Swenailie
JF-Expert Member
- Feb 15, 2016
- 240
- 230
Jaman ninaswali kuna mtu nampenda ananipenda kuna sababu zilifanya tusiwe wote. Ameoa nimeolewa nawatoto wawili anawatoto wawili. Ila ni mtu ananifaham nami namfaham kiundani zaidi ya wenzi wetu. Tulikuwa na uhusiano kabla ya kuwa na familia. Na uhusiano wetu haukuwa na mpango wakuwa na familia pamoja hilo tulilielewa mapema. Alipopata mwenza alinijulisha na tukaweka mikakati ya kutomkwaza mwenza wake. Alipoooa tuliendelea kuwa pamoja ila kwa mikakati ile ile. Nilipopata mwenza basi tukaweza kufanya vile vile. Na leo ninamiaka mitano katika ndoa na yeye anaiaka sita na nusu katika ndoa yake. Ni mwanaume anaenifaham anajua kipi napenda kipi sipendi wapi nimekwazika wapi sijakwazika hata mm pia. Kamuita mtoto wake jina langu. Nilishindwa kuamua jina la mwanangu maana madaraka yako kwa mume wangu ila nilitamani nimuite pia. Maisha yetu yameendelea. Kuna kipindi tulikwama ujenz alinisaidia sana. Kwakweli ni mtu wakaribu katika maisha yangu. Ila kila napofikiria huyu niliefunga nae ndoa najiona nafanya kosa kubwa. Ni ngumu yeye kujua kwani uhusiano wetu si wakujionesha hata kidgo siwez kaa bar wala sehem ya starehe nikiwa nae wala siwez kulala gesti. Ninapotaka kuonana nae naenda umbali na mazingira ninayoishi. Ambako hakuna uwezekano wa wenza wetu kujua. Ninaumia tu kwamba nitaacha lini kutoka nje ya ndoa yangu niliyoapa kanisan. Hebu nishaurini maana huyu nampenda ila si wangu halali