NCCR Mageuzi wapinga vikali mkataba wa LATAFIMA kuzuia Uvuvi ziwa Tanganyika

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
NCCR - MAGEUZI wapinga vikali mpango wa serikali ya Tanzania ulioridhia kuzuia uvuvi kwa miezi mitatu mitatu katika miaka ya 2023, 2024 na 2025 ambao miezi mitatu ya mwanzo itaanza mwezi Mei 2023 ziwa Tanganyika kupumzisha uvuvi kwa miezi mitatu kisha mpango huo kurudiwa mwaka 2024 na mwaka 2025 ili kusaidia samaki wasiendelee kupungua ziwani.

NCCR-MAGEUZI wanasema mpango huo umekuja ghafla sana bila kuwashirikisha wavuvi na maslahi mapana ya wananchi wanaohusika ktk mnyororo mzima wa uvuvi katika Ziwa Tanganyika na utaenda kuathiri maisha ya maelfu ya wananchi. Hivyo NCCR Mageuzi kuitaka serikali kusitisha mpango huo na serikali iwe imejipanga vizuri zaidi kabla ya kuanza utekelezaji wa kusitisha uvuvi.

Mkataba wa LATAFIMA unaofadhiliwa na FAO, EU pamoja na nchi za Zambia, Tanzania, DR Congo na Burundi kusimamia matumizi mazuri endelevu ya Ziwa Tanganyika. Takwimu za wizara ya mifugo na uvuvi zinasema kuna wavuvi takribani zaidi ya laki moja upande wa Tanzania.

This is official. The Lake Tanganyika Authority has launched the Lake Tanganyika Fisheries Management project, LATAFIMA. It was on this Thursday, December 3, 2020, at the Tanganyika Lake Hotel. The LATAFIMA project is funded by the European Union for the amount of 2 million Euros. The implementation was entrusted to FAO, the United Nations Food and Agriculture Organization, for a project duration of 3 years. With this project, approximately 10,000 direct beneficiaries will be supported from the four countries bordering Lake Tanganyika, namely the Republic of Burundi, the Democratic Republic of Congo, the United Republic of Tanzania, and the Republic of Zambia.

The fight against illegal, unregulated and unreported fishing in Lake Tanganyika, including the capture of immature fish, fishing in regulated areas, and the use of illegal gear will be targeted by the project. The activities of the project were launched by the Permanent Secretary of the Ministry of Environment, Agriculture, and Livestock with the presence of the European Union Ambassador.

“Through this project, the Tanganyika Lake Authority aims to turn fishing into a sector driven by dynamic public and private actors capable of creating jobs, increase production and productivity through sustainable exploitation of Fisheries Resources to reduce poverty, ensure food and nutrition security and access to basic social services», said the Executive Director of the Tanganyika Lake Authority, Mr. TUSANGA MUKANGA Sylvain.

As for the Ambassador of the European Union to Burundi, Mr. Claude BOCHU, the protection of fisheries resources is a priority of the European Union both in Europe and in its external actions in the world. The U.E considers fisheries resources to be common to the humanity,” he mentioned in his speech.

For his part, Mr. Isias ANGWE OBAMA, FAO Resident Representative in Burundi, said that “Open access to the lake, high pressure on the lake due to a very high number of fishermen, the use of prohibited gear and illegal fishing practices are all factors that are responsible for the decline in productivity of Lake Tanganyika. The implementation of this project will contribute to the reduction and mitigation of the many threats to the lake. This project will contribute to ensure the achievement of FAO strategic objective 2, namely to make agriculture, more productive and sustainable forestry and fishing.” The ceremonies ended with the signing of the Memorandum of Understanding between the FAO and the Lake Tanganyika Authority source : Official Launch of the Lake Tanganyika Fisheries Management Project – LTA ALT

Frank Luhasha katibu Uenezi wa NCCR- Mageuzi akiongea na waandishi wa habari kuhusu kadhia inayokuja mwezi Mei 2023

1678179375008.png

Picha maktaba 2022: Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amezindua Kampeni ya Kitaifa ya Uelewa ya Mkataba wa Kikanda wa Usimamizi wa Uvuvi Endelevu wa ziwa Tanganyika LATAFIMA mkataba unaojumuisha nchi zote zinazonufaika na Uvuvi wa Ziwa Tanganyika ambazo ni Tanzania, Burundi, Zambia na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo yenye mikakati mbalimbali ya ulinzi wa rasilimali za uvuvi za ziwa hilo.
 
Wafanyabiashara zaidi ya elfu Kumi wa mazao ya uvuvi ya Ziwa Tanganyika Kigoma wahofia uamuzi wa serikali

 
08 April 2023
Dodoma

Mbunge Aida Khenani azungumzia sekta ya uvuvi hususan mpango wa kufungwa ziwa Tanganyika kwaleta taharuki kwa wananchi wa Rukwa, Katavi na Kigoma



Mbunge Aida Khenani awasilisha kilio cha wadau wa uvuvi kuhusu serikali kufanya maamuzi bila kushirikisha wananchi kama Wavuvi ambao wamesha kata leseni zao za mwaka, wamechukua mikopo n.k huku ni kutowajali wananchi ....
 
02 May 2023

NCCR-MAGEUZI KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA ZOEZI

1683275565381.png

Picha: Frank Luhasha katibu Uenezi wa NCCR- Mageuzi akizungumzia hatua watakazotumia kupinga mkataba wa ziwa Tanganyika


NCCR-MAGEUZI KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA ZOEZI , NAO WAVUVI WAELEZEA WASIWASI KUHUSU UCHUMI WAO ZIWA LIKIFUNGIWA KWA MIEZI MITATU



Katibu huyo Mwenezi wa NCCR – Mageuzi alisema kuwa karibu watu milioni moja wanategemea shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika kama njia kuu ya kujipatia kipato kwa ajili ya maisha yao ya kila siku lakini pamoja na hivyo serikali inafunga shughuli hizo huku kukiwa hakuna njia mbadala ya watu hao kwa ajili ya kujiingizia kipato.


Kwa upande wao wadau wa uvuvi mkoani Kigoma wameitaka serikali kutafakari upya mpango wa kufunga shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika kwani kutekelezwa kwa mpango huo kutaathiri maisha ya wananchi wa mkoa huo ambao wanategemea uvuvi kama shughuli yao kuu ya kuwaingizia kipato.


Picha: makamu mwenyekiti wa chama cha uvuvi Tanzania, Bw. Francis John akizungumza uvuvi ziwa Tanganyika kutoruhusiwa ufugaji samaki wa cage ziwani wakati wavuvi wenzao wa ziwa Victoria wanaruhusiwa kufuga samaki ziwani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau hao walisema kuwa mpango wa kufunga shughuli za uvuvi ambao ulitangazwa kuanza Mei 15, 2023 mwaka huu unapaswa ufanyiwe tathmini ya kina kabla ya kuanza kutekelezwa ili kubaini athari kubwa zitakazojitokeza kwa miezi mitatu ambayo shughuli hizo zitakuwa zimefungwa.


Mwenyekiti wa chama cha wavuvi manispaa ya Kigoma Ujiji, Ally Kibore alisema kuwa moja ya mambo ambayo wanapinga kutekelezwa kwa mpango huo ni Kanuni zilizowekwa na Mamlaka ya usimamizi ya ziwa Tanganyika (LTA) kupitia mradi wa maendeleo ya uvuvi ziwa Tanganyika (LATAFIMA) ambazo zinakwenda tofauti na sheria na kanuni za uvuvi nchini.

Kibore alisema kuwa pamoja na tofauti hiyo ya kanuni ambazo zinapingana na sheria za uvuvi nchini lakini pia changamoto kubwa ni uvuvi haramu ambao ndiyo unaochangia kuua mazalia ya samaki na kuvua samaki wachanga lakini bado changamoto hiyo wasimamizi wa uvuvi wameshindwa kufanyia kazi.

Kwa upande kiongozi wa wavuvi mwalo wa KGODECO, Bi. Ambatanisye Mwakalambile alisema kuwa hawakubaliani na mpango wa serikali wa kufunga shughuli za uvuvi kwa kutumia kanuni za LATAFIMA wakati wizara inayo sheria na kanuni zake ziko vizuri lakini zimekosa usimamizi hivyo wanapingana bna mpango huo badala yake wasimamie sheria na kanuni za uvuvi za nchi.

Mmoja wa wavuvi wa ziwa Tanganyika kutoka Mwalo wa Katonga manispaa ya Kigoma Ujiji,Juma Yahaya alisema kuwa mpango wa serikali kufunga shughuli za uvuvi ziwa Tanganyika ni kilio kikubwa kwao na hasa kutekeleza kwa kutumia kanuni za mradi badala ya kutumia sheria na kanuni za nchi ambazo zinapingana kwenye taratibu mbalimbali.
 
CHADEMA YATOA WITO WA JINSI YA KUBORESHA MAENDELEO YA SEKTA YA UVUVI TANZANIA, NA AJIRA KWA MAMILIONI YA RAIA KUPITIA UVUVI



Makamu Mwenyekiti kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa CHADEMA , kamanda Sijaona James Karoli akizungumza .. kuhusu serikali kushindwa kuona fursa ya uvuvi na nini kifanyike ili taifa linufaike pakubwa kupitia uvuvi ..
 

ULEGA : TUMEJIPANGA KUINUA BIASHARA YA DAGAA WA KIGOMA​

medium-1635496813-WhatsApp%20Image%202021-10-29%20at%2011.08.32%20AM(2).jpeg
Imewekwa: Friday 29, October 2021


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhakikisha Dagaa wa Kigoma wanakuwa ni zao la kimkakati kibiashara litakalokwenda kuvutia uwekezaji na kusisimua uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

Ulega aliyasema hayo wakati akiongea na Wadau wa Uvuvi alipofanya kikao nao katika Mwalo wa Katonga uliopo Mkoani Kigoma Oktoba 17, 2021.

Alisema kuwa serikali imejipanga kufanya zao la dagaa wa Kigoma kuwa la kimkakati kwa sababu biashara ya dagaa inahusisha watu wengi katika jamii, hivyo kuiimarisha biashara hiyo ni kuwaimarisha wananchi kiuchumi.

"Sisi Serikali tunataka kuinua biashara ya dagaa wa Kigoma, tunataka wavuvi wainuke kiuchumi, na tumejipanga kuondoa vikwazo vyote vinavyowasumbua na tutalitangaza vyema zao hili ili kuvutia uwekezaji zaidi hapa Kigoma," alisema Ulega

Pia, Naibu Waziri Ulega aliwataka Viongozi wa Mkoa huo kuanza mikakati na kampeni maalum kwa ajili yakutangaza ubora wa dagaa wa Kigoma ili kuvutia uwekezaji wa viwanda vidogovidogo na vikubwa kwa ajili ya kuchakata dagaa hao.

Aliendelea kusema kuwa zao hilo la dagaa likitangazwa vizuri, wawekezaji na Taasisi za kibenki wote watakwenda kuwekezana ndio itakuwa mwisho wa dagaa wa Kigoma kutupwa tupwa hovyo kwa sababu ya kukosa soko.

Aidha, aliongeza kwa kusema kuwa uvunaji wa dagaa hao uendane sambamba na utunzaji wa mazalia ya samaki ili upatikanaji wa rasilimali hiyo uwe wa uhakika wakati wote.

"Ndugu zangu, mkakati huu wa kuinua biashara ya zao la dagaa hautafanikiwa kama malighafi haitakuwepo, ili viwanda viweze kuanzishwa ni lazima malighafi ipatikane ya kutosha," alisistiza Ulega

Alisema Serikali imejipanga kuwawezesha wavuvi vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia kuvuna dagaa kwa uhakika na kuwakausha kwa kutumia vichanja vya kisasa ili kupunguza upotevu wa dagaa na kuongeza ubora wake.

Naye, Diwani wa Kata ya Bangwe, Hamisi Besete alisema Serikali kwa Sasa inapoteza mapato mengi kwa sababu Mwalo wa Katonga haujajengwa hivyo kuwafanya wafanyabiashara wa Samaki na Dagaa kukosa sehemu ya kuuzia.

"Mhe. Naibu Waziri, Mwalo wa Katonga ni mkubwa sana hapa Kigoma, tunaomba mtujengee mwalo huu ili Serikali iweze kukusanya mapato ya kutosha hapa kutokana na biashara ya mazao ya Uvuvi, sasa hivi mapato yanapotea kwa sababu Wafanyabiashara hawana sehemu rasmi ya kuuzia samaki wao," alisema Besete

Mbunge wa Kigoma Mjini, Kilumbe Ngenda nae alisema kuwa kwa sababu sasa nchi inaelekea katika uchumi wa buluu ambao unataka kuongezeka kwa kasi ya uzalishaji katika Bahari na Maziwa ili kukuza uchumi wa nchi, Serikali ione uwezekano wa kupunguza baadhi ya masharti ili wananchi wengi waweze kuingia katika uchumi wa buluu
Source : https://www.mifugouvuvi.go.tz/news/ulega-tumejipanga-kuinua-biashara-ya-dagaa-wa-kigoma
 

Wavuvi wanawake Kigoma wapata mtandao wao, shukrani kwa FAO​

29 Julai 2022
Katika kutekeleza lengo namba 8 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu ajira za staha na ukuaji kiuchumi sambamba na namba 5 la usawa wa kijinsia, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo duniani FAO nchini Tanzania, limezindua tawi la tatu la Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi TAWFA kupitia mradi wake wa kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika. Devotha Songorwa wa Radio Washirika KIDS Time FM ya Morogoro nchini Tanzania ameshuhudia uzinduzi na kuandaa taarifa hii.
Sherehe za uzinduzi huo zimefanyika mkoani Kigoma nchini humo ambapo wanawake wavuvi, viongozi wa serikali na wafanyakazi wa FAO walifungua rasmi tawi hili ikiwa ni la tatu nchini humo baada ya mwengine mawili yaliyozinduliwa huko kanda ya Ziwa Victoria na Ukanda wa Bahari ya Hindi.
Uzinduzi huo unafanyika kupitia mradi wa FISH4ACP unaotekelezwa katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi ambapo Mratibu wa Sekta ya Uvuvi Kitaifa kutoka FAO, Oliva Mkumbo akizungumza na Devotha Songorwa wa Redio washirika wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alimueleza lengo ni kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia uvuvi ili kuinua kipato cha familia na kuondokana na umasikini.
“Lengo la kuanzisha jukwaa la wanawake ni kuwawezesha kina mama ili mchango wao utambulike na kuleta athari chanya katika jamii. Tunataka kila mwanamke anayejihusisha na mnyororo wa thamani katika uvuvi anakuwa na sehemu ya kutoa mawazo yake na kubadilishana uzoefu ili kwa pamoja wachangie uboreshaji wa uvuvi,” Anasema Oliva.
Oliva Mkumbo Mratibu wa Sekta ya Uvuvi Kitaifa kutoka FAO

UN News
Oliva Mkumbo Mratibu wa Sekta ya Uvuvi Kitaifa kutoka FAO
Mratibu huyo wa FAO amesema hili halitakuwa tawi la mwisho nchini humo. “Jukwaa rasmi kitaifa lilifunguliwa 2017 ili kuwafikia wanawake wengi wakaanzisha Zone Chapters, Chapter ya Kanda ya Ziwa Victoria 2019, baadaye ikaja ya Uvuvi baharini, Kanda ya Ziwa Tanganyika na baadaye huko tutakuwa na linguine linalohusika na wavuvi kutoka katika maziwa madogo madogo,” Ameeleza Mratibu huyo.
Beatrice Mmbaga ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi Tanzania (TAWFA) anasema jukwaa hili ni sehemu ya kutatua changamoto zinazowakabili kina mama walio katika sekta ya uvuvi.
“Nia ya kuanzisha chombo hiki ni kumfikia mama popote alipo anayejishusisha na samaki na mazao yake Tanzania nzima ndipo sasa tunashuka ngazi za chini katika Mikoa yetu, Kanda na Wilaya ili tuwe na sauti moja kwa sababu kina mama ndiyo asilimia kubwa wanajihusisha na samaki baada ya mavuvi hasa kwenye kuchakata na masoko lakini wana changamoto nyingi sana,” amebainisha Mwenyekiti huyo.
Wanawake wajasiriamali katika sekta ya Uvuvi Tanzania

UN News
Wanawake wajasiriamali katika sekta ya Uvuvi Tanzania
Kwa upande Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia masuala ya Udhibiti Ubora na Mazao ya Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Steven Lukanga amebainisha kwamba wanawake bado wanahitajika kupatiwa elimu ya uvuvi salama na kukidhi mahitaji ya walaji.
“Kikubwa ni kuwajengea uwezo wanawake kutambua viwango vinavyopaswa kuzalisha yale mazao yanayowaendea walaji kwa kuzingatia viwango vilivyopo chini ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwahiyo sisi kama wizara tunashirikiana nao kuhakikisha wachakataji wanawake wanakidhi viwango vinavyotakiwa,”Amesema Lukinga

Source : Wavuvi wanawake Kigoma wapata mtandao wao, shukrani kwa FAO
 
Back
Top Bottom