Nawezaje kupata michango yangu yote NSSF? Kikwazo 33℅

Kwani mkuu ile hela wakati inakatwa hauukuambiwa kwamba utapewa uzeeni? Na infact sio yako tu, mwajiri pia alikuwekea ikusaidia uzeeni wewe ndo unataka upewe saivi
 
Kwani mkuu ile hela wakati inakatwa hauukuambiwa kwamba utapewa uzeeni? Na infact sio yako tu, mwajiri pia alikuwekea ikusaidia uzeeni wewe ndo unataka upewe saivi
Sasa ya mwajir ulitaka iwe mali ya mwajiri hii sheria imebadilika hapa mwaka jana tu kama ulikuwa ufahamu haya mafao yaligawanyika kuna watu wanafanya kaz na mikataba inaisha au anaachiashwa kazi sheria ya mwanzo ilikuwa inamruhusu huyu mnufaika kuchukua pesa yake yote cjui umeelewa hapo walivyoleta 33℅ wakatoa hicho kipengele ni vyema ungekuwa umeelewa kwanza mambo haya ndipo uje kuchangia hapa hata wewe ingekusaidia
 
Wakuu labda namimi niunge hapa mtanipa ushauri,
Mimi nilifanya kazi mahali fulan km professional ila baadae mkataba ukaisha nikaenda kufanya kazi sehem nyingine bila mkataba just kibarua sababu hata malipo ilikuwa ni cash tu sio bank.

Sasa imepita miaka miwili tangu niache kule pa mwanzo je naweza kupewa hela zangu zote nssf?
NSSF ili ulipwe inatakiwa uambatanishe barua yako ya kuisha kwa mkataba au kusitisha mkataba hapo ndio wanaanzia kuanza kufanya mchakato wa malipo kama umefukuzwa kazi ujue huna chako.
 
Huwezi kupata mpaka hiyo miezi 18,ungekuwa uliajiriwa kama UNSKILLED (KIBARUA)ungepata, lakini kwa kuwa ni graduate NSSF wanaamini utapata kazi nyingine na kuendelea kuchangia hivyo HAWAKUPI

Huu huwa ni ukiritimba tuu pesa zetu wenyew afu masharti kibao, mm huwa sielewi sababu ya kuliowa hela kwa mafungu wakati wao wanakata kwa lazima
 
Sasa mkuu utafukuzwa kazi bila mkataba kusitishwa?
Dah kweli dunia hii ina watu tofauti kufukuzwa kazi either umeshiriki mgomo kazini au umeiba hapo barua huwezi pewa ukipewa barua ya kusitisha mkataba inamaana umeondoka kwa amani otherwise huambulii kitu.
 
Before nilishafanya kaz kwenye campuni nyingne kama cashier tu na kuingia pale hakukutakiwa uwe na chet cha chuo nilipoacha hapo ndipo nikaingia huku sasa pesa zote ziliingia kwenye account moja
Ikitokea kazi uliyokuwa unafanya ni ya kitaaluma, hata ulie unagala gala chini hutapata pesa zako, zaidi ya 33% ya Mshahara wako kwa miezi 6.

Fao la kujitoa lipo maalum kwa wafanyakazi wasio wa kitaaluma, na walio achishwa kazi.

Sheria ndivyo zilizo, na haziwezi kubadilika leo au kesho.

Ni utafute namna ya ku-deal nazo wakati unataka pesa zako.
 
Hebu ngoja kidogo, kwahiyo nikiacha udaktari nikaenda kwenye ulinzi wanajumlisha makato ya nssf pamoja..?...😋😋😋
NSSF hawaangalii kazi uliyokuwa unafanya wakati unaachishwa:

Wanachoangalia ni:

- Kazi ni ya taaluma (skilled) au siyo TAALUMA( unskilled)

- Umeacha kazi mwenyewe au umeachishwa/kufukuzwa

- Una termination letter na letter of appreciation.

- Una barua ya kiapo kuwa ni kweli wakati huo huna kazi.

Muhimu wakati unafanya hiyo transition, hakikisha Account ya NSSF unayotumia ni hiyo hiyo.
 
NSSF ili ulipwe inatakiwa uambatanishe barua yako ya kuisha kwa mkataba au kusitisha mkataba hapo ndio wanaanzia kuanza kufanya mchakato wa malipo kama umefukuzwa kazi ujue huna chako.
Kufukuzwa na kuachishwa tofauti iko wap??lazima waajili wakupe termination later au barua ya kuisha kwa mkataba wako zote nssf wanapokea na unalipwa ondoa hofu ishu sasa kupata mpunga wote kama wewe graduate hapo ndio shida
 
Ikitokea kazi uliyokuwa unafanya ni ya kitaaluma, hata ulie unagala gala chini hutapata pesa zako, zaidi ya 33% ya Mshahara wako kwa miezi 6.

