Naweza kununua online kwa kadi yangu ya NMB?

Kakati

Senior Member
Apr 11, 2009
167
47
Nilijiunga na huduma fulani ya ku host website bure kwa hostinger.co.uk. Wakanipa. Sasa nafanya upgrading kupata huduma bora zaidi. Nikatakiwa kulipia pauni za UK kama 15. Nimejaribu kulipa kwa NMB, nikashindwa.

Kadi yangu ni mpya, ina alama ya Mastercard na ina chip. Pia niliwahi kutolea pesa kwenye ATM nikiwa ulaya kwa hiyo nilidhani inatambulika kununua online. Lakini nimeingiza particulars zake kununua online nimeshindwa.

Nikajaribu pia kuweka details zake kwenye paypal ili labda niweze kukatwa na paypal na kununua kwa paypay lakini haikubaliwa na paypal pia. Meseji imetoa inasema card not accepted, use another card!

Nishauri ninatakiwa niifanyeje kadi hii au kama haiwezekani basi nifanyeje kulipia shida yangu hii ya mara moja kwani sinunui vitu online mara kwa mara online.
 
Asante ikibidi nitaenda kwao.
Nimepiga simu NMB customer service wakanishauri niende na kadi yangu waweze kuiwezesha kufanya biashara online. Nikifanikiwa nitaweka habari hapa.
 
Kadi ya benki haiwez kununua vitu online bila ya kufanyiwa usajiri wa kufanya malipo online. Nenda ktk benk ya kadi husika, kuna fomu maalum utaijaza kuomba kuwezesha kadi yako kufanya malipo ya kimtandao (online), kisha utaambiwa usubiri kwa muda fulani. Ikiwa tayari utajuzwa.
 
Mdau ushamaliza kila kitu. Hata CRDB ni hivyo hivyo mkuu.
 
Kadi ya benki haiwez kununua vitu online bila ya kufanyiwa usajiri wa kufanya malipo online. Nenda ktk benk ya kadi husika, kuna fomu maalum utaijaza kuomba kuwezesha kadi yako kufanya malipo ya kimtandao (online), kisha utaambiwa usubiri kwa muda fulani. Ikiwa tayari utajuzwa.
Asante lakini nakumbuka kujaza fomu kwa ajili hiyo siku za nyuma, nitafanya hivyo tena kesho nione.
 
Mkuu ulijaza form kwa ajili ya kuiruhusu kadi kufanya online transaction au sim banking?? Kama ulifanya hivyo, je umewahi kufanya muamala wowote wa online? Kumbuka pia kadi huwa zinaexpire kwa hiyo ni lazima upate authorization upya kutoka bank.
 
Kadi yangu ni mpya, ina alama ya Mastercard na ina chip. Pia niliwahi kutolea pesa kwenye ATM nikiwa ulaya kwa hiyo nilidhani inatambulika kununua online. Lakini nimeingiza particulars zake kununua online nimeshindwa.

Hiyo yawezekana kweli! Na je uli toa tsh au usd $?
 
Mkuu ulijaza form kwa ajili ya kuiruhusu kadi kufanya online transaction au sim banking?? Kama ulifanya hivyo, je umewahi kufanya muamala wowote wa online? Kumbuka pia kadi huwa zinaexpire kwa hiyo ni lazima upate authorization upya kutoka bank.
Kadi ni mpya, na habari ya nmb mobile sio kwani ninatumia hiyo huduma miaka mingi sana. Sijawahi kufanya online transaction, na ndio maana ya kuomba ushauri na utaalamu humu. Nitajaribu kesho kwenda kwao. Nitawajuza
 
Hiyo yawezekana kweli! Na je uli toa tsh au usd $?
Mkuu hiyo ni jambo la kawaida kama una master au visacard. Mimi nilishawahi kutoa rand kwenye ATM za south Africa, nishafanya manunuzi kwa kutumia kadi kwenye shoping malls za south. Hela inayotoka ni ya nchi uliyopo kwa wakati huo, ila inafanya exchange rate na kuangalia balance kwenye akaunti yako kama linaruhusu kutoa kiasi unachotaka. Dunia kijiji.
 
Shukran! Nilikuwa sijui hilo.
 
Back
Top Bottom