NBAA inakomoa watahiniwa badala ya kuwawezesha na kuwasaidia

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Jana napiga story na mdogo wangu ambae anafanya mitihani ya NBAA ananiambia juzi hapa walifanya mitihani migumu hadi wakaongezewa muda kwenye chumba cha mtihani zaidi ya dakika 30.

Nikajiuliza kwani NBAA kabla hawatoa mitihani yao hua hawaifanyii moderation kuona kama inaweza kufanyika kwa wakati hadi ifike kwenye chumba cha mtihani ndio wajue kua mtihani ni mgumu ama mrefu hauwezi kufanyika ndani ya muda uliopangwa?

Binafsi nategemea hizi profession bodies ziwasaidie wanafunzi zaidi kuliko kuwakomoa. Wakati Dunia inabadilika na kujali zaidi ujuzi na ufahamu sisi bado wataalam wetu akili zao zimeganda kwenye mitihani migumu ya kukomoana kwa kudhani kua ukifanya mtihani mgumu ama swali gumu basi wewe ndie unajua, wewe ndie mwenye akili.

Mimi binafsi ni mhasibu mwenye cpa ingawa si practice uhasibu miaka mingi sana. Sasa I thought NBAA wanabadilika lakini naambiwa bado wana mentality ile ile ya kizamani ya kutunga mitihani ya kukomoana. Nimeambiwa hata ACCA wamebadilika sana lakini wenzetu NBAA bado wana mawazo ya karne iliyopita.

Karne hii ya 21 waajiri wengi hasa wa kimataifa wanataka mtu mwenye skills, kwamba you got the skills to make the job done, not papers.

NBAA badilikeni, boresheni taaluma ya kihasibu, msikae kutunga tu mitihani migumu na kudhani mnawafanya wahasibu wawe competent. Leo hii watu wengi wana CPA lakini hawajui kitu, hii ina maana kwamba mnawakaririsha wafaulu mitihani.
 
Watu kazi wanazijulia kazini. Hata wafanyakazi wa zamani. Hao wenye CPA wa zamani kazi walizijua walipoingia kazini.
 
Najiuliza sn kwa nn bodi hazitoe training kuongeza watu skill zinazo saidia wahusika bali zinatoa mitiani ya chuo, nauna kuta chuoni mwalimu alifuata muogozo wao na kutoa mapast paper ya kwao kabisa. kwa mm sioni faida ya hawa watu zaidi ya kupiga pesa na masheria yasio na faida kwa wahusika.

naisi ni muda wakuangalia maitaji na sio kuiga kila kitu cha mabeberu tutakua nyuma miaka yote.

Tunaitaji skilled people, sio vyeti safi.
 
Marehemu baba yangu alikuwa anasahihisha hii mitihani na wakati mwingine alikuwa invigilator, anasema kabla ya kusahihisha alikuwa anafanya huo mtihani mwenyewe., Sababu ya kufanya mtihani ninkuangalia kama muda uliowekwq ni sahihi na pia kutengeneza marking scheme ambayo atailinganisha na ile waliyopewa kutumia.

Kuna kipindi aligundua hata marking scheme ilikuwa na makosa kiasi wanafunzi wanafelishwa bila sababu ya msingi.
 
Wanairudisha enzi za

Utouh
Daniel Yona
Mzee Mengi
Musa Assad n.k

Siku hizi uhasibu hata kama ni form four failya ukisoma TALLY, MYOB na Excel vizuri unafanya kazi. Teknolojia nyoooko sana
 
Back
Top Bottom