Nay wa Mitego apata pigo kubwa

Nay wa Mitego apata pigo kubwa

ricktz

Member
Joined
Jun 25, 2016
Posts
20
Reaction score
11
Nay wa Mitego anauanza mwaka 2018 kwa kupitia mtihani huu mkubwa sana kwake akiwa kama msanii. Hii ni baada ya wadukuzi kuweza kuichukua akaunti yake ya [HASHTAG]#YouTube[/HASHTAG] na kufuta video zake zote ambazo aliziweka kwenye akaunti yake hiyo, yaani video zote ambazo ameziweka kwenye akaunti yake toka aanza muziki zimefutwa.

Mr Nay ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kuandika kuwa
. “Kwa miaka zaidi ya 17 nahangaika na Muziki anatokea mjinga mmoja anafuta video zangu YouTube siwezi kumsamehe hata kidogo”.
.
Hili ni pigo kubwa sana kwa Nay haswa ukizingatia ndiyo mwaka unaanza na anakutana na janga kama hili. Kwa upande mwingine inasadikika kuwa hata akaunti yake ya Instagram imedukuliwa pia.
.
Usiache kutembelea website yako pendwa ya rickmediatz kwa habari za [HASHTAG]#Burudani[/HASHTAG] na [HASHTAG]#Michezo[/HASHTAG] kila siku siku.
.
[HASHTAG]#RickMedia[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TanzaniaLeadingEntertainment[/HASHTAG]&CelebrityNewsChamber.
ee37e6c22e4c2e448a979c4c143d8e53.jpg
 
Hawa jamaa (superstars wa bongo) inabidi watafute IT & security consultant. Awaelekeze namna ya kujilinda na awe nao bega kwa bega kugundua pale akaunti zao zinapokuwa matatani na namna ya kujilinda. Pia ahakikishe akaunti zao zote zina 2FA na recovery processes zinazoeleweka.

Fursa hii wakuu wenzangu tuliobobea kwenye haya masuala (stress on kubobea).

Sijui kama wataelewa umuhimu wa mtu wa aina hii lakini.
 
Niliposikia jina ney wa mitego fasta nikajua ni binti la haula kumbe ......abadilishe jina
 
Back
Top Bottom