NAWAZA KWA SAUTI KUBWA HUKU

NAWAZA KWA SAUTI KUBWA HUKU

retweeted

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
1,339
Reaction score
920
Ivi CHADEMA KWANINI BADO MNASIMMISHA WAGOMBEA KWENYE HIZI CHAGUZI NDOGO WAKATI MWASEMA NI UBADHIRIFU WA KODI ZETU.. GOMENI KUSIMAMISHA WAGOMBEA TUOKOE PESA KAMA KOROGWE VIJIJINI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uliza vzr uelewe ili uwaze kwa sauti kama simba,kwa sasa unawaza usichokijua.
 
kwenye chaguzi kuna faida inapatikana kwa pande zote
 
Mkuu wew ni me au ke? Kama ni me ashawahi kujiuliza kwanin jiwe kapiga 1.5 tr na bado kijani wanamshangilia na kusema ni kiboko ya mafisadi
 
Wakulaumiwa sio wapinzani ni chama Tawala chenye dhamana ya kusimia kodi zetu zilete maendeleo.
Wao ndio wanaowapa kichwa watu wazidi kubadilisha chama cha kuwapa watu ajira za udiwani na ubunge.

Suala sio wapinzani kusimamisha wagombea Bali ni kuacha mtindo wa kuwarubuni au kuwakubalia watu militia hasara taifa kwa maslahi yao binafsi.

Kinachofanyika cha watu kulitia hasara taifa ni ubinafsi.

Kila mtu anataka atukuzwe na kusifiwa binafsi badala ya taifa.
Leo hii wananchi maisha yao yapo chini sana lakini watu wanaona kuwa wakisema ukweli watachukiwa na watakosa ubunge na udiwani . Watu walichaguliwa wasemee Maslahi ya wananchi sio serikali wala chama.
Wapinzani wapo hivyo na Chama tawala kipo hivyo; wote wanatetea maslahi ya wenyeviti wao badala ya maslahi ya Taifa.
Kila mtu anaonekana pale tu atakapojitokeza na kumuunga mkono mwenyekiti wa chama Fulani.
Ukitaka upate maisha mazuri ndani ya chama au nje ya chama basi msifie mwenyekiti wa chama.

Wanaoharibu zaidi ni CCM na serikali yake kwenye hili suala LA militia hasara taifa kwa ajili ya chaguzi zisizo na rija.
Mwita Kwa mfano alikua anawawakilisha wananchi wa Ukonga bungeni na hiyo ndiyo kazi ya mbunge. Ana fungu lake la maendeleo ya jimbo. Kasi yake sio kupeleka hospitali Jimboni wala kupeleka madakrari wala kujenga Barbara ,wala kuajiri ,hizo ni kazi za serikali inayochukua kodi za wananchi bila kujali vyama vya. Cha ajabu mtu aliyekua na kazi hiyo ya kuwakilisha wananchi anaacha Leo kazi hiyo ya kuwakilisha wananchi aliyoipata kwa gharama kubwa halafu kesho tena anarudi kuomba kazi hiyo hiyo kwa sababu tu ya Chama kilichojawa na woga wa kushindwa. Kiburi na utani unawajaa hao wanaohama kwa sababu ta kutumia nguvu kuwarudisha kwenye nafasi walizolitia hasara taifa Mara mbili. Hii sio sawa.

Tungekuwa wazalendo wa kweli kwa Taifa hili na tungekua tunamchukia mtu yeyote anayelisababishia hasara Taifa letu ambalo linapata pesa kwa kuwaumiza wananchi kwa kodi nyingi hakika tungemwadhibu huyo mtu kwa kumweka benchi hata mwaka mmoja aone ugumu wa maisha ili akumbuke kuwa halipwi kwa pesa za mifukoni mwa wenyeviti wa chama Bali kwa kodi za wananchi ambao mara nyingine maisha yao ni duni kuliko ya hao wanaocheza na nafasi walizopewa za ubunge.

Hivi unafikiri kama wakurugenzi na wale wanaopewa dhamana ya kusimamia haki wakati wa uchaguzi wangekua wachamungu wa kweli na wazalendo wa kweli nani angelisababishia taifa letu hasara za kuacha ubunge halafu kesho anautaka ?

Ukiona uhalifu Fulani unaongezeka basi ujue kuna udhaifu kwa wasimamizi wa sheria. Huu uhalifu na ufisadi wa kufuja fedha za umma kwa wabunge wenye uroho wa madaraka na ubinafsi unaendelea kwa sababu kuna wasimamizi wa sheria za uchaguzi walioshindwa kazi ya kusimamia haki.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom