifa , bila kujali tofauti zozote zile tulizo nazo. MASLAHI YA TAIFA yako juu ya tofauti zetu za kiitikadi, uanachama wa vyama, imani zetu za kidini, makabila na koo zetu, madaraja ya kipato, rangi , jinsia na au umri. Tunapaswa kudumisha mifumo na taratibu zitakazohakikisha kwamba, kwa MASLAHI YA TAIFA tunajitambua kwamba sisi ni watanzania wamoja na kamwe tofauti zetu hazitugawi kwa namna yoyote ile. Kwa kuheshimu umoja wetu, ndio maana sisi katika NCCR-Mageuzi tungependa kuona kwamba hakuna masuala ya kitaifa yanayoonekena kuwa na mwelekeo wa kuvinufaisha au kuvishirikisha vikundi fulani tu katika jamii na vingine vinabaguliwa.

  Mfano dhahiri ni jinsi chama cha CCM kilivyobinafsicha Mwenge wa Taifa. Ndugu wananchi, ,kadri mwenge utakavyoendelea kuonekana au kutumika kwa maslahi ya CCM, tutakuwa tumehalalisha hata upotoshaji wa lengo la msingi la kuanzishwa kwa mbio zenyewe. Tunaitaka serikali katika hili itangaze wazi kuwa mbio za mwenge zitashirikisha vijana wote wa taifa hili bila ubaguzi wowote wa kisiasa tangu sasa na siku zote.

  Haki, kama inavyotajwa hata katika misahafu, inaposhamiri katika taifa lolote hakika italiinua taifa hilo. Nchi yetu inazo sheria kadhaa ambazo ndio chanzo cha ukiukwaji wa haki za wananchi. Tukichukulia mfano wa matatizo yanayowakumba walimu hivi sasa na jinsi walivyozuiliwa na mahakama kugoma. Kama tunashuhudia waalimu wa watoto wetu wakizibwa midomo kwa nguvu za dola, je tunatazamia walee vijana wetu kuwa binadamu huru au makondoo tu.

  Kila mtanzania ana haki sawa na anastahili kulindwa maslahi yake na vyombo vya dola. Mbona tunashuhudia haki za raia binafsi na makundi zikivunjwa kila siku na vyombo vya dola? Mbona wastaafu wa Jumuia ya Afrika Mashariki hawalipwi malipo halali wanayodai? Mbona wafanyakazi katika sekta mbalimbali wanagoma kutokana na mishahara kiduchu na mazingira duni ya kazi na serikali haichukui hatua muafaka kuwaondolea kero zao? Mbona wanafunzi wanagoma kila kukicha, wakilalamikia mfumo mbaya wa mikopo, na serikali haiwajali?

  Katika hili tunawaomba tena watanzania wote popote walipo,watu wote ambao wana mamlaka ya aina yoyote juu ya watu, watende haki yote. Hatuna budi kuondokana na ukiukaji wa haki za binadamu. Tuondokane na vitendo vya kunyanyasa watu na kuwanyima mafao yao.Amani ni tunda la haki. Hivyo tunatoa wito kwa serikali yetu, kwamba wakati umefika ichukue hatua za dhati za kuliondolea taifa sheria zote zisizotenda haki hapa nchini.

  Ndugu wananchi, sote tunafahamu jinsi Mungu alivyolijalia taifa letu utajiri wa rasilimali. Wajibu wetu sote ulio MASLAHI KWA TAIFA, ni kuzitunza rasilimali hizi na kuzitumia kwa busara kubwa. Tusimame kwa pamoja sasa na kuamua kuwa kwa maslahi ya taifa tutatunza kwa uangalifu sana rasilmali na mazingira yetu. Aidha tudhamirie kuvuna na kutumia raslimali zetu kwa namna ambayo ni endelevu na inaliletea taifa letu faida. Ili zitunufaishe sisi na vizazi vyetu vijavyo.

  Ustawi wa jamii, ni miongoni mwa mambo yenye maslahi makubwa kwa taifa katika mantiki ya kwamba kusitawi kwa jamii ndiko kustawi kwa kwa taifa lenyewe na watu wake. Hatuna budi sote kwa pamoja kuhakikisha kwamba tunajiepusha na mambo yote yanayodumaza jamii yetu. Sote kwa pamoja tunalo jukumu kubwa la kufanya katika hili, lakini serikali yetu inao wajibu ambao imekabidhiwa rasmi na wananchi iufanye.

  Tunapenda kuikumbusha serikali kwamba izingatie maslahi haya ya taifa kwa kuhakikisha inaondoa na kudhibiti vikwazo vyote vinavyozuia ustawi wa mtanzania mmoja mmoja na jamii kwa ujumla. Tunaitaka serikali iondokane na matumizi ya sera au programu zinazonyima watu fursa ya kupata elimu bora hadi upeo wao. Serikali inatakiwa kuhakikisha kwamba jamii nzima inapata huduma za afya na maji bila ubabaishaji wowote na visingizio visivyoisha.

  Kwa bahati mbaya baadhi ya watumishi wa umma na viongozi wetu wamekengeuka kimaadili katika nafasi zao za kazi na wametindikiwa uaminifu. Ndugu wananchi, katika baadhi ya nchi hapa ulimwenguni ambako watu wake wanajali maslahi ya taifa lao, wanajivunia uwepo wa ‘zero corruption' tuamue sasa kwa maslahi ya taifa kuchapa kazi na kurejesha kiwango cha juu cha uaminifu katika nafasi zetu za utumishi.Tupige vita ufisadi Kwani huyu ni adui wa kwanza wa taifa.

  Sisi katika NCCR-Mageuzi kuanzia sasa program zetu za elimu ya uraia na ziara tutakazozifanya katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu zitatanguliwa na dhima hii ya MASLAHI YA TAIFA.

  Mungu ibariki Afrika,

  Mungu ibariki Tanzania, utuwezeshe tuyalinde maslahi ya taifa letu.

  Ahsanteni kwa kutusililiza,

  Imetolewa na Secretariat ya Halmashauri kuu ya Taifa,

  NCCR-Mageuzi
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Oct 27, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Asante Kahangwa,

  Walau siasa za CHADEMA vs CCM zinaweza kupungua JF :)
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mkuu kweli ni nani atapoteza muda kuzungumzia NCCR mageuzi a dead thing?
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mchukia Fisadi,
  Chukua tano ndugu yangu. Kule Tarime NCCR walionyesha rangi zao halisi.
   
 5. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  haya mambo angalau wangeyasema mengine kule tarime nadhani ningewaona wako serious. lakini kwa sasa mi naona ni politics tu na kama alivyosema mdau mwengine "ndo mambo ya ntoke vipi".
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Oct 28, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280
  NCCR:

  Kabla ya kuongea hayo mnayoongea kwanza

  1. Waelezeni watanzania role yenu hapa nchini nyie ni wanamageuzi au CCM-B?

  2. Waelezeni watanzania kuwa mmefanya nini mpaka leo kuimarisha vyama vingine vya upinzani au, mmehusika vipi kuua upinzani Tanzania?

  3. Hayo mliyoeleza mmepoteza muda, kwani CCM-wenyewe hawasikii, hawaambiliki, hawaelewi, wala hakuna mtu yeyote atakayesoma na kutekeleza maoni yenu, nadhani kazi kubwa iwe kubadilisha katiba na kuingia madarakani kidemokrasia huku mkiungana na kuwa kitu kimoja.

  4. Kitu gani kimewafanya mshindwe TARIME? mnaweza mkasoma picha ya watanzania wanawasomaje?

  waberoya
   
 7. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hawa ni maarufu sana kwa kudandia hoja.It's as if wanasubiri jambo flani litokee then nao wajifanye kushikia bango.NCCR imebaki kuwa jina tu,na kama kuna kama kuna mahesabu ya hivi karibuni waliyokosea zaidi basi ni katika ishu ya kifo cha Wangwe na uchaguzi mdogo huko Tarime.Totally discredited!!!
   
 8. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #8
  Oct 28, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF,
  Nashukuru sana kwa mchango wenu unaodokezea picha potofu inayojengwa kuhusu chama cha NCCR-Mageuzi.Awali ya yote naomba niweke wazi kwamba mimi ni George Kahangwa, mwanachama wa NCCR-mageuzi, sioni sababu ya kuficha ukweli huo, maana ni vizuri niseme sasa ili hata mnapoendelea kututumia makombora mjue yanafika na tunaendelea kuyatafakari na kuyaona kama changamoto kwetu maana tunaamini ninyi ni watanzania na myasemayo ni sehemu ya ujumbe mlionao kwetu, japo yameghubikwa na hoja zilizojengwa juu ya uongo.

