NBC: Yanga SC 1-0 Ihefu FC: Uwanja Benjamin Mkapa

babu onyango

JF-Expert Member
Jan 12, 2023
329
814
Machampioni watetezi wa ligi kuu nchini Tanzania Young Africans S.C almaarufu Yanga leo wanashuka dimbani kukabilia na Ihefu katika mwendelezo wa ligi kuu ya Nbc...

Mchezo huo utakuwa mgumu kwa timu zote kwani Yanga wanataka kushinda ili kulipa kisasi cha kuvunjiwa rekodi yao ya unbeaten na Ihefu kwenye mechi yao ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Nov 29 mwaka Jana.

Pia ushindi Kwa Yanga utaisaidia kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi huku Ihefu nao wakiitaji alama zote tatu ili kujinasua kutoka kwenye nafasi za mwisho mwisho mwa msimamo wa ligi.

Utakuwa nami mwanzo paka mwisho wa mbungi hili

Vikosi vya timu zote ni kama ifuatavyo

""""""""""""""""""'''''
00' Mpira umeanza Kwa Kasi sana hapa Uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye Dakika 90 za kisasi Kwa Wananchi

03' Ihefu wanapata faulo nje kidogo ya lango la Yanga ila mpira wa Never Tigere unaokolewa na mabeki wa Yanga

05' Yanga wanatandaza soka safi hapa langoni wa Ihefu lakini Tuisila Kisinda anaotea

08' Kisinda anapiga shuti kali langoni mwa Ihefu lakini linaenda juu ya lango

10' Kona ya kwanza ya mchezo inapigwa kuelekea lango la Ihefu ila golikipa wa Ihefu anaondoa hatari ile

28' Shambulizi Kali langoni mwa Ihefu lakini Kisinda anapoteza nafasi pale

HT' Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimetamatika milango yote bado migumu
Tukutane kipindi cha pili

46' Kipindi cha pili kimeanza hapa Uwanja wa Benjamin Mkapa

62' Yanga wanafanya mabadiliko, anaingia Kennedy Musonda kuchukua nafasi ya Kisinda, mashabiki wanamshangilia

64' Gooool.... Fiston Mayele anaifungia goli la kwanza Yanga

70' Musonda anaachia shuti kali lakini linapanguliwa na golikipa wa Ihefu.
Huyu Musonda anaonekana ni mtu hatari sana

88' Yanga bado wanaliandama lango la Ihefu kama nyuki na wanapoteza nafasi nyingine ya wazi kupitia Dickson Ambundo

90' Zimeongezwa dakik 2 hapa
Naaam mpira umekwisha hapa Benjamin Mkapa, Wananchi wanafanikiwa kulipa kisasi na kuondoka na ushindi wa bao Moja goli likifungwa na mfalme Fiston Mayele.

20230116_180727.jpg
20230116_180732.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom