NCCR Mageuzi yaambulia Patupu Babati

Jobo

JF-Expert Member
May 15, 2008
586
43
Habari zilizotufikia sasa hivi ni kwamba Jaji Fatuma Massengi amekataa ombi la NCCR Mageuzi kutengua matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM Virajilal Jitu Son. Hii ndiyo hukumu ya kwanza kutolewa katika kesi za uchaguzi zilizofunguliwa na kusikilizwa hadi mwisho. Habari zaidi zitawajia hivi punde!
 
Business as usual!!
Sikutegemea hukumu nyingine zaidi ya hiyo!
 
Nadhani Malalamikaji alishindwa kuithibitishia Mahakama kuhusu malalamiko yake. Ukweli ni kwamba kwa mahesabu ya kawaida alikuwa amembwaga chini huyo Mhindi lakini kwa kuwa rushwa ndiyo huamua mshindi na hasa kama mwenye pesa mwenyewe anatoka CCM! Ngoja tusubiri tarehe 4 tuone ya Lema!
 
Kesi yapili kunaile ya hiness ilemela mwanza ilipanguliwa na mkali lisu,hongera kwa habari tuliokua tukiisubiria
 
Habari zilizotufikia sasa hivi ni kwamba Jaji Fatuma Massengi amekataa ombi la NCCR Mageuzi kutengua matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM Virajilal Jitu Son. Hii ndiyo hukumu ya kwanza kutolewa katika kesi za uchaguzi zilizofunguliwa na kusikilizwa hadi mwisho. Habari zaidi zitawajia hivi punde!

Mkuu asante kwa kutujuza. isipokuwa hapo kwenye red; nadhani siyo hukumu ya kwanza, kwani hivi karibuni hukumu ilitolewa kwa kesi ya kupinga matokeo ya mbunge wa jimbo la Ilemela, mkoani Mwanza ambapo mlalamikaji bwana DIALLO wa CCM alibwagwa katika hukumu hiyo.
 
Ni kweli, but it is sad kuwa uchaguzi haukutenguliwa. Sijui ni uzembewa Mawakili au ndo basi CCM hawashindwi kesi!
 
Mahakama za ccm unategemea nini?

Napinga dhana hiyo kuwa Mahakama ikikataa kutengua ushindi wa CCM basi directly mnaihusisha mahakama kuwa inawapendelea CCM!

Mbona kesi 2 za uchaguzi hadi sasa hukumu zake UPINZANI ULISHINDA;mahakama hiyo hiyo mnayoilamu nakuiita ya CCM ILITUPITILIA MBALI malalamiko ya wagombea wa CCM ktk majimbo ya ILEMELA NA KILWA;sikumsikia hapa JF tukisema kuwa MAHAKAMA INAPENDELEA UPINZANI!

Chadema-ILEMELA walithibitishiwa ushindi wao na mahakama hivi karibuni na CUF kule Lindi Mbunge wao Bwenge alithibitishwa na mahakama pia mwezi uliopita kwa kukataa hoja za CCM!

Tusiwe biased kiasi hiki jamani!
 
Ni kweli, but it is sad kuwa uchaguzi haukutenguliwa. Sijui ni uzembewa Mawakili au ndo basi CCM hawashindwi kesi!

Mkuu katika kesi ya jimbo la Ilemela mbunge wa CHADEMA Mh. KIWIA alishinda kesi dhidi ya mlalamika Bwana Diallo wa CCM, hivyo CCM hushindwa pia. Kwa kesi ya babati nadhani mawakili wa mlalamikaji hawakujenga hoja vizuri au hapakuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha wanayolalamikia.
 
Mkuu asante kwa kutujuza. isipokuwa hapo kwenye red; nadhani siyo hukumu ya kwanza, kwani hivi karibuni hukumu ilitolewa kwa kesi ya kupinga matokeo ya mbunge wa jimbo la Ilemela, mkoani Mwanza ambapo mlalamikaji bwana DIALLO wa CCM alibwagwa katika hukumu hiyo.

Lindi pia hukumu ilishatolewa tangu mwaka jana kwenye jimbo moja huko.
 
