Elections 2010 NCCR Mageuzi wameniduwaza...

Ramos

JF-Expert Member
May 13, 2010
498
130
Pamoja na ushindi wa kuridhisha wa CHADEMA, ulioniduwaza zaidi ni wa NCCR Mageuzi. From no where, chama tulichokuwa tunakiona kimekufa, kimeweza kuibuka na kubeba majimbo matatu (kama sio mawili) ya ubunge?!!!!!! For me it was amazing. Naaamini strategy yao ya kuandaa watu strong inafaa sana....
 
Mkuu Ramos,

Sio majimbo matatu bali ni majimbo manne tena mkoa mmoja. Hata mimi nimeshindwa kuelewa nini kimetokea mkoa wa Kigoma?

Hivi matokeo ya udiwani yakoje kwenye mkoa huo? Huko kuna haja ya kufanya utafiti kujua nini kimetokea.

Huenda factor kubwa ni wagombea wenyewe, kwamba hao wa NCCR walikuwa wanauzika zaidi ya wengine lakini ilikuwaje mpaka NCCR ikawa na wagombea bora sana kwenye mkoa mmoja tu?

Kama NCCR ina wapenzi wengi huko, kwanini 2005 hawakupata hata mbunge mmoja?

Hongera NCCR kwa mafanikio hayo makubwa huko Kigoma.
 
Itabidi pia tufanye na utafiti wa Jimbo la Kyela kwa nini wanampenda sana Dr!
 
Kwanza hawa wagombea wote wa NCCR walikuwa CHADEMA na kuhamia NCCR ulipotokea mgogoro wa kina kafulila.kwa kifupi ni kwamba wagombea wenyewe walikuwa karibu na wapiga kura wao na wanauzika.labda kitu ambacho ninachojiuliza ni nani aliyewapa elimu ya uraia watu wa kigoma kwani ni tofauti sana na watu wa mikoa mingine.
 
Usishangae mkuu. Wa-Kigoma walikuwa wanaangalia watu sio chama. Vijana wote ni wazuri kwa kuzungumza japo tusubiri matendo yao kwa miaka 5 ijayo kama wataweza kuwafanyia wananchi wao mambo ya maendeleo. Wengi wana washirika CHADEMA, kama Kafulila ambaye alikuwa CHADEMA akaondoka. In other words, ugomvi ndani ya CHADEMA umewakosesha majimbo Kigoma
 
Itakuwa support ya Dr. Slaa na Zitto. Sehemu nyingi Dr. Slaa alikuwa alitambua mgombea wa CHADEMA hakubaliki basi alimtambulisha mwingine wa upinzani anayekubalika zaidi, alifanya hivyo Kibondo, Babati n.k.
 
Pamoja na ushindi wa kuridhisha wa CHADEMA, ulioniduwaza zaidi ni wa NCCR Mageuzi. From no where, chama tulichokuwa tunakiona kimekufa, kimeweza kuibuka na kubeba majimbo matatu (kama sio mawili) ya ubunge?!!!!!! For me it was amazing. Naaamini strategy yao ya kuandaa watu strong inafaa sana....

Mkosamali na Kafulila walijiandaa tangu wakiwa CHADEMA, usije ukawapa credit NCCR kwa kazi ambayo hawakuifanya. Mkosamali alihama kutoka CHADEMA kwenda NCCR mwezi Januari mwaka huu. Pia Kafulila alihama CHADEMA. Wote wawili walianza kujiandaa kugombea tangu wakiwa CHADEMA, so walipoamua kuhama waliondoka na mtandao wa watu wao na ndio uliowasaidia zoezi la uwakala na kupiga debe pia.
 
Mkuu Ramos,

Sio majimbo matatu bali ni majimbo manne tena mkoa mmoja. Hata mimi nimeshindwa kuelewa nini kimetokea mkoa wa Kigoma?

Hivi matokeo ya udiwani yakoje kwenye mkoa huo? Huko kuna haja ya kufanya utafiti kujua nini kimetokea.

Huenda factor kubwa ni wagombea wenyewe, kwamba hao wa NCCR walikuwa wanauzika zaidi ya wengine lakini ilikuwaje mpaka NCCR ikawa na wagombea bora sana kwenye mkoa mmoja tu?

Kama NCCR ina wapenzi wengi huko, kwanini 2005 hawakupata hata mbunge mmoja?

Hongera NCCR kwa mafanikio hayo makubwa huko Kigoma.
Mhe Kafulila alikuwa Kada wa CHADEMA. hao wengine walikuwa ama CHADEMA au CCM. Kura za maoni ziliwafanya wahamie NCCR. Mfano ni Mbunge wa Muhambwe. Kwenye kura za maoni za CCM kulitokea Mizengwe. Yeye na Ntagazwa wakakimbia CHADEMA wakamchukua Ntagazwa, Huyo akaenda NCCR. Kwa hiyo haishangazi na wala si jitihada za NCCR bali ni bahati tu kwa Chama hicho.
 
Usishangae mkuu. Wa-Kigoma walikuwa wanaangalia watu sio chama. Vijana wote ni wazuri kwa kuzungumza japo tusubiri matendo yao kwa miaka 5 ijayo kama wataweza kuwafanyia wananchi wao mambo ya maendeleo. Wengi wana washirika CHADEMA, kama Kafulila ambaye alikuwa CHADEMA akaondoka. In other words, ugomvi ndani ya CHADEMA umewakosesha majimbo Kigoma

Well said, na hao wote sitashangaa kusikia Zitto kabwe ni mentor wao au aliwapa msaada mkubwa. Chadema inapaswa kutulia na kushikamana kama ilivyokuwa wakati wa kampeni. miaka mitano ni mingi ccm hawatanyamaza watajitahidi kuisambaratisha. maumizi ya kupoteza jimbo la kawe ambako wakuu wote wa cccm, serikali, mabalozi, matajiri wakubwa na usalama wa taifa wanaishi si madogo. hawawezi kutulia, watajitahidi kuivuga CHADEMA ili kulipa kisasi.
 
Pamoja na ushindi wa kuridhisha wa CHADEMA, ulioniduwaza zaidi ni wa NCCR Mageuzi. From no where, chama tulichokuwa tunakiona kimekufa, kimeweza kuibuka na kubeba majimbo matatu (kama sio mawili) ya ubunge?!!!!!! For me it was amazing. Naaamini strategy yao ya kuandaa watu strong inafaa sana....

Labda jambo la kujiuliza ni kwa nini Kigoma tu? mwisho wa reli. Ama kwa kuwa Hashim Rungwe anatokea huko?
 
Poleni ndugu zangu,

Ni kwamba Daniel Nsanzugwanko mbunge aliyepita alikuwa mwanachama wa NCCR Mageuzi mwaka 1995, alitumia resource nyingi kukijenga chama huko na alikubalika sana na inadhaniwa alishinda katika uchaguzi ule akachakachuliwa live, baada ya hapo akajisalimisha CCM badala ya kuendelea kujenga upinzani dhabiti, mwaka 2005 alirudi kugombea baada ya kifo cha mbunge wa jimbo hilo.

Kwa kuwa watu walifikiri bado ana mawazo ya kuleta maendeleo walimwamini tena, kumbe alikuwa ameshabadilika na hakufanya lolote la kujivunia Kasulu, wakati wa kampeni alikuwa mkali kama pilipili kwa watu waliokuwa wakiuliza maswali ya kutaka kujua alifanya nini au kwa nini alihama NCCR mageuzi, kosa alilofanya kubwa ni kupiga watu vibao kwenye mikutano ya hadhara eti ni vibaraka wa upinzania wakati yeye alikuwa huko.

Hivyo NCCR Mageuzi ina nguvu sana huko sababu ya Mheshimiwa Nzanzugwanko kuweka misingi imara, siyo Kasulu na Kibondo bali hata Kigoma Ujiji mwasisi wa mageuzi huko na Dr.Aman Walidi Kabour aliyefanya Chadema ikubalike mpaka leo unawaona akina zito na wengine ni matunda ya akina Kabuor.

Kivuli chake ndiyo kimemwangusha Bwana Nsanzugwanko, siyo majimbo hayo tu Kasulu magharibi napo CCM iliponea chupuchupu kwa tofauti ya kura 4.
 
Mkuu Ramos,

Sio majimbo matatu bali ni majimbo manne tena mkoa mmoja. Hata mimi nimeshindwa kuelewa nini kimetokea mkoa wa Kigoma?

Hivi matokeo ya udiwani yakoje kwenye mkoa huo? Huko kuna haja ya kufanya utafiti kujua nini kimetokea.

Huenda factor kubwa ni wagombea wenyewe, kwamba hao wa NCCR walikuwa wanauzika zaidi ya wengine lakini ilikuwaje mpaka NCCR ikawa na wagombea bora sana kwenye mkoa mmoja tu?

Kama NCCR ina wapenzi wengi huko, kwanini 2005 hawakupata hata mbunge mmoja?

Hongera NCCR kwa mafanikio hayo makubwa huko Kigoma.

