Natumai mu wazima kwa yeyote ambae ana tatizo nampa pole. Huwa nasikia watu wakizifia computer zao kwa kudownload haraka. Unakuta mtu kudownload file la 1GB haoni tatizo. Mambo ni tofauti kwangu kwa sababu laptop nayotumia ina speed ya kobe kiasi kwamba hata kudownload file la mb 10 unategesha labda unataka kuondoka au kulala ndo unaiacha ikidownload. Natumia simu (nokia) kama modem na mtandao wa voda. Pia natumia macbook pro ina operate mountain lion na browser yake ni Safari. Wapendwa wanaJF je, kuna uwezekano wa kufanya manouver ili kuongeza speed? Natanguliza shukuran na upendo ili busara amani na uvumilivu viwe pamoja nasi kuepusha lugha za matusi, kejeli, na dharau. Ahsanteni sana.