LEARNED BROTHER
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 585
- 831
Wakuu habari,
Nimekuwa member wa JF since 2012, tangu wakati huo sijawahi kuanzisha thread yeyote isipokuwa nimekuwa mchangiaji wa baadhi ya mada zinazowasilishwa JF sanjari na kusoma thread mbalimbali.
Nimeamua kuleta mada humu ili ni-share nanyi jambo linalonisibu pengine naweza kupata mawazo yatakayonisaidia kuvuka salama.Kwangu mie mwaka 2015 ulikuwa wenye changamoto nyingi ambapo nyingine zilinikatisha tamaa.
Kwamba katika mwaka huo nilipanga kufanikisha mambo mengi ikiwemo kumuabudu Mungu katika roho na kweli, kufunga ndoa, kujiendeleza kitaaluma kwa kusoma masters degree, kuendeleza ujenzi wa nyumba waishiyo wazazi wangu, kupunguza kiwango cha utumiaji wa pombe, kununua kiwanja mahali ninapoishi, kufanya saving n.k.
Nasikitika kwamba mengi kati ya niliyopanga sijafanikisha hata moja. Kuhusu kumuabudu Mungu, mahudhurio yangu yamekuwa hafifu kanisani ninakoabudu @AIC-T, na mara kadhaa ninekuwa nikianguka dhambini. Kuhusu kufunga ndoa, binti niliyekuwa naye kwenye uhusiano aliniacha.
Kuhusu kujiendeleza kutaaluma sikufanikisha kukamilisha taratibu zinazotakiwa. Kuhusu utumiaji wa pombe kuna nyakati nilikunywa kupita kiasi ( I normaly drink Castle lite/ ndovu au Ballantines). Kwamba kwa kiasi fulani nilifanikiwa kubadili makazi ya wazazi ingawa sio kwa kiwango ninachotaka.
Kutokana na hali hiyo, wakati wa mwaka mpya 2016, nilipanga kufanikisha yote yaliyoshindikana in 2015. Hata hivyo nimeanza kuona dalili mbaya za utekelezaji wa malengo hayo, kwa kuwa hata yale mambo madogo nilokusudia kuyafanya in this January sijayafanikisha. Kwamba kanisani bado sijaanza kwenda.
Lengo la ndoa pamoja na kwamba ni changamoto kumpata mtu sahihi, pia bado sijawa in a serious relationship. Kuhusu pombe ndo mweeeh, pamoja na hali ngumu ya January but this month nimekunywa sana. Hali hii imenifanya nijifanyie tathimini upya na kuona ipo haja ya kubadili mwenendo wa maisha niishio.
Eee Mwenyezi Mungu nisaidie.