Nayaonea Huruma Maisha yangu

Nayaonea Huruma Maisha yangu

Wakuu Habari za Jioni.

Kiuhalisia Zaidi ya Miaka 17 nimekuwa mtu wa kusoma na sijawahi kuyaexperince zaidi maisha ya mtaani zaidi ya likizo.

Lengo La kuja Humu ndani wakui tangu nimemaliza chuo nimekuwa sipi sawa kabisa yaani mpaka nashindwa kujielewa naelekea wapi juu ya maisha haya.

1..Nimekuwa mtu wa kuogopa watu kupita maelezo yaani ni mtu wa kujifungia ndani yaani Hata kanisani nashindwa kwenda tena na Hata kumeet na watu siwezi kabisa.

2.Maisha yangu ya mahusiano yamekuwa ya ovyo siko na interest ya kupenda tena maana nimejikuta nafeel happy nikiwa alone kuliko vyovyote vile.

3.Nikianzisha jambo simalizi imagine kuna bussiness nilihitaji nianze nikawa nashindwa kuanza mpaka mtu mmoja akaniinfluence ndo nikajikuta ninaenda kuchukua product lakini bado sijaanza hata kufanya.

4..Ninakuwa mtu mbaya mpaka ninajishangaa yaani Sijui nitakuwaje huko mbele.

Msaada Hata wa Ushauri juu ya Haya Maana yale niliyoyatarajia hayajawa vile nilivyotarajia.
Mkuu huna tofauti namm, Niko mkoa x Kuna sehemu nimepata ajira..mpaka Sasa yapata miezi Kama mitano...
Nimekua mtu wa kushinda ndani Kila ninapotoka kazinii....ninaogopa kuchanganyana na wadau kitaa....
Mida yangu yakutoka labda wakati wa jioni ndio nakua comfortable Ila mchana nikiwa natembea nahisi Kama watu wananiangalia mm tu...

Najaribu kujiforce kuchanganyana lkn nashindwa....
Huwezi amini mpaka mda huu nipo Ila cna rafki hata mmoja tofauti na wale tunafanya kazi pamoja...

Natamani sana kuwa mtu wa watu ka wengine Ila cjui nifanyaje ili niweee
 
Unajua am church Boy btw sasa mara nyingi kanisanj kuna ile hali ya kuulizana upo wapi unafanya nini!? Ulikuwa wapi!? Mara mbona hauonekani sikuizi!? Maswali mengi kama hayo uwa naonaga very difficult kuyajibu na uwa naona kama kuna watu baadhi wananifuatilia maisha yangu
Duh pengine Kuna roho imekuingia inakufanya uwe ivyo!!
mh sijui Sana Mambo hayo sikiliza tu ushauri wa wakuu .
 
Kama unajifungia sana ndani hujifungi na magoli mwenyewe(Nyeto)Huwa inapunguza kujiamini,Tatizo mkishaenda chuo mnajua mkirudi mtaajiriwa ofisi ya maana,nyumba ya ofisi au upange nyumba nzima na mkopo wa gari lakini haiko hivyo,JIAJIRI.kinachoanzia juu ni mvua tu vingine vingi huanzia chini msomi Ujinga Mtupu
 
Dont worry mkuu, you are not alone , vipi draft unaidea nalo ? , i mean unaweza kucheza mchezo wa draft ?. If the answer yes, hebu jaribu kutafuta hii App inaitwa online checker , wenzio tumejificha huku , just image i can play draft with different people around the whole , good enough basing on my skills, i have managed to get alot of friend from different angles of the world to chart with while i' m playing it .

Hivyo kwasasa sina haja yakwenda vijiweni kucheza coz sipend kuonana na watu plus corona na mambo mengine mengine mengi hii app imekuwa msaada kwangu kuliko unavyofikiri.