Fao la kujitoa lipo maalum kwa wafanyakazi wasio wa kitaaluma, na walio achishwa kazi.

Sheria ndivyo zilizo, na haziwezi kubadilika leo au kesho.

Ni utafute namna ya ku-deal nazo wakati unataka pesa zako.
Sasa hapo kwenye kufukuzwa kazi ndio pananihusu boss cwez pata yote??
 
NSSF hawaangalii kazi uliyokuwa unafanya wakati unaachishwa:

Wanachoangalia ni:

- Kazi ni ya taaluma (skilled) au siyo TAALUMA( unskilled)

- Umeacha kazi mwenyewe au umeachishwa/kufukuzwa

- Una termination letter na letter of appreciation.

- Una barua ya kiapo kuwa ni kweli wakati huo huna kazi.

Muhimu wakati unafanya hiyo transition, hakikisha Account ya NSSF unayotumia ni hiyo hiyo.
Hapo nimekupata mkuu wa kaz, sasa nisaidie kaz ya customer care hyo inaweza kuwa skilled maana hakuna bachelor hyo hapo imekaaje mkuu
 
Hapo nimekupata mkuu wa kaz, sasa nisaidie kaz ya customer care hyo inaweza kuwa skilled maana hakuna bachelor hyo hapo imekaaje mkuu
Kazi ambazo havipo vyuoni ndio kazi zisizo za kitaaluma.

Kazi ambazo hazitaki vyeti au vyeyi vya sekondari tu
 
Dah kweli dunia hii ina watu tofauti kufukuzwa kazi either umeshiriki mgomo kazini au umeiba hapo barua huwezi pewa ukipewa barua ya kusitisha mkataba inamaana umeondoka kwa amani otherwise huambulii kitu.
Sasa kama hupewi barua wanakuondoaje? Yani wanakuachisha kazi bila kutoa barua? We jamaa usijifanye unajua sana.

Wakati nipo mahali fulani kuna watu walifukuzwa kazi kwa kosa la wizi na barua walipewa.
 
Shukuru Mungu Pesa zako ziko huko NSSF they are very smart ukikamilisha taratibu zote unapata mshiko wako .mimi niko sekta binafsi pesa zangu ziliwekwa pspf Kabla mifuko haijaunganishwa Kuwa Psssf ya sasa hivi nilivyotaka kuzichukua wakaleta milolongo mirefu (japokuwa nilimaliza) lakini wafanyakazi wana mambo ya ajabu, wanajiskia mfuko wa Pssf una poor customer care.
 
Habari,

Naomba ushauri kwa anayefahamu namna gani naweza kupata pesa zangu zote NSSF ipo kiasi ni chini ya mill 5 na kazi nimeachishwa hivyo ukifuata utaratibu wa kawaida unaambiwa kuna kikokotoo unapewa 33℅ ya gross sallary yako ndan ya miez sita kisha unasubir miez 18 ndio upate yote.

Sasa nahitaji niongeze kwenye mtaji wa biashara hyo pesa yote nifanyaje ili niweze kupata pesa yangu yote,?elimu yangu bachelor.

Asanteni nipo hapa napitia comment zenu wanajopo

Hujaeleweshwa vizuri na hao NSSF.

Mimi nilikuwa nafanya kazi sehemi mkataba ukaisha nikasubiri muda ulivyofika nikajaza maombi ya kulipwa pesa yangu,nikaambiwa kwakuwa ni professional unalipwa asilimia 33 ya mshahara wako wa mwisho na fedha nyingine utapata baada ya miezi 18 kama hujapata kazi

Nikakubali,nililipwa asilimia 33 kwa muda wa miezi sita kama kawaida,baada ya miezi 18 kupita nikaenda kudai kilichobaki hapo ndipo nilishangaa,waliniambia kiasi kilichobaki siwezi kupata chote,nitapata kiasi fulani kwa formula hii.

Fedha nitakayopata= fedha iliyobaki baada ya kulipwa awamu ya kwanza-(minus) fedha jumala niliyochukua kwa muda wa miezi sita.

Mfano jumla ya michango yote= 4,000,000
Ukalipwa milioni 1,400,000 kwa muda wa miezi sita,itabaki 2,600,000.

Hivyo baada ya miezi 18 utalipwa.
2,600,000-1,400,000 (uliyochukua)= 1,200,000
Fedha utakayoipata ni 1,200,000/=
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom