Hongera sana kwa kuuliza swali la msingi ambalo wengi huwa hawazingatii hilo na matokeo yake ni maumivu yasiyo na huruma,, nitakusaidia kidogo kukupa baadhi ya njia za kibiblia ambazo zitakusaidia ili uweze kujua na kupata mtu sahihi wa maisha yako;
Jambo la Kwanza: Usifanye haraka, muombe na umwamini Mungu.
Hili ni jambo ambalo linawasumbua watu wengi sana hasa wasichana, wanaamini umri fulani ukifika ni lazima uolewe na huo umri ukipita basi hufai kuolewa NO.! ratiba ya maisha yako iko mikononi mwa Mungu yeye ndiye anaejua dhahiri ni wakati gani unafaa. Mhubiri 3:1 inasema "kwa kila jambo kuna wakati wake, na majira kwa kila jambo chini ya mbingu" Hivyo na wewe una wakati wako sahihi, usishindane na mtu. Ninao ushuhuda wa mama mmoja aliokoka mdogo sana lkn hakukurupuka kuolewa, alisubiri saa ya Bwana, ameolewa sasa ana miaka zaidi ya 30 na ni mrembo kupindukia, Mungu alimtunza kwa wakati sahihi.
Jambo la Pili : Zijue sababu na vigezo vya mtu unaemtaka.
Kwenye vigezo hapo sina tatizo naamini tayari utakua na vigezo vyako ambavyo ungetamani huyo mtu awe navyo labda muhimu kujua ni kwamba kuna vigezo vya kibinadamu (personal) na vigezo vya kibiblia (biblical) Ndio maana moja ya vitu ambavyo Mungu alikua akiwakataza sana waisraeli ni kuoa au kuolewa na yeyote, Mungu ana vigezo vyake pia.., Je! unafahamu ni sababu zipi zinakufanya uwe na mtu unaemtaka? achilia mbali watoto, kuna sababu zaidi ya hiyo, ngja nikupe mfano, Yusufu alimposa Mariamu na alipotaka kumwacha kwa siri baada ya kuona ana ujauzito wa Yesu, Malaika akamtokea kwenye ndoto na kumzuia, Yeye alijua ameposa binti wa kawaida kumbe amemposa mtu aliyepewa jukumu zito la kumzaa Yesu..,, hii iwe tahadhali kwako kwamba usije ukampata mtu leo halafu kesho ukamkimbia kwa sababu hukujua kwa nn huyo mtu amekuja kwako,,, hapo ndipo suala la subira na maombi linapochukua nafasi., ukishajua sababu itakua rahisi sana mtu akijitokeza kujua kwamba huyu ni sahihi au huyu siye.
Nilitamani kukueleza zaidi, lakini hayo machache naamini yanaweza kukusaidia.
Mungu akubariki.