Nazi Zao Yatima Hana Mzazi Hana Mlezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nazi Zao Yatima Hana Mzazi Hana Mlezi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by chema, Dec 25, 2010.

 1. c

  chema Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikianza kwa kunukuu maneno ya Rais Kikwete kuwa zao la minazi limepatwa na " Ugojwa usiotibika kwa sasa ",nakuwataka wakulima wa zao la mnazi kulima kokoa kama zao mbadala .Wazo kama hili si geni ,kwani hapo nyuma wakulima huko Mwanza walitakiwa kubadilisha zao la pamba kwa kahawa .

  Inaniwia vigumu kukubaliana na Rais hasa pale alipowahakikishia wakulima wa zao la minazi kuwa atawapa wataalamu kushirikiana nao ili kuweza kufanikisha zoezi hili la kubadilisha Mnazi kwa Kokoa, na ndiyo hapo sera ya kilimo kwanza ninapohisi kushindwa.

  Lengo kuu la kilimo kwanza ni kumkomboa mkulima mdogo toka kilimo cha kuchumia tumbo hadi kilimo chenye kunyanyua kipato cha mkulima na serikali . Na ndipo hapo ninakuwa na shaka na mkulima wa minazi kumuona kuwa ni yatima hana mzazi wala mlezi.

  Minazi mingi iliyopo imetokana na mashamba ya kurithi ambayo huenda tumerithi toka kwa wazee wetu ama mara baada ya harakati za ukombozi wananchi kujimilikisha kama matunda ya uhuru.

  Kutokana na umri mrefu na kutoboreshwa mashamba kutokana na uwezo duni au tamaa za wenye mashamba kwa kuangalia mavuno bila kutahadhari uboreshwaji wa zao hilo kwa kukuza miche mipya na uwekaji wa mbolea , zao hili limejikuta siku hadi siku likiwa linatokomea.

  Miaka ya 80 hadi 90 zao hili lilikuwa likishughulikiwa na Mradi wa Kitaifa wa Kuendeleza Zao la Mnazi , vipi iwezekane kutoa wataalamu kuwezesha kubadilishwa zao moja kwenda lengine na kusiwezekane kutoa wataalamu wa kuendeleza na kuboresha zao lililopo.

  Ushauri wangu kwa wizara husika hasa ya kilimo na mazingira,jaribuni kufanya utafiti kujua jinsi gani ya kuokoa utowekaji wa zao la mnazi na pia ili serikali ijiridhishe haina budi kuchukua uzoefu wa nchi nyengine mfano wa Sri lanka, kwani kisiwa hichi kinafaidika sana na zao la Mnazi.

  Ukitazama athari iliyopo ni kuwa,zao la mnazi likiboreshwa litanyanyua kiwango cha maisha kwani nazi hutumika sana kwa mapishi,kutoa mafuta na ni kiburudisho cha koo na uboreshwaji wake utanyanyua uchumi kwa nchi na wananchi .

  Zao la Mnazi ni alama kuu katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki na ukiangalia kwa makini kutokomea kwake ni sawa na kuondoa meno halisi na kuyabadili kwa meno bandia.
  Wako : mtazamojamii.blogspot.com
   
Loading...