  Napenda kutofautiana nanyi katika mambo kadhaa:
  Mosi, si kweli kwamba NCCR ni a dead thing, we are alive and well. Kufa kwa chama huthibitishwa na msajiri wa vyama vya siasa kwa kufuata vigezo rasmi. vipo vyama vilivyokwisha kufa na kufutwa, nanyi mnalijua hilo.Aidha kumbukeni nchi yetu kwa sasa ina vyama vya siasa 18, vipo vinavyosikika vikifanya kazi na vipo vilivyosinzia, fanyeni tathmini ya kina ili madai yenu ya ufu wa chama yawe na msingi. chama gani mnathubutu kusema kimekufa wakati mnajua vizuri kinaongoza serikali za vijiji na kina madiwani kadhaa hapa nchini, nk.

  Tunajua chanzo cha propaganda hii, tunamjua kiongozi mwandamizi wa chama fulani anayezunguka nchini akiwaaambia watanzania kwamba NCCR imekufa, tulipombaini na kumwuliza kulikoni akatuma ujumbe wa kutuomba radhi, au mwataka nimtaje jamani...

  Pili,kumbukeni ujumbe tuliouandika unahusu maslahi ya taifa, someni vizuri ili mtambue kwamba hatudandii hoja bali tunatekeleza wajibu wetu kama chama cha siasa wa kutoa rai kwa jamii nzima ya kitanzania, hatukuiandika serikali tu na hata hivyo serikali isiposikiliza sisi tumetimiza wajibu wetu.

  Tatu, suala la Tarime, niwambie wazi kwamba sababu kubwa ya NCCR kutofanya vizuri Tarime ni propaganda ya adui yetu tunayemjua aliyeamua kueneza uongo kwamba sisi tumetumwa na CCM na kwamba ana ushahidi.Mtakeni basi atoe ushahidi, vinginevyo itakuwa ni jambo la kusikitisha kama watanzania mtaendelea kuushabikia uongo ushinde na kutamalaki juu ya ukweli, wanatarime walituhukumu kwa kudhani ni kweli tumetumwa na CCM.

  Wakati huo huo mtakumbuka kulikuwa na uchaguzi mwingine mdogo kule Nguruka, NCCR tukaishinda CCM, lakini vyombo vya habari vilivyolishwa sumu ya uongo vikaandika kuwa ni CHADEMA imeshinda Nguruka, tafuteni basi ukweli nani alishinda kule Nguruka.

  Vile vile mtakumbuka kuwa chama chetu pamoja na vyama vingine vitatu tuko katika ushirikiano, katika suala la Tarime vyama hivi tulikaa kukubaliana kumsimamisha mgombea mmoja, katika kikao kilichofanyika huko huko Tarime tarehe 11 September, vyama hivi vilimpitisha mgombea wa NCCR, lakini CHADEMA hakikukubaliana na hayo,kikasimamisha nacho mgombea.Huu ukweli msiukimbie, pendeni kujua hasa ni nini kilitokea Tarime.Mkitaka niulizeni ikawaje CHADEMA kikashinda.

  Nne, kuhusu mchango wa NCCR katika mageuzi nchini, uko wazi labda kwa wasiojua historia ya mageuzi nchini.Kwa ufupi tu kumbukeni NCCR ilianza kama vuguvugu la wanamageuzi nchini hata kabla ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini. Kutoka NCCR vilizaliwa vyama vingi sana kikiwemo hicho ambacho baadhi ya wanajf hapa mnaonekena kukishabikia sana.Someni historia hiyo, mtagundua pia kuwa kumbe hata jina la chama kipenzi chenu limetokana na maneno ambayo hadi leo yako katika nembo ya NCCR.

  Binafsi mimi ni shuhuda wa jinsi ushirikiano wa vyama ulivyoanzishwa, na nilikuwepo siku tamko la ushirikiano linaandaliwa pale makao makuu ya NCCR, siku chache kabla ya tamko kutangazwa tr.10 May 2007.Ndugu zangu niwashirikishe siri ninayoijua,kabla tamko halijatoka neno ushirikiano lilisomeka muungano, aliyelibadili tunamjua na huyo ndiye mnapaswa kumtupia madongo ya kutokuwa na mchango wa kuviimarisha vyama vya upinzani.

  Suala la muungano, NCCR tulilipendekeza kwa wenzetu mara kadhaa (na ushahidi upo) tulilipendekeza baada ya kulifanyia utafiti wa kina nchini (research report ipo), Hamtutendei haki kusema hatuna mchango wowote katika mageuzi ya nchi hii, kusema hivyo ni kupotosha ukweli.

  Wana JF, yafaa basi tusimamie ukweli kuliko ushabiki.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Oct 28, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kahangwa,
  Mkuu unazungumza na watu ambao walikuwa NCCR mageuzi na wameondoka humo baada ya kuona mnababaisha!...Binafsi nimeongea na watu ambao walikuwa chama hicho na wengi wametoka baada ya kutambua kwamba mnasimamia maslahi yenu watu binafsi zaidi ya Taifa..
  Mnachokitazama ni hizo ruzuku za bungeni kuendesha maisha yenu hamna agenda za kitaifa zaidi ya kufunga kamba mashua yenu ndogo nyuma ya Melikebu CCM, bila kujali wala kujua mnapelekwa wapi.. Umediriki hata kuita chama kingine kuwa ni maadui wenu wakubwa!.
  Huo Uadui wenu umeanza lini na imekuwaje muite chama kingine kuwa ni MAADUI zenu ikiwa kweli mnajali demokrasia na unayoyatangaza hapo juu yanatoka rohoni mwako!...
  Mnatisha mkuu..
   
 10. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #10
  Oct 28, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Adui yetu (sijasema mkubwa kama unavyotaka kunilazimisha wewe) ni mtu binafsi. Jujali kwetu demokrasia hakumaanishi hata mtu akisema uongo tuiite hiyo nayo ni demokrasia
  Naomba nawe usijiunge na wanaoshabikia uongo, nitajie kiongozi wa chama cha NCCR anayeishi kwa pesa ya ruzuku. Labda ungeuliza NCCR inapata ruzuku kiasi gani na inazitumia kufanya nini, na auditors wanakuta nini katika mahesabu ya mapato na matumizi ya chama hiki.
   
 11. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Kahangwa mdogo wangu

  bado umri wako unakuruhusu kuwa kwenye siasa muda mrefu, angalia usijipake uchafu wa kina Mbatia.

  Nitakutafuta hapo UDSM tutaongea zaidi.

  Unaweza kuniambia NCCR ilifanya mara ya mwisho uchaguzi wa chama lini na katiba iliwataka kukaa madarakani mpaka lini? Katika ofisi ya msajili inaonyesha uongozi wa Mbatia ulisha-expire toka Agosti, 2008.

  Kama unataka NCCR iinuke itisheni uchaguzi muwaondoe wote wenye kutumika

  Kuhusu Tarime, ni Lipumba, Mrema na Mbatia walikaa DSM na kukubaliana kumuunga mkono mtu wa NCCR kwa shinikizo la Mbatia na hamkutaka kabisa kuihusisha CHADEMA.

  Na unajua ni nani alitoa zile fedha za kampeni kule? Kwa sisi tulio karibu na vigogo wa New Habari Corporation tunapata fursa ya kupata habari za ndani zaidi

  Lakini nikurekebishe, kule Tarime uamuzi ulikuwa ni kuunga mkono CHADEMA ndio maana CUF Tarime wameunga mkono CHADEMA na hivyo kufanya CUF taifa kuwa neutral.

  Kule Nguruka CHADEMA haikusimamisha mgombea iliunga mkono NCCR, kwa nini na nyinyi hamkuiunga mkono Tarime?

  Hilo la ushirikiano wa vyama wakati wa majadiliano ya ushirikiano, wenzenu CHADEMA na CUF waligundua mtego wenu wa kutaka kuunganisha vyama wakati sheria hairuhusu hali ambayo ingepelekea vyama hivyo kupoteza wabunge.

  Nayajua haya vizuri kwa kuwa ni sisi Habari Corporation ndio tuliovujisha kwamba vyama kuungana, na tuliletewa habari yote na Polisya Mwaiseje na Dr Mvungi. Na unajua nani alifadhili ule mchakato?

  Sasa mmewekwa katika wakati mgumu, CUF na CHADEMA wameanza kuwasusa nyinyi na TLP baada ya kutumika. Na mkiendelea na staili hii, wananchi nao watasusa.

  Niseseme mengi, ila nitakueleza kwa kirefu tukionana. Najua unapenda mageuzi, ila NCCR ni MASIHARA. Labda uifanyie mageuzi kwanza.

  PM
   
 12. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  NCCR ilikufa siku ilipoanza kuokoteza mizoga kutoka CCM - mojawapo Augustine Lyatonga Mrema - na kuipa uongozi wa chama. Wakati wa vuguvugu la vyama vingi NCCR iliwapa matumaini makubwa watanzanaia makini na kuashiria mageuzi ya kweli mpaka pale ilipoanza kulamba matapishi ya CCM. NCCR iliyozaliwa na kuanza kutambaa ikaingizwa kwenye mbio za masafa marefu kabla ya kutembea na ikajikuta inalamba dume. Pamoja na kuwa NCCR ilizoa makapi mengi toka CCM yaliyosindikiza mpiga zumari Mrema, lakini ilikuwa wazi kuwa yalikuwa ni kama mapanya yaliyoitikia zumari ya "Peter Piper" na yakaongozwa mapaka mtoni yalipotumbukia na kufa kama mende.

  Wengine tuliokuwa na tumaini na chama kipya chenye mawazo mapya tulijikuta tukirudi kwenye maganda yetu kama kobe aliyenusa moshi wa pili pili. Huo ndio ulikuwa mwisho wa NCCR na hivi sasa tunalolishuhudia si chama makini bali kijiwe cha machinga wa siasa. Hakina tofauti na TADEA, DP, NLD na utitiri wa vyama visivyo na dira. Ungeni mkono wanademokrasia wa kweli kwa kujiunga na vyama serious na acheni kudandia migongoni mwa MAFISADI. Huo unaitwa ULAFI.
   
 13. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #13
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mimi nachoka kabisa, sielewielewi eti
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Oct 28, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kahangwa,

  Mku tuache uswahili ktk ukweli. Mtu yeyote atayekae soma maelezo yako hapo juu inaonyesha wazi kuwa umekitaja chama Chadema mara nyingi katika mabaya na ya Uadui..

  Wewe hapa umeandika kama Kahangwa ni mtu mmoja lakini maelezo yako yanabeba uzito wa chama cha NCCR, hatuwezi kusema kuwa maneno haya ni ya Kahangwa mtu mmoja ikiwa upo hapa kwa niaba ya chama.

  Huyo mtu mmoja hakusema aliyoyasema kwa maslahi yake ila ya chama na kam imefikia wewe kumuita kiongozi wa Chadema kuwa aduii YENU bila shaka una maana Chadema ni adui...

  Hata Marekani wanapotangaza maadui wao haina maana wanazungumzia rais ama kiongozi mmoja ni utawala mzima kutokana na itikadi ama matendo ya Utawala huo..

  Jambo jingine, nimesoma Tamko lenu NNCR kuhusiana na Maslahi ya Taifa ni upotoshaji kama unavyoonyesha ktk kutaka undugu wakati huo huo unajenga Uadui na vyama vingine...

  Mkuu katika maelezo yangu mengi sana nimekuwa nikitumia vitu hivi viwili WATU na MAZINGIRA kuwa chanzo cha mabadiliko yoyote ya Kijamii..Huwezi kutaka kuboresha maslahi ya Taifa kwa kuzuia culture ama asili ya kundi moja linalotengeneza jamii kufanya mambo ya kikabila, kijinsia, rangi ama kidini kwa sababu nchi yetu haina ubaguzi.. Ni kinyume.

  Kuboresha jamii ni pale sisi tutakapo kubali tofauti hizo, kukubali identity ya makundi hayo na kupokea culture zao maadam zitaboresha maslahi ya Taifa kama ulivyoorodhesha hapo juu. Kukataza matumizi ya culture hizo ni mwanzo wa kutenganisha jamii hizo.

  Tatizo kubwa la nchi yetu ni KUIGA, leo hii tunatunga na kusimamisha sheria kwa kutazama nchi kama Uingereza ambazo kwa miaka mingi wamekataa hata kukubali haki za Ireland, Scotland na kadhalika kiasi kwamb wamekuwa na matatizo ya ndani kwa karne. Tunakubali mifumo ya nchi kama Ujerumani, Holland na kadhalika ambazo zimeundwa na kudumisha culture ya kabila moja, dini moja na kadhalika kuzipandikiza Tanzania mahala ambapo tuna makabila zaidi ya 120 dini zisizopungua kumi na zote zimeshiriki ktk kuunda taifa letu..

  Tazama nchi kama Marekani ambayo imeundwa na culture tofauti inakubali na kuenzi hata Culture za Wachina pamoja na kwamba hakuna uhusiano mzuri na nchi yao China. Wanatukuza culture za Wa Ireland pamoja na kwamba walikuwa hawana uhusiano mzuri na ERA kwa sababu kinachounda Taifa ni WATU..Na hakuna mtu wala kabila jingine wanaofikira mbona sisi Wataliani hatuna siku maalum kama Ireland..

  sababu ni ndogo sana kuwa Wataliani hawana culture hiyo na sio lazima kinachofanywa na Wairish ni culture ya Wataliani pia..

  Lakini wakati huo huo utakuta kwamba Marekani ni nchi ilijengwa na values za Kikristu, hivyo wana kila haki ya ku protect values hizo kwa kupinga culture za Kiislaam ama dini nyingineyo kujenga sheria ambazo zinapingana na value za Kikristu..

  Sisi Tanzania nchi yenye mseto kama nchi za Marekani, Canada, Australia, au South Afrika ni nchi ambazo tunatakiwa kukubali na kupokea zaidi culture za wahusika kulingana na historia ya nchi yetu ambayo imejengwa na WATU wa makabila tofauti, dini tofauti, rangi tofauti na kadhalika kuliko kupinga na kuwatenga baadhi ya watu tukifikiria kwamba tunajenga maslahi ya Taifa.

  Ni katika mazingira tunayoishi mkuu tunakaribisha zaidi utengano na haswa katika maswala ya VYAMA na DINI kwa kufikiria kwamba tukikataa na kujenga Uadui tutakuwa tunaboresha Haki na Ustawi wa jamii zetu..Mkuu ukweli ni kwamba tutakuwa tunabomoa na kuhatarisha zaidi vifungu vyote vya maslahi ya Taifa..

  Nitakupa mfano mmoja mdogo sana ambao hauna maana kama ndivyo inavyotakiwa. Leo hii sidhani kama tunaweza kukubaliana Ijumaa iwe siku maalum ya ibada kwa Waislaam kisheria na mjadala kama huu hauwezi kuwa na suluhu hata kidogo lakini ukibadilisha kidogo tu.. iwe kwamba Tanzania ilikuwa ikichukua Ijumaa kama siku ya Mapumziko, then Wakristu wakaomba Jumapili iwe pia siku ya Mapumziko... ungeona malumbano na hukumu tofauti kabisa..Yote haya yanatokana na kwamba hatukubali wala kutambua culture ya mtu mwingine..

  Ni katika mtazamo kama huu ndio maana tunashindwa kuliweka swala la OIC kando, kulitazama, kupima kama linaweza kuathiri hata sehemu moja ya hizo orodha ulizoziweka hapo juu bali tunatumia hisia zetu zaidi kama ulivyotumia wewe katika kutoa maelezo yako kuhusiana na Chadema...
   
 15. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2008
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kahangwa...kahangwa...kahangwa...

  Huu uwanja ni mkubwa kwako kaka. Unaweza kuwa mkali sana darasani lakini sio katika siasa kaka. Haswa siasa za kiasasa. Angalia usije ukajikuta hapo baadae watu wanashindwa kutofautisha ukilaza wa MBATIA na wewe....

  Huyo mtu unayemsema kuwa ni adui yenu unadhani unaweza kupambana naye kaka. Kama unataka mwisho wako kisiasa basi simama hadharani na kumnyoshea kidole. Wengi walijaribu lakini angalia wako wapi. Wameshindwa CCM mtakuwa ninyi na siasa zenu zilipendwa. Soma alama za nyakati kaka. Watanzania hawawezi kukuelewa ukianza kumtusi huyo unayedhani kuwa ni adui yenu.

  Adui yenu ni kuendesha chama kizamani, kichuki na siasa za wivu ambazo viongozi wako wamekua wakiziendesha tangia uchaguzi wa 2005. Kukubali kupokea msaada wa CCM "kuwamaliza" wapinzani wenzenu na wivu wa kijinga ambao mweneyekiti wenu alionyesha wakati wa msiba wa CHACHA na baadae uchaguzi wa TARIME 2008 ni makosa makubwa mmeyafanya. Tatizo la NCCR badala ya kujipanda kama asasi na kujionyesha kuwa ninyi ni wabora kuliko wapinzani wenzenu na hata CCM mnabakia kuendeleza libeneke na wapinzani wenzenu. kabla ilikuwa CUF na sasa CHADEMA.

  Hivi ninyi na akili zenu mlitegemea mnaweza kushirikiana zaidi na CUF kuliko CHADEMA ukizingatia historia mliyonayo na CUF haswa wakati ule wa kura za maruhani PEMBA? Na hapa sijasema prejudices za kitaifa na kijamii zilizojaa miongoni mwa makundi yenu ya kisiasa...Waanglikana Vs Waislamu Siasa kali..siamini hivyo lakini ndio existing perceptions kaka..


  Na kuhusu hii ajenda ya MASLAHI YA TAIFA acheni hii copy and pest strategy. Wenzenu CHADEMA wameshaweza kujijenga kama chama kinachosimamia MASLAHI YA TAIFA na hata kuizidi CCM ilikuwa na uhodhi wa ajenda hiyo. Watanzania walio wengi wanaamini kuwa CHADEMA wameweza kusema na kutenda kiasi kikubwa kuonyesha kuwa wanajali maslahi ya Taifa. Sasa ninyi kutaka kunyang'anyana ajenda hiyo kama ilivyo kwa CUF Vs CHADEMA on ufisadi ni ushuhuda wa kushindwa kufikiri tu na sio zaidi. Umizeni vichwa kufikiri ajenda nyingine ambayo itakuwa ya kwenu kimuono na kuipigania kuipeleka kwa jamii wakaikubali na kujenga imani nanyi na sio hizi za kuiga na kugombania miongoni mwa the so called WAPINZANI....


  Kaka i know u ar damn smart and class A brainer but huko uliko sipo....

  Tanzanianjema
   
 16. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #16
  Oct 28, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mkandara, tatizo hapa (kwenye thread hii) ni hilo la wanaJF kuacha mada wakaanza upenzi wa vyama, nilitarajia tokea mwanzo mjadala ungeelekea zaidi kwenye maslahi ya taifa, ili sisi tulio watanzania tutafakari kwa pamoja na kupeana mawazo kuhusu maslahi ya taifa letu. Ni vema kwamba angalau post yako hii inamwelekeo wa kujadili mada, endeleza basi mwelekeo huo.
   
 17. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  Mimi ninaposikia au soma NCCR - Mageuzi napata kichefuchefu mpaka nakosa akili, chama hiki nilikipigia kura mwaka 1995, sikujua ubaya wake masikini, ingekuwa bora kife kabisa sasa.

  Kimsingi, natamani Tanzania tuwe na Chama kimoja cha upinzani chenye nguvu. Sasa hawa NCCR ni kama DP tu, kuvuruga upinzani. kife, kife kabisa, sitaki kukisikia.
   
 18. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #18
  Oct 28, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mkuu Paparazi,
  yaelekea unanifahamu vizuri. Nipe kabisa appointment tutaonana lini unipe hizo nyeti.Siku zote natamani kujua ukweli wote. Karibu UDSM, pendekeza ni namna gani tuwasiliane ili kufahamishana namna ya kuonana.
   
 19. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #19
  Oct 28, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Tanzanianjema,
  I hope you are not trying to intimidate me and you are not accusing NCCR of plagiarism, ARE YOU?
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Oct 28, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,137
  Trophy Points: 280
  Kahangwa,

  ..usikatishwe tamaa na watu wanaosukumwa na ushabiki na mapenzi kwa vyama vya siasa.

  ..hoja isimame kwa uzito wake. siyo vizuri kuanza kushambulia mtoa hoja, na kumchimba kuwa ni mwanachama wa chama kipi.
   
Loading...