Ifike mahari tujikubali vile tulivyo kuwa hatuna uwezo mkubwa wa kusocilize na watu , hivyo si vibaya tukajaribu kujitengenezea dunia yetu ya kufikirika japo kujipa furaha kidogo.
Mbona sikuoni kwenye ilo game
 
Wewe una stress tu za maisha na si kitu kingine...

Watu wa namna yako huwa mkipata hela mnakuwa na fujo laana
 
Huko ulipokuwa unasoma, ulikuwa peke yako?

Acheni kukuza matatizo ambayo hayapo.
 
Mkuu huna tofauti namm, Niko mkoa x Kuna sehemu nimepata ajira..mpaka Sasa yapata miezi Kama mitano...
Nimekua mtu wa kushinda ndani Kila ninapotoka kazinii....ninaogopa kuchanganyana na wadau kitaa....
Mida yangu yakutoka labda wakati wa jioni ndio nakua comfortable Ila mchana nikiwa natembea nahisi Kama watu wananiangalia mm tu...

Najaribu kujiforce kuchanganyana lkn nashindwa....
Huwezi amini mpaka mda huu nipo Ila cna rafki hata mmoja tofauti na wale tunafanya kazi pamoja...

Natamani sana kuwa mtu wa watu ka wengine Ila cjui nifanyaje ili niweee

Mbona kujichanganya ni easy mkuu, kama ni mshabiki wa mpira wa miguu kupata marafiki wapya ni rahisi mno binafsi nilikuwa kama wewe kwa kiasi fulani ila ushabiki wa mpira umesaidia sana kunipa watu wapya kwnye maisha yangu tena wa kila namna. Hata nikiwa na stress nikiingia tu mpirani stress zinapungua kama sio kuisha kabisa
 
Mwanaume hutakiwi kuwa mwoga, ondoa wazo kuwa huwezi kwanini usiweze wengine wamewezaje?
 
Ukiendelea kusema huwezi utakuwa huwezi kweli ondoa hilo wazo kwenye kinywa chako, fuata ushauri unaopewa huku wa kujichanganya na watu mbalimbali halafu ulete mrejesho baadaye, kila lakheri.
 
mwenyewe umejiita "ujinga mtupu" unategemea nini katika maisha??maneno HUUMBA.
 
Huko ndani unakojifungia huwa hupigi magoli ya kujifunga?
Na hii inaweza kuwa sababu kwani tabia ya kujichua na kuangalia pornography hupoteza uwezo wa mtu kujiamini na kufikia hatua ya kujikataa sababu pia ni mlango wa roho chafu kuingia katika maisha ya mtu pamoja na mikosi ya kutosha na unaweza kujikuta unaoa au unaolewa na roho hizo chafu na katika suala la uzalishaji unakuwa mvivu sana kwani hata mwili na akili vinakuwa vinachoka. Kama una tabia hizo hapo juu kuna uwezekano hata utendaji wako kitandani ukawa ni duni, Athumani kichwa kidogo anachoka mapema. Lakini inawezekana ukatoka huko na ukarudi katika hali nzuri, mshirikishe mtu anayekuamini udhaifu huu na hapo ni hatua nyingine kubwa utakuwa umefanya pamoja na kuteketeza vyanzo vya picha au video za ngono na safisha simu yako na jifunze taratibu kujiamini kwa kuanza kufanya mazoezi ya kukimbia jioni au asubuhi mtaani.Mafanikio katika jambo lolote unahitajika kuwa mvumilivu na kuwa na bidii na ubunifu kila inapoitwa leo na jitahidi uwe na nidhamu ya fedha, weka akiba katika kidogo unachopata na kuwa na bajeti katika kila jambo.Bado mapema sana, kaza buti mtoto wa kiume.
INAWEZEKANA KURUDIA AU KUWA NA UJASIRI NA KUENDELEA NA MAISHA NA UTAFANIKIWA. "NO RETREAT NO SURRENDER, ALUTA CONTINUA".
 
Back
Top Bottom