Kwanza nianze na kujiamini. Hivi ni kitu gani kinasababish m2 kutojiamini? Maranying napenda kukaa na watu wenye uwelewa wa kutosha kuhusu mambo, napia napenda kujifunza zaid. Lakini nakuwa sijiamini hususani pale wanapo anzisha topic: nakuwa muoga kuchangia kabisa na ingali kichwani huwa nina point zuri 2 ya kuchangia lkn nasita kuipresent, mara chache sana ninapojikuta nimeropoka, huwa wanakubali point yangu na kuisuppot kwa asilimia kubwa. huwa najiuliza nini hasa kinanisibu mpaka nakuwa muoga? hii hali huwa inanitokea mara kwa mara hata nikiwa na wazazi nyumbani. Tatizo hili linanisumbua xana na pia huwa napenda kujitenga pekeyangu kwa mda mrefu bila kuonana na marafk na hata sometym wanapojaribu kuonana na me huwaga nawa chukia pasi na sababu. Hii inapelekea baadhi ya watu wanasema me naringa. lakini me siringi huwa natumia silaa hiyo kuficha udhaifu wangu 2. Nisaidieni wakubwa, nawasikiliza nyie