Nawaunga mkono Walimu wa Tanzania kwenye mgomo wao

"Matokeo yake yalikuwa mabaya kiasi kwamba hawezi kupata hata kujiunga na chuo cha Ualimu" Tafakari na uchukue hatua
 
Ni kweli swala kuu sasa ni jinsi gani ya kutoa elimu bora na si bora elimu! Juhudi za serikali zielekezwe huko, moja ya maoni yangu ni kuangalia uwezekano wa kuwaajiri walimu waliostaafu ambao bado wana nguvu kufanya kazi kwa mikataba. Kusema kuwa watawala wetu wanaongea tu is not fair sababu naamini enrollment ya walimu imeongezeka sana na moja ya vivutio walivyotoa serikali ni pamoja na kuwa wale walimu walioorodheshwa vyuoni watalipiwa tuition fees zao kwa jumla na si kukopeshwa kama wanafunzi wengine. Ingefaa hili lifanywe pia kwa madakatari na wahudumu wa afya kuongeza idadi yao, pamoja na hilo nakubaliana na wewe kuwa ni muhimu vilevile kuongeza uwezo kwa wale ambao wako kazini kwa sasa kwenda kwenye kozi na mafunzo mengine.

Hata walimu waliyomaliza mwaka huu wamepewa mkopo na wala si kulipiwa na serikali tena kwa kunyanyasika sana. Hivyo hakuna juhudi yoyote ya kuwasaidia walimu ili kuboresha elimu. Kumbuka hata walimu waliomaliza wamekaa zaidi ya mwaka hakuna ajira, tuache siasa katika hili.
Kuna walimu waliyojiendeleza na kufikia ngazi ya Shahada au uzamili akirudi mshahara wake unabaki uleule kama si kupunguzwa anapopelekwa sekondari kutoka E na kuanza na D kama alikuwa na E elimu ya Msingi. Hii serikali imeshindwa kuwajali wataalam na kufanya kila mtu afikirie kuwa mwanasiasa.
 
Ni kweli swala kuu sasa ni jinsi gani ya kutoa elimu bora na si bora elimu! Juhudi za serikali zielekezwe huko, moja ya maoni yangu ni kuangalia uwezekano wa kuwaajiri walimu waliostaafu ambao bado wana nguvu kufanya kazi kwa mikataba. Kusema kuwa watawala wetu wanaongea tu is not fair sababu naamini enrollment ya walimu imeongezeka sana na moja ya vivutio walivyotoa serikali ni pamoja na kuwa wale walimu walioorodheshwa vyuoni watalipiwa tuition fees zao kwa jumla na si kukopeshwa kama wanafunzi wengine. Ingefaa hili lifanywe pia kwa madakatari na wahudumu wa afya kuongeza idadi yao, pamoja na hilo nakubaliana na wewe kuwa ni muhimu vilevile kuongeza uwezo kwa wale ambao wako kazini kwa sasa kwenda kwenye kozi na mafunzo mengine.

Cha msingi mi nasema kugoma sio solution in the long run, sababu kama serikali ikiwakubalia walimu na madokta leo, kesho medereva, mesenja na wengine wakigoma itakuwaje? kwa sababu cha msingi hawa wanadai mishahara bora na tunajua kuwa uwezo wa serikali kulipa kila mtu kipato kizuri haupo. Hivyo narudia tena solution ni kuweka chombo huru kusimamia mishahara na posho za watumishi wote wa umma, hiyo itaondoa jukumu la kupanga mishahara toka serikalini na kukipa hicho chombo hilo jukumu na kuwa fair kwenye kupanga hiyo mishahara kwa kuangalia uwezo halisi wa serikali na mapato yake.


Suala hapa sio enrollment wala nini! Sisi walimu tunataka usawa katika viwango vya mishahara ukiangalia katika ngazi za cheti,stashahada, shahada na uzamivu za ualimu viwango vyao vya mshahara viko chini ukilinganisha na sekta nyingine za kilimo, afya, na Sheria kwa nini? Huko mishahara mizuri!

Au sisi sio watumishi au kazi yetu ni rahisi kuliko zingine? Tunachotaka ni KIWANGO CHA mshahara kipande at least basi TUWE Sawa na watumishi wengine wa serikali.

Dai letu lingine ni madeni Sugu ya walimu kwa nini serikali siku zote ikope walimu? Hata walimu WALIOJARIWA MWEZI wa pili tayari wana hizo mnaziita arrears madeni hayo ni pamoja na hela za likizo, nauli, mishahahara, pesa za kujikimu, uhamisho, KUPANDISHWA Madaraja madeni yetu ni karibia bilioni 11, hizo pia tunataka kulipwa mengine ikiwa ni pamoja na kuboreshewa mazingira ya kazi, tupewe nyumba za kuishi..

Suala la makazi imekuwa ni tatizo hasa kwa Shule ambazo zipo mbali na makazi hadi kuna walimu wanalala madarasani na HICHI ni miongoni mwa vikwazo vinvyofanya walimu kukimbia ajira zao kama serikali haijengi hizo nyumba iwalipe walimu HOUSING ALLOWANCE haiwezekani mnanitoa kwetu nauli hamjanipa mmenikopa, naenda KUANZA maisha pesa ya kujikimu danadana ni deni Hilo ntadai baadae hamna nyumba nipange house allowance sina nitegemee mshahara huo mdogo hii ni HAKI!

Walimu walioko katika mazingira magumu walipwe posho, na pia na sisi TUWE na posho TEACHING ALLOWANCE kwa wale ambao wana vipindi vingi.na kuwepo na malipo ya overtime.

Vifaa vya kujifunz na kufundishia viboreshwe, kuwe na majengo, madawati, vitabu.. Sio Sa hivi tunachoshana......

TSD iboreshwe ikiwezekana ivunjwe kiundwe CHOMBO kipya matatizo ya Madaraja ya walimu, scale za mishahara zishughulikiwe.

KIWANGO CHA kiangaliwe UPYA YAANI 14% kodi,5% PENSHENI,8% NHIF,2% CWT kwa KIWANGO CHA mshahara wa 255000 alipe na pango, nauli.. Kweli hii ni haki?



YAANI THIS TIME. HATUKUBALI TUKIMALIZA TUNARUDI KUISAFISHA CWT.....TUNAIOMBA SERIKALI IFANYIE KAZI MADAI YETU WAKUMBUKE KUNA SENSA! OOHOO

 
Mwanakijiji kumbe huna maana siku hz au siyo wewe kuna mtu amejifanya ni wewe nashangaa sana natilia mashaka uadilifu nia na dhamira zako
 
Back
Top Bottom