Nawauliza wana JF

Nawauliza wana JF

mankachara

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2013
Posts
6,161
Reaction score
3,496
Leo nimepokea SMS hii kwenye simu yangu

"+12062596616:
COCA COLA AWARD YOUR NO HAS WON 250,000 DOLLARS TO CLAIM SEND YOUR NAME ADRES WORK AGE TO DR.LOISE ON EMAIL ONLY:cocacola.us12345@outlook.com"

Je! Hivi hii ni kweli au kuna watu wajanja tu
 
Kama hela zingekuwa zinakuja kirahisi hivi dunia ingekuwa ni mahali pazuri sana pa kuishi..
 
Ukitaka jibu unilipe kwanza la sivyo utajibeba. Hiyo pesa unajua ni tzs ngapi?
 
maisha siyo rahisi namna hiyo mkuu!!
 
Nobel prize award, grammy awards, oscar award, kili award (mifano tu) huwa wanapewa watu kwa achievements flani. SWALI: we ume-achieve nini hadi upewe hiyo award. Alafu search google kama kuna award kama hiyo duniani.
 
Hao ni wezi wa kwenye mtandao, baadaye watakutaka uwatajie account yako ya benk wakutumie hizo pesa na ndiyo utakuwa umeliwa hivyo, halafu hii ilikuwa kwenye email tu ila siku hizi wanakuja mpaka kwenye simu?
 
Sina hata huduma yoyote niliyojiunga Mimi mwenyewe nashangaa baada ya kupokea hii sms
 
Hao ni wezi wa kwenye mtandao, baadaye watakutaka uwatajie account yako ya benk wakutumie hizo pesa na ndiyo utakuwa umeliwa hivyo, halafu hii ilikuwa kwenye email tu ila siku hizi wanakuja mpaka kwenye simu?

Asante sana nimekuelewa
 
Kama hujui maana ya msamiati "utapeli" basi jaribu kufuatisha hayo maelekezo uliyopewa...
 
Next utaambiwa uwatumie pound kadhaa ili waweze transfer kwa account yako then urafiki utaishia hapo. Watu walikopa ili watume ili watumiwe hayo ma lottery wanalia hadi kesho. Acha ndoto za mchana
 
Pole,ni matapeli,my mom ashatumiwa msg frm nokia company eti kazawadiwa $ laki 3 out of nowhere na ye anatumia samsung..
 
Je ulicheza hilo shindano?

Nakushauri kimbia mbio nyingi sana, usigeuke nyuma
 
Leo nimepokea SMS hii kwenye simu yangu

"+12062596616:
COCA COLA AWARD YOUR NO HAS WON 250,000 DOLLARS TO CLAIM SEND YOUR NAME ADRES WORK AGE TO DR.LOISE ON EMAIL ONLY:cocacola.us12345@outlook.com"

Je! Hivi hii ni kweli au kuna watu wajanja tu
Wewe utaliwa hao ni wezi kama wale wa Facebook na ukishakubaliana nao watakuomba account no yako halafu wanakomba kila kilichopo. Chukua tahadhari.
 
Back
Top Bottom