Ni rahisi kuwaeliwa wanawake wanaoenda makanisa haya kwasababu wao wana hitilafu kidogo kwenye imani, ni rahisi kuvutwa na mazingira haya. Kwao haya makanisa ya miujiza, muziki mnene, ni kama sisi wanaume tunavyoangalia mpira zile kelele, shangwe, kutambiana na mpira ukiisha unasema “leo ilikuwa kali.”
Lakini mwanaume mzima, umepewa akili, macho yanaona vizuri, halafu unaenda haya makanisa ?
Unakaa dakika 10 tu tayari watu wanasukumwa wanaanguka kama majani ya mwembe. Wengine kila wiki wana mapepo yale yale. Najiuliza tu, bado hustuki tu ?
Halafu mchungaji anasema “mapepo yatoke!” mtu anaanguka. Lakini hujawahi kusikia “wagonjwa wote wa hospitali ya karibu wapone sasa hivi.” Hapo ndipo naanza kushuku hii ni trailer ya sinema fulani.
Katikati kanisa linageuka club ndogo. Muziki mnene, watu wanacheza kama sherehe ya kilabuni. Na wewe mwanaume umevaa suti yako nzuri unaanza kucheza bolingo kama uko kwenye TikTok challenge.
elimu yake ina mashaka au kwa uhakika alichonga O, sio ya ndevu ni ya form 4, confidence aliyonayo kwa kuona ana waumini wengi ataanza kuzungumzia vitu vya uchumi, geo politics, n.k. wale wasaidizi wake wanashangilia hata anapochanganya mafaili na wewe upo bize unatikisa kichwa, are u ok ?
Mchungaji meanwhile anaishi maisha ya kifahari, gari kali, suti kali, watoto shule kali. Wewe sadaka yako ndiyo nishati yake, lakini bado unapiga kelele “Mimi ni mshindi!” mpaka macho yanatoka kama umebanwa na mkanda wa suruali.
Halafu mwisho unaambiwa nunua maji ya upako na keki ya upako laki moja. Mimi hapo huwa najiuliza: imani yako imefikia level ambayo hata maji ya bomba hayakusaidii mpaka yawe na brand ya mchungaji?
Na sasa kuna ile nyingine ya ajabu zaidi. Unaambiwa “mkemee shetani kwa saa nzima!” watu wanapiga kelele “toka! toka! toka!” kama wanagombana na mbu chumbani. Wengine wanaambiwa watoke nje wachape ardhi kwa viboko wakimkemea shetani. Zimo kichwani kweli ?