Utoto sana,
Demu wangu wa kitambo tu tulitengana akiwa chuo,ghafla mi niko maskani home ushuani flani kula kulala.
Huyu hapa,kaja na bito kali na hapo hatujaonana miaka km mi5 hivi
Mi nikaitwa na Sister kuna mgeni wako.
Kutoka dooh ni yule X,
kumuuliza imekuaje umefika hapa
Kanivuta twende kwenye gari tukaongee.
Aloo kufika ndani mle demu katoa fuko la khaki lina zile noti za buku 10 za blue acha msimbazi mabunda kwa mabunda.
Duuh mtihani,basi ikawa twende hotel tukaongee.
Sikujivunga nikazama gheto kubadili kisha tukayeya.
Kule ndo demu kanipiga sound kwamba sasa yeye ni mfanyabiashara wa madini Tanzanite,na kamba nyingi sana.
Nakumbuka baada kumzagamua na kumbanganya haswa usiku tukaenda Out lang'ata kino,
ilikua kipindi Tupac& Big wameuana memorial concert,tukala bata la kutosha kule.
Home nikawa nimepotea mazima,
Hapo fuko lote la mbesa nimekabidhiwa.
Tunakaa Hotel
Yaani nilirudi maskani kukusanya pamba tu nikasepa.
Ndo kuanza Maisha Sasa Kitaa
Dah,kumbe demu bana kaja kutafuta Mimba,
Nakuja kushtuka imooo,hela nazo zinaisha.
Demu kawa mtu wa home tu ila hela akitoka anarudi nazo rundo.
Nikajiongeza nikaanza kupiga mzigo,
Maana nilijua tu hapa badae huyu atakua mzigo tu.
Kusema kweli tuliishi poa tu na yalitokea mengi ila ndo kijana wangu wa kwanza alizaliwa.
Leo hii ni mtu mzima kabisa and i feel proud of him.