Naweza kutumia Mkataba wa mauziano ya Serikali ya Mtaa kupata hati miliki ya kiwanja?

ububudu

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
266
414
Nilinunua kiwanja kutoka kwa mmiliki wa awali ila mikataba ya mauziano nilifanya na ndugu yake katika Serikali ya Mtaa. Hii ilikuwa ni baada ya kudhibitisha yeye mwenyewe kwa njia ya simu mbele ya uongozi kuwa atumiwe pesa kwa njia benki alafu mchakato wamauziano nimalizane na nduguye.

Hivyo nilimtumia pesa na kubaki na payslip ya benki then tukaandika mkataba na ndugu yake ikisimamiwa na uongozi wa mtaa na mashahidi nika attach na ile payslip.

Kwasasa nahitaji kutengeneza hati kwakuwa kiwanja kilipimwa na namba ilikuwepo hata kabla ya mimi kununua eneo hilo ingawa mmiliki wa awali hakuwahi kufanya maombi ya hati.

Swali langu kwenu wakuu je naweza kutumia ile document kuombea hati au Kuna vitu vya ziada nahitaji kuwa navyo?
 
To be on the safe side, mtafute mwenye mali/kiwanja muandike mkabata ambao atausaini mwenye. Hii ni muhimu! Kesho akikataa kuwa hakumpa mamlaka ndugu yake kuuza kiwanja chake utakuwa na utetezi upi unaokubalika KISHERIA? Idara y ardhi haiezi kukubali ktu kama hicho maana hawana uhakika kama kweli huyo aliruhusiwa kuuza kiwanja chake!

NB serikali za mitaa kisheria hawana mamlaka ya kusimami uuzaji wa ardhi. hao ni mashahidi kama mashahidiwowote ambao unaweza kuwatumia katika nununua ardhi. Hawana nguvu ya kisheria zaidi ya mtu wa kawaida!
 
Back
Top Bottom