Kesi yapili kunaile ya hiness ilemela mwanza ilipanguliwa na mkali lisu,hongera kwa habari tuliokua tukiisubiria

Ya Babati ni ya 3, kuna ya jimbo la Mwibara ambayo kama kawa, wamekataa kutengua matokeo despite ushahidi lukuki, tumekata rufaa Court of Appeal. Hakuna kulala mpaka kieleweke!!!!

Ilinishangaza Mwibara Jaji anasema, ni kweli uchaguzi ulitawaliwa na Rushwa lakini haikuathiri matokeo!!!! Du!!! Au ndo katika kubana matumizi kuogopa chaguzi ndogo?????
 
Habari zilizotufikia sasa hivi ni kwamba Jaji Fatuma Massengi amekataa ombi la NCCR Mageuzi kutengua matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM Virajilal Jitu Son. Hii ndiyo hukumu ya kwanza kutolewa katika kesi za uchaguzi zilizofunguliwa na kusikilizwa hadi mwisho. Habari zaidi zitawajia hivi punde!

hapo umedanganya mkuu, hapa Mwanza HIGHNESS alishatawazwa rasmi wiki ya kwanza mwisho kabla kampeni hazijazinduliwa za uchaguzi mdogo kata ya kirumba
 
Matokeo watu walio yatarajia yakitoka vile vile huwa watu hawashangai
 
kesi tunayoijua ni moja tu ya mpndazoe na yule mwizi mahanga......hii ndiyo yenye mashiko
 
Jamani hata nccr wanakata rufaa?.....basi hakuna upinzani....mi nilidhani kwa kuwa mbatia anawafagilia ccm basi nccr hawatakuw wakikata rufaa pale ccm au ccm-b wakishina.
 
Napinga dhana hiyo kuwa Mahakama ikikataa kutengua ushindi wa CCM basi directly mnaihusisha mahakama kuwa inawapendelea CCM!

Mbona kesi 2 za uchaguzi hadi sasa hukumu zake UPINZANI ULISHINDA;mahakama hiyo hiyo mnayoilamu nakuiita ya CCM ILITUPITILIA MBALI malalamiko ya wagombea wa CCM ktk majimbo ya ILEMELA NA KILWA;sikumsikia hapa JF tukisema kuwa MAHAKAMA INAPENDELEA UPINZANI!

Chadema-ILEMELA walithibitishiwa ushindi wao na mahakama hivi karibuni na CUF kule Lindi Mbunge wao Bwenge alithibitishwa na mahakama pia mwezi uliopita kwa kukataa hoja za CCM!

Tusiwe biased kiasi hiki jamani!

Nakuunga mkono ndugu;

KWa mtazamo wangu ni kwamba sasa hivi Serikali kutokana na UMKAPA uliopo tusitegemee kama kuna kesi yoyotwe ya kupinga matokeo ya Uchaguzi iwe wa Uraisi, Ubunge au Udiwani itakayopewa hukumu ya Mlalamikaji kuwa ameshinda kesi kiasi ya kwamba italazimu Uchaguzi urudiwe.

Kesi zote iwe zimefunguliwa na CDM, CCM, NCCR, UDP nk. hakuna hukumu itakayotoka tofauti na hii ya BABATI, ILEMELA.

Kwani kurudia uchaguzi ni gharama sana hivyo serikali itabidi itumie pesa nyingi sana. Mfano amgalia sakata la Mbunge Kafulila wa NCCR au Mbunge wa CUF ambao vyama vyao vimewavua Uanachama ambapo kisheria inakuwa wamevuliwa ubunge. Lakini tumeshuhudia hata Bunge lilitoa mpya kwa kumteua Kafulila kuwa mwakilishi wake katika Msiba wa RIP Regia Mtema, hii ni kuonyesha kuwa bado Bunge linawatambua, na hawako tayari kufanyike uchaguzi tena.

Hivyo ni matokeo ambayo tuliyatarajia na pia tunayatarajia kwa kesi zote za kupinga matokeo ya uchaguzi mbalimbali.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom