NBAA yatoa matokeo leo 28.06.2012

Rogie

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
7,581
6,675
Heshima Mbele Wakuu..
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi-NBAA leo imetoa matokeo ya watahiniwa wake waliofanya mitihani mwezi Mei mwaka huu. Niwapongeze wale woote waliofanya vizuri katika matokeo hayo. Pongezi za dhati kabisa ziende kwa mkubwa wangu kwa kufanikiwa kupata CPA. Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa hatua hiyo.

Mum and dad..this is for you..Although you are gone ,we still go on with the primary you have set, Barakallah.
 
WATAHINIWA 1,845 kati ya watahiniwa 3,857 waliofanya mitihani ya Uhasibi na Ukaguzi wa Hesabu nchini(NBAA) Mei mwaka huu, watarudia mtihani huo baada ya kufanya vibaya katika mtihani huo.Watahiniwa 797 sawa na asilimia 31 ndio waliofaulu mitihani hiyo huku watahiniwa 1,845 sawa na asilimia 47 wanatarajia kurudia mitihani hiyo baada ya kufeli.

Akitoa taarifa hiyo juzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Pius Maneno alisema watahiniwa 797 sawa na asilimia 31 ndio waliofaulu katika mitihani ya Uhasibu na Ukaguzi wa mahesabu kwa mwaka huu.

"Watahiniwa 797 sawa na asilimia 31 wamefaulu mtihani wa uhasibu na ukaguzi wa hesabu huku watahiniwa 1,215 watarudia mtihani huo na wengine 1,845 sawa na asilimia 47 hawakufanya mtihani, "alisema.
Maneno alisema matokeo ya mitihani hiyo yalitangazwa baada ya kukaa kikao cha 155 cha wakurugenzi wa bodi hiyo.

Pia watahiniwa 259 wamefaulu mitihani ya shahada ya juu ya Uhasibu nchini yaani CPA na idadi hiyo inafanya wahitimu waliofaulu mitihani ya CPA kufikia 4,135 tangu mitihani hiyo ianzishwe mwaka 1975.

Maneno alisema katika ngazi ya uandishi na utunzaji wa hesabu( ATEC 11) watahiniwa 35 kati ya 127 walifaulu mtihani huo huku watahiniwa 57 wakitarajia kurudia mtihani huo.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa katika ngazi ya awali ya mitihani ya uandishi na utunzaji wa hesabu (ATEC 1), watahiniwa 37 kati ya 110 walifauli mitihani hiyo sawa na asilimia 33.

Vile vile katika ngazi ya Module E watahiniwa 319 kati ya 2161 walifaulu mtihani huo huku katika ngazi ya mwisho watahiniwa 258 kati ya 1026 sawa na asilimia 25 ndio wamefaulu mtihani huo.

Sanjari na matokeo hayo pia bodi hiyo ipo katika mchakato wa kubadilisha mitalaa ya masomo ambapo mitalaa mipya itaanza Novemba mwakani na hatua hiyo inalenga kuboresha mfumo wa masomo.

Vile vile bodi hiyo imepanga Novemba 6 hadi 9, mwaka huu watahiniwa wote waliofanya vibaya katika mitihani yao kurudia na matokeo yatawekwa katika tovuti ya bodi .

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom