Nawaunga mkono Walimu wa Tanzania kwenye mgomo wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawaunga mkono Walimu wa Tanzania kwenye mgomo wao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 28, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Kama kuna janga kubwa lenye matokeo dhahiri na ya moja kwa moja kwa uhai wa taifa ni janga lililoko kwenye elimu. Janga hili ninaamini linatokana na kushindwa kwa sera mbovu za chama tawala; sera ambazo zimegeuza elimu kuwa bidhaa adimu ambayo wale wanaotaka iliyo bora inawapasa walipe zaidi. Janga hili limefanya elimu itolewe kwa matabaka huku wenye uwezo wa kimudu elimu nzuri na bora kwenye mazingira mazuri wakati maskini na wale wa kipato cha kati wakihangaika na elimu duni na mazingira duni ya elimu.

  Sera yetu ya elimu imejikita zaidi kwenye "wingi" kiasi kwamba taifa limekuwa na vitu "vingi" lakini visivyo na ubora wa kuweza kutolewa mfano. Tumeweza kuandikisha watoto "wengi" kwenye elimu ya msingi na sekondari huku tukijenga shule "nyingi" za viwango hivyo huku kwenye elimu ya juu vijana wetu "wengi" wakipata elimu hiyo kwenye vyuo "vingi" vya juu vilivyotapakaa nchi nzima. Katika sera hii ya "wingi" Tanzania inaweza kujivunia "high enrollment rate" au "high completion rate" kiasi kwamba wenyewe tukajipongeza kwa "kufanya vizuri" kwani sasa vipo "vingi" kulinganisha na tawala tatu zilizopita.

  Ubora wa elimu hauwezi kabisa kutenganishwa na maslahi ya walimu. Naweza kujenga hoja kuwa kuongeza wingi wa vitu bila kuboresha maslahi ya walimu ni janga lililokuwa linasubiri kutokea tu. Tunaliona hili kwenye sekta ya afya na pia kwenye elimu. Ndio maana maneno ya Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kuwa "Maendeleo ni ya watu siyo vitu" yana maana ya pekee. Kama watawala wetu wameweka mkazo katika kuendeleza "vitu" (shule nyingi, barabara za juu kwa juu, magorofa ya vioo, magari ya kila namna n.k n.k) na wakasahau kuwa kama vitu hivyo havimuinui mwanadamu basi matokeo yake watu huasi kwanza moyoni na pili kwa vitendo.

  Tunachoshuhudia sasa hivi kwenye hii migomo na migongano tunayoiona ni watu kutoridhika na "maendeleo ya vitu". Watu wanataka kuona maisha yao yanaboreshwa zaidi, watoto wao wanasoma vizuri, wanakula vizuri, mama na dada zao wanajifungulia katika mazingira bora zaidi na kuwa maisha yao yana "afueni" inayoonekana siyo inayosimuliwa.

  Ni kutokana na hili basi naunga mkono wa walimu kama nilivyounga ule wa madaktari nikiamini kuwa watawala wetu hawawezi tena kwenda bila kushinikizwa au kulazimishwa. Sababu ni kuwa wao wameinuka dhidi ya wananchi na kujifanya wako juu ya raia badala ya wao kuwa watumishi wa wananchi. Walichokifanya watawala ni sawa na mapinduzi ya kuwanyang'anya raia madaraka yao chini ya Ibara ya 18 ya Katiba na hivyo kuwafanya wananchi washindwe kutumia njia nyingine yoyote (hasa kama kwa kura imeshindikana) kuanza kulazimisha mabadiliko.

  Nikitambua hili natambua vile vile serikali ambayo inaanza kulazimishwa kwa migomo na maandamano haina namna ya kujibu isipokuwa kwa kutumia nguvu. Kwa vile serikali inaonekana haiwezi kuzungumza na kada mbalimbali bona fide ni wazi watu wa sekta mbalimbali wanajikuta wanalazimika kutumia nguvu pekee ambayo wanayo yaani "hiari" yao. Ni matumaini yangu serikali itakubali kurudi kwenye meza ya mazungumzo na kubadilisha mwelekeo wa sera yake ili kuboresha maslahi ya walimu na kushughulikia madai yao mbalimbali ili hatimaye watoto wetu wapate elimu iliyo bora kwenye mazingira bora na hatimaye kuachana na kutegemea misaada ya madawati na vyoo kutoka kwa makampuni mbalimbali katika jitihada za kuficha kushindwa kwa sera zao!

  MMM
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Serikali yetu imeiweka elimu yetu rehani. Tufanye transformation
   
 3. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono,lakini watagoma kweli??
  Walimu siku zote wamesaidia kuiingiza CCM madarakani kwa hofu yao.
  CCM siku zote huwapa vitisho na kuwatumia kama Makanda Kanzu wa CCM

  Tuna kazi kweli kweli
  Kazi ya kwanza ni kuiondoa CCM madarakani.
  Hili lisipofanyika tujue bado ni MISUKULE tu
  Kazi ya pili ni kurejesha utawala wa sheria
  Megine yote yamezuka kutokana na ukosefu wa utawala wa kisheria.
   
 4. W

  WaMzizima Senior Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sera ya uwingi kama unavyoielezea ni kweli ina upungufu wa ubora (quality) na changamoto nyingine kadhaa, lakini nafikiri hiyo ilikuwa ni juhudi ya makusudi nami pia naiunga mkono kwa sababu zifuatazo;

  Kabla ya shule za kata watu wetu wengi hasa vijijini walikuwa hawana uwezo wa kupeleka watoto wao sekondari na miaka si mingi iliyopita ilikuwa ni kawaida sana kwa shule kuwa na mtoto mmoja au wawili tu waliochaguliwa kwenda sekondari. Hali sasa imebadilika ni kinyume shule nyingi watoto karibu wote wanachaguliwa na wawili au watatu ndio wanaoachwa.

  Matokeo ya hilo na impact yake kwa society yetu ni kubwa. Kwanza hawa watoto wengi hupata lishe shuleni, hii kwa kaya maskini ni afueni kubwa. Pili ingawa mimba zimeongezeka mashuleni, lakini kwa ujumla idadi ya mimba kwa wasichana kwenye jamii imepungua sana kulinganisha na kabla. Tatu wale wazazi wenye afueni kidogo badala ya kulipa malaki kadhaa kuwapeleka watoto wao shule binafsi ambazo nazo nyingi zina changamoto zilezile kama shule za kata wamepata unafuu na kuweza kutumia hizo hela kwa shughuli nyingine za maendeleo.

  Hivyo kwa mawazo na uzoefu wangu bado shule za kata ni bora sana kulinganisha na mwanzo ambapo kulikuwa hakuna shule kabisa. Na kwenye afya ni hivyo hivyo hizi kliniki za vijiji ingawa hazina dawa za kutosha wala watendaji wenye ujuzi wa juu bado ni bora kuliko mwanzo ambapo kulikuwa hakuna na zimesaidia kuokoa maisha ya watoto na wakina mama wengi.

  Cha msingi ni kuanza kuboresha hizi huduma, hivi sasa kuna shule za sekondari na kliniki karibu kata zote Tanzania na kwa hilo JK kafanya kazi nzuri. Changamoto zipo katika kuboresha hizi huduma kuwapa elimu walimu na wahudumu wa afya kitu ambacho serikali inafanya kwa juhudi, kuongeza maabara na vitendea kazi kwa ujumla wote tunajua jinsi ya kuboresha hizi huduma. Ila ni muhimu tukubali kuwa kazi kuu ya kujenga na kuweka mazingira ya mwanzo imeshafanyika na ni jukumu letu wote kuchangia maendeleo yake. Tukishirikiana na kufanya harambee tutaweza mfano badala ya kutumia mamilioni ambayo tunatumia kwenye vikao na maharusi tukiweza kutumia kiasi kama hicho kuchangia shule na zahanati basi nchi yetu itapiga hatua kubwa.

  Migomo ya madaktari na walimu ingeweza kuepukika kabisa iwapo serikali ingeweka chombo huru cha kupanga mishahara ya watumishi wote wa umma kuanzia rais, mawaziri, wabunge, walimu, madakatari, wahudumu, mashirika ya umma na wote ambao kipato chao kinategemea hela zetu za walipa kodi. Hiyo ndio itakuwa suluhisho ama sivyo kwa mpango wa sasa kila mtu atagoma leo madaktari na walimu kesho madereva na kuendelea kila mtu ataona anaonewa na mshahara hautoshi. kama unakumbuka wakati wa Mwalimu kulikuwa na SCOPO nafikiri ilikuwa inaitwa, na kazi yake ilikuwa kupanga mishahara ya watumishi wa umma. Lakini nafikiri Mkapa aliivunja na matokeo ndio haya ya sasa, kuna upendeleo wabunge, TRA, na wengine wanauwezo wa kujipangia mishahara ilhali wengine kama madaktari, walimu, madereva hawana huo uwezo zaidi ya kugoma hawana namna.

  Mi ushauri wangu ndio huo, tuwe na chombo huru cha kupanga mishahara ya watumishi wote wa umma kwa kulingana na uwezo wa serikali yetu na kitumie haki (fairness) na ukweli (realistic), tuwe fair kwenye kugawana national cake. Bila hivyo migomo haitaisha hata Yesu aje!
   
 5. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,901
  Trophy Points: 280
  Unajua mtu ukifikir vizuri sna utagundua kuwa wanaopata elimu nzuri hapa Tanzania siyo mtoto a mkulima aliyeko kijijinina sababu kubwa iko katika kile ninachokiita utumwa wa kifikra ambao pia hauwez kuleta uhuru wa kimaendeleo. sioni haya kuyasema haya kwani mawazo ya kushikiwa ni mabaya sana kwa mtu yeyote yule na hasa anapokuwa ni mtawala. Huwez jua yule anyekusemezesha juu ya haya mawazo anafikiria uhuru gani wa kimaendeleo juu ya mawazo anayokufikirisha.

  Jiulize mpango wa maendeleo wa MMEM na MMES ulikuwa na nia gani hasa, na aliyeibuni aliubuni chini ya influence gani.Nachelea kusema kuwa kwa kua mipango yote hii ilifanywa na donor funds na seriali ilikuwa imepigika sana kiuchumi to them waliona ni afadhali waikubali ili wapate fedha but wakasahau kwamba fedha hizo hizo zitawahukumu manake watajenga shule nyingi sana sawa lakni nguvu kazi ni finyu sana, what next????? ..............wakaona tueke waalim wa voda fasta...............matokeo yake ndio haya tunayoyaona ambayo siku hizi ufaulu umeshuka na hata uelewa wawanafunzi no matter kwamba alifaulu ni mdogo sana na hii output utaiona hata kwa atakapo maliza chuo.

  haikuishia hapo waalim waliokuwwepo ambao ni commpetent hakuna aliyewajali na hii ni kutokana na ukweli kwamba mpango wa hii ya elimu haikujua wala kuwaza juu ya maslah ya mwalim huyu. unaongeza enrollment waalim ni wachache, maslah ni madogo what do you expect next? tunategemea deliveries below standard na ndio haya wanafunzi hadi anamaliza la saba can't read and write, form four student can't comprehend even a single paragraph.

  hayaishii hapo yanapelekea kuwa na wanafunzi ambao hata kama watajoin higher education but hawatakuwa competent kwenye labour market kwani hata huko juu bado ni usanii tu. Sasa ukiwaza yepi yalikuwa ni mawazo ya hao donors mimi nayaona kama vile lets allure them by giving money and definitely whatever we propose to be the allocations lets stick into it. wabongo tupokeapo pamoja na masharti hayo bila kufikiria vizur we accept the money and zimekuwa allocated kwa ajili ya ujenzi tu wa majengo sasa hivi waweza kusema mpango wa maendeleo wa elimu halafu uurestrict kwenye majenzi tu? ama maendeleo hayo ni kuwa na majenzi tu? vipi kuhusu quality ya wanafunzi wanaotoka kama products, vipi kuhusu waalim wanaowafundsha and so on.

  Kumbe watoa fedha wameshaona kuwa tuwapunguzie idadi ya professionals kwa kutoa elim mbovu and in a long run tutarudi tena sisi wenyewe kuwatawala na ndicho ambacho sasa tukitegemee. kwani dalili zipo zimeshaanza kuonekana.

  Waalim kukaa kimya na kuendelea kuvumilia haya mishahara midogo, teaching allowances hakuna, mazingira mabaya ya kufanyia kazi matokeo yake nikuendeleza kudidimiza elimu hii kwa kiasi kikubwa pia ni kutokutendewa haki yake ya msingi. hawana haki ya kunyanyasika katika nchi yao. na kweli mimi nikiwa mmoja wapo wa waaalimu nitagoma na hapa ni hadi kieleweke.
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji taarifa niliyo nayo walimu wengi wanavyeti vya kufoji kwahiyo mkwara kidogo tuu wanafyata Mkia
   
 7. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,901
  Trophy Points: 280
  ndugu yangu WaMzizima umesema vyema sana kwamba nia ya mipango hii ya elimu ni delaying of early motherhood but not giving them the quality education. kwa upande kwa kumpunguzia mwanafunzi muda wa kuwa mama katika umri mdogo lmefanikiwa kwa asilimia kubwa.

  Swala la kuiboresha elimu hii kwamba ameshakuwa darasani sasa apate elimu yenye tija nalo nilakuangaliwa sasa. Ila tukumbuke kwamba maboresho haya hayaji kwa kuongea tu na watawala wetu we need to go further aisee, mara ngapi tunaongea na bado hayaangaliwi? ni afadhali tugome ili kuishinikiza na kweli hapa wanaotuangusha ni waalimu wa vyeti tu ila wengine wote tunania sana tumesha sema na hii serikali waziri mkuu mwenyewe keshaommngea na sisi maa kibao lakin hakuna matokeo sasa tufanyeje?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,901
  Trophy Points: 280
  swla la vyeti hapa halina mashiko manake siyo wengi ukilingansha na na waalim wengne. Hii ishu ya vyeti feki iko pronounced sana katika kada ya elimu kwasababu tu elimu ni sekta yenye watumisha wengi sana so anything to them lazima kigain publicity kubwa lakni sitaki kuamini kwamba ndiyo field pekee yenye vihiyo, hata kidogo. Mbona huko polisi iko hivyo, jeshi na kila mahali?

  hoja hii isitumike kama loophole na if real you are taking it as loophole basi hilo kwetu siyo shida tuko tayari tugome wale wa shahada na shahada za uzamili. basi. Hivi unajua mwl mwenye elimu ya uzamili leo hii anaajiriwa kwa mshahara wa sh ngap? FYI huyu kwenye salary scheme hana category ukienda mwajiri nafanya kukwambie lets think btn tgts E and F na hapo unashangaa hivi hawa tsd wanafanyaga nini? inamaana mwalim at mastre's degree level haimtambui? mbona huko kwenye field zingine tu tena serikalini wana category na mishahara mikubwa? acheni bana mimi salary ninayopokea kwa kiwango changu cha elimu ni kama degree holder wa kilimo na mifungo for god's sake huu ni unyanyasaji.
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  mkuu hujanielewa nazungumzia wale wa msingi
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,901
  Trophy Points: 280
  lakini nani mwenye kosa mwajiri ama mwajiriwa? manake kama ni cheti feki basi aliyeajiri ndiye mkosa wala si aliyeajiriwa.
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Nani alikudanganya kuwa walimu wengi wa shule za msingi wamefoji vyeti? Acheni kuwadharau walimu wajameni, ndio waliowafikisha hapo mlipo.
   
 12. W

  WaMzizima Senior Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli swala kuu sasa ni jinsi gani ya kutoa elimu bora na si bora elimu! Juhudi za serikali zielekezwe huko, moja ya maoni yangu ni kuangalia uwezekano wa kuwaajiri walimu waliostaafu ambao bado wana nguvu kufanya kazi kwa mikataba.

  Kusema kuwa watawala wetu wanaongea tu is not fair sababu naamini enrollment ya walimu imeongezeka sana na moja ya vivutio walivyotoa serikali ni pamoja na kuwa wale walimu walioorodheshwa vyuoni watalipiwa tuition fees zao kwa jumla na si kukopeshwa kama wanafunzi wengine.

  Ingefaa hili lifanywe pia kwa madakatari na wahudumu wa afya kuongeza idadi yao, pamoja na hilo nakubaliana na wewe kuwa ni muhimu vilevile kuongeza uwezo kwa wale ambao wako kazini kwa sasa kwenda kwenye kozi na mafunzo mengine.

  Cha msingi mi nasema kugoma sio solution in the long run, sababu kama serikali ikiwakubalia walimu na madokta leo, kesho medereva, mesenja na wengine wakigoma itakuwaje? kwa sababu cha msingi hawa wanadai mishahara bora na tunajua kuwa uwezo wa serikali kulipa kila mtu kipato kizuri haupo.

  Hivyo narudia tena solution ni kuweka chombo huru kusimamia mishahara na posho za watumishi wote wa umma, hiyo itaondoa jukumu la kupanga mishahara toka serikalini na kukipa hicho chombo hilo jukumu na kuwa fair kwenye kupanga hiyo mishahara kwa kuangalia uwezo halisi wa serikali na mapato yake.
   
 13. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mwalimu na aliyosema mwanakijiji ni ukweli ulio wazi. Nawaambia vijana kwa sasa watakaowapa elimu bora ni walimu wazalendo tu ambao ktk shule hakuna kabisa ama mmoja. Lazima tugome na uongozi wa cwt ubanduliwe waoga wale.. Ukombozi wa haki unakuja.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kusema kweli sitarajii maana hawa wangeweza kuwa chachu ya mabadiliko tangu zamani sana lakini tangu watengenezewe programu za ualimu wa voda ikawa ndio dilution kabisa!
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja, japo niliikimbia chaki kwa udhaifu wa serikali
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Tatizo wanaanza kugoma pindi shule nyingi zimefungwa
   
 17. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 1,746
  Trophy Points: 280
  Honestly nilikua kwenye kundi hili..lakini ilibidi nikimbie nibadilishe upepo, ni maamuzi magumu lakini nashukuru angalau sipati tena stress kama mwanzo.
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  MMM.
  Umeongea vyema katika bandiko lako kuna baadhi ya vitu ulivyoandika nakubalia na wewe kwa sehemu kubwa, kwenye suala la kuwaunga mkono Walimu kwenye mgomo wao sijui unawaunga mkono kwa mtindo gani! migomo mingi inayofanikiwa ni raia wengi kuwa nyuma ya huo mgomo kuisukuma serikali kuwalipa madai yao, kuwaunga mkono Walimu kwa kuandika unadhani ndio njia sahihi ya kuwasaidia au kuna njia nyingine.
   
 19. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Nilichakachua hukooooo
  Kwa hasiraaa nyingiii......

  From Dip. Teacher to Financial Economist........

  Tanzania, masomo ya Ualimu hayamtengenezi mtu akawa na akili za maisha

  T.I.T (This Is Tanzania)
   
 20. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Sina uhakika walimu kama watagoma kweli. Hawana confidence enough, wana mashaka na maslahi yao individually. Sijui ni kwa vile elimu yao ni ndogo. Nawakumbuka hata wale wa vyuo kikuu last time walivyokosa mshikamano wakamwacha kiongozi wao peke yake, ni waoga sana na hawana mshikamano.
   
Loading...