Mkuu Mtanzania,

Pamoja na factors nyingine, uongozi wa CCM mkoa wa Kigoma una matatizo. Kwenye baadhi ya majimbo kulikuwa na madai kwamba fedha nyingi zilitumika kwenye kura za maoni na hivyo kuna wagombea ambao hawana sifa walishinda. Nadhani kuna mgombea mmoja aliandikwa sana magazetini kwamba ana kashfa za ujambazi, mambo ya albino na ufisadi pia. Lakini mgombea huyo alikuwa kipenzi cha Mwenyekiti wa Mkoa. Kwenye jimbo hilo wananchi walionyesha hasira za wazi kwa kumpa mpinzani 97% ya kura, kitu ambacho ni nadra sana kwa mgombea wa CCM .... watanzania si mabwege tena.

Kama unakumbuka Katibu Mkuu wa mkoa alipewa barua ya uhamisho saa sita usiku, siku ambayo JK alienda kupiga kampeni mkoani Kigoma. Mama wa watu alitakiwa akaripoti Makao Makuu Dodoma. Sasa hivi huyo Mama atakuwa anashangilia tu maana alikuwa mstari wa mbele kuwapinga baadhi ya wagombea Ubunge na Udiwani kwenye majimbo ya mkoa na alikuwa na valid reasons ambazo Mwenyekiti wa mkoa hakuziona.

Tatizo la mafisadi wa CCM wanaamini kwamba fedha inaweza kununua kura, which is wrong maana watu wameamka na wana uelewa wa kutosha. Mgombea yeyote akienda kujikita huko vijijini kwa miaka 2 anawasomesha wapiga kura, ukija uchaguzi lazima wampe kura hata kama kuna mtu ataenda kumwaga fedha, khanga, fulana na kofia.
 
uchaguzi huu watu walishachoka na CCM na watu wao, kwa hiyo watu wengi walikuwa hawachagui Chama bali mtu, na bahati ikatokea NCCR wameweka watu ambao wanakubalika, hivyo hao wa kigoma hawajachagua chama bali walichagua watu
 
Kwa kila kiti kinachoenda upinzania, kwangu ni sherehe.
haiwezekani tukawa na bunge la kihafidhina linalotumika kama mhuri wa kipuuzi na wapuuzi walioko madarakani
 
Kwanza hawa wagombea wote wa NCCR walikuwa CHADEMA na kuhamia NCCR ulipotokea mgogoro wa kina kafulila.kwa kifupi ni kwamba wagombea wenyewe walikuwa karibu na wapiga kura wao na wanauzika.labda kitu ambacho ninachojiuliza ni nani aliyewapa elimu ya uraia watu wa kigoma kwani ni tofauti sana na watu wa mikoa mingine.

Hao watu wa Kigoma si unaujua ni majirani na DRC.
 
Ni vigumu kueleza lakini siyo siri NCCR inapendwa "naturally" huko kigoma. Nilikuwepo mwaka 2005 niliona bendera nyingi sana za NCCR mpaka vijijini. CCM na CHADEMA ni chaguo lao la pili baada ya kumkosa mtu bora wa NCCR. Kulikuwepo kijana mmoja machachari kutoka maeneo ya Nguruka (kabla ya enzi za zito) alikuwa anapendwa kama almasi na alikuwa NCCR.

Ila muhimu zaidi ni mkoa ambao umesahaulika mno na watu wake wanajitambua. Ungefikiri vitisho vya CCM vya amani wangeogopa kuliko mikoa mingine maana wakimbizi huanzia kwao, sivyo na kwa hiyo hii factor ya AMANI ambayo CCM inaitumia kama limbwata haifanyi kazi. Pengine interaction na wakimbizi imewasaidia kujua ni kwa nini watu upigana kuliko kuwa kondoo wanaochinjwa bila hata kurusha miguu. Bravoo Batama Imana Ibhaaye!
 
Nadhani tufanye utafiti wa CCM kuchakachua matokeo, nini kifanyike ili kuzuia kisitokee tena.
 
ongera NCCR, ila kwa ushauri mbatia achana na Kwenda mahakamani kuishitaki CHADEMA, unajisumbua BURE
 
Itabidi pia tufanye na utafiti wa Jimbo la Kyela kwa nini wanampenda sana Dr!

Mkuu Shalom,

Sawa unaweza kwenda kufanya utafiti wako lakini majimbo kama Kyela yako mengi tu Tanzania ambako wananchi waliamua kuwabakiza walioko madarakani.

I hope uwezo wako ni zaidi ya vijembe vya JF. Wengine tulijitolea kugombea, tumeshindwa na tunasonga mbele na maisha, nafikiri ndio demokrasi tunayohubiri hapa JF. Kama ulitegemea watu tuwe ICU, hapo utasubiri muda mrefu sana (Dua la kuku halimpati mwewe).

Kama kufanya hivyo ni tatizo kwako, well, that is and will not be my problem! Uzuri wake, tulioshindwa mwaka huu tuko wengi tu ikiwa ni pamoja na hao unao waabudu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom