Nazeeka kwa kasi ya ajabu mno. Nifanye nini?

WhoWeBe

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
2,301
4,243
Yeyote aliyeniona miaka miwili au mitatu tu iliyopita ananishangaa na kutishika.

Walionilea na niliowakuta wakiwa wakubwa sasa ninawapita. Mvi zimetamalaki kidevuni na kichwani mara nne yao.

Nimegeuka kuwa kichekesho na mshangao kwa wanafamilia tunapokutana kwenye matukio yanayotukutanisha wanafamilia. Nina aibu muda wote.

Hata mwili, naona una dalili zote za kizee, kuumwa kiuno, kuchelewa kuitikia (response), na usingizi wa hovyo hovyo.

Yote haya yanatokea nikiwa na miaka 40 tu. Age mates wangu wengi wanaonekana km wana 20+ au 30+. Ni wa tatu kuzaliwa lakini naonekana wa kwanza kiumri, si kwa 'kukochopaa' huku.

Nimebahatika, mkate wangu wa kila siku siupati kwa kutumia nguvu nyiiingi za kilimo au kubeba zege, lakini kwa kasi ya kuzeeka, mimi ndo naonekana ninafanya kazi ya ukulima zaidi yao.

Msaada tafadhali.
 
Yeyote aliyeniona miaka miwili au mitatu tu iliyopita ananishangaa na kutishika.

Walionilea na niliowakuta wakiwa wakubwa sasa ninawapita........mvi zimetamalaki kidevuni na kichwani mara nne yao.

Nimegeuka kuwa kichekesho na mshangao kwa wanafamilia tunapokutana kwenye matukio yanayotukutanisha wanafamilia........nina aibu muda wote.

Hata mwili, naona una dalili zote za kizee.....kuumwa kiuno, kuchelewa kuitikia (response), na usingizi wa hovyo hovyo.

Yote haya yanatokea nikiwa na miaka 40 tu. Age mates wangu wengi wanaonekana km wana 20+ au 30+. Ni wa tatu kuzaliwa lakini naonekana wa kwanza kiumri.......si kwa 'kukochopaa' huku.

Nimebahatika, mate wangu wa kila siku siupati kwa kutumia nguvu nyiiingi za kilimo au kubeba zege, lakini kwa kasi ya kuzeeka, mimi ndo naonekana ninafanya kazi ya ukulima zaidi yao.

Msaada tafadhali.....
Aisee, yani hata mimi nimelala usika, kuamka asubuhi nakuta uso umetelemuka!
Yaakh...balaa!
 
Yeyote aliyeniona miaka miwili au mitatu tu iliyopita ananishangaa na kutishika.

Walionilea na niliowakuta wakiwa wakubwa sasa ninawapita. Mvi zimetamalaki kidevuni na kichwani mara nne yao.

Nimegeuka kuwa kichekesho na mshangao kwa wanafamilia tunapokutana kwenye matukio yanayotukutanisha wanafamilia. Nina aibu muda wote.

Hata mwili, naona una dalili zote za kizee, kuumwa kiuno, kuchelewa kuitikia (response), na usingizi wa hovyo hovyo.

Yote haya yanatokea nikiwa na miaka 40 tu. Age mates wangu wengi wanaonekana km wana 20+ au 30+. Ni wa tatu kuzaliwa lakini naonekana wa kwanza kiumri, si kwa 'kukochopaa' huku.

Nimebahatika, mkate wangu wa kila siku siupati kwa kutumia nguvu nyiiingi za kilimo au kubeba zege, lakini kwa kasi ya kuzeeka, mimi ndo naonekana ninafanya kazi ya ukulima zaidi yao.

Msaada tafadhali.
Paka supa blaki
 
Unatakiwa uufurahie uzee wako kama ulivyoufurahia utoto na ujana pia.

Vyote vina raha yake.

Mimi nipo 30s lakini naonekana wa 20s na huwa sifichi miaka yangu na nina furahia na mvi zangu kidevuni.

Ukijitahidi kuficha uzee ndivyo unazidi kuzeeka sababu ya stress.

Ila usipojali uzee wako basi unakuwa kijana zaidi maana hujali.

Mwisho wa siku uzee au ujana unategemea na fikra zako
 
Unatakiwa ufurahie uzee wako kama ulivyouufurahia utoto na ujana pia.

Vyote vina raha yake.

Mimi nipo 30s lakini ninaonekana wa 20s na huwa sifichi miaka yangu na nina furahia na mvi zangu kidevuni.

Ukijitahidi kuficha uzee ndivyo unazidi kuzeeka sababu ya stress.

Ila usipojali uzee wako basi unakuwa kijana zaidi maana hujali.

Mwisho wa siku uzee au ujana unategemea na fikra za mtu mwenyewe
 
Back
Top Bottom