Nawatafuta ndugu zangu upande wa Mama

Nawatafuta ndugu zangu upande wa Mama

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Posts
1,637
Reaction score
463
Habari zenu wanaJF!

Natafuta ndugu zangu upande wa mama yangu: Jina lake ni Pendo/Khadija Rubeni mzaliwa wa Tabora (Igunga?) kwenye ukoo wa mzee Rubeni. Baadae alihamia Mwanza na kunizaa mimi baada ya kukutana na mwanaume (Baba) kwa jina: Ali Saidi (majina yake ya utani yalikuwa ni: King Solomoni Ali au Ali Manyege). Alikuwa maarufu sana Mwanza, alifariki mwaka 2015 kama sikosei.

Nawafahamu ndugu upande wa Baba lakini sikubahatika kujuana na ndugu upande wa mama baada ya kwenda nje kimasomo na kurudi nikiwa nimeshakuwa, na kwasasa ninaendesha maisha yangu hapa Dar es Salaam.

Msaada tafadhali.
 
Sorry, huyu Ali manyege ni marehemu? Au yupo....nnamfahamu mie nilisikia alifariki alikua maarufu sana mwanza
 
pole sana mkuu...MUNGU ataonyesha njia belive.
Vp mama yupo au?
 
Hata kama ni jina la utani lakini dah lina ukakasi! ALI MANYEGE!!!!!!!

Ingia pia facebook ni rahisi sana kupata majina yao...
 
Ndugu wa upande wa mama unawatafuta wa nini kama unawafahamu ndugu wa upande wa baba achana na hao wengine maana ule ndo ukoo wako.
 
Sorry, huyu Ali manyege ni marehemu? Au yupo....nnamfahamu mie nilisikia alifariki alikua maarufu sana mwanza

Ndio, ni marehemu. Ni kweli alikuwa maarufu sana Mwanza, alikuwa dreva tax. Una data zozote? Mie ni mtoto wake wa kwanza.
 
Ndugu wa upande wa mama unawatafuta wa nini kama unawafahamu ndugu wa upande wa baba achana na hao wengine maana ule ndo ukoo wako.

Asante kwa maoni lakini sina mtazamo huo, napenda kuwafahamu ndugu wa pande zote. Asante.
 
Huyo mzee wako ni hatari, inawezekana Yule Morris wa Kenya ni ndugu yako...(Morris nimechoka, Morris I surrender)
 
Ndio, ni marehemu. Ni kweli alikuwa maarufu sana Mwanza, alikuwa dreva tax. Una data zozote? Mie ni mtoto wake wa kwanza.

Aisee pole sana, mmh hapana kwakweli sina data zozote ila kwa mwanza ukiulizia tu kuhusu ally lazma upate taarifa zake, kwanini hao ndugu wa baba wasikupe taarifa za upande wa mama?
 
Habari zenu wanaJF!

Natafuta ndugu zangu upande wa mama yangu: Jina lake ni Pendo/Khadija Rubeni mzaliwa wa Tabora (Igunga?) kwenye ukoo wa mzee Rubeni. Baadae alihamia Mwanza na kunizaa mimi baada ya kukutana na mwanaume (Baba) kwa jina: Ali Saidi (majina yake ya utani yalikuwa ni: King Solomoni Ali au Ali Manyege). Alikuwa maarufu sana Mwanza, alifariki mwaka 2015 kama sikosei.

Nawafahamu ndugu upande wa Baba lakini sikubahatika kujuana na ndugu upande wa mama baada ya kwenda nje kimasomo na kurudi nikiwa nimeshakuwa, na kwasasa ninaendesha maisha yangu hapa Dar es Salaam.

Msaada tafadhali.

Mkuu nenda ukatangaze redioni naamini itakurahisishia zaidi kuwafahamu,hasa Kiss FM au hata Star TV.
 
Yaah kujua ndugu wa pande zote si jambo baya kila la kheri ndug.
 
Hakika huyu ni Ali Manyege siyo mchezo.

We muuza Copy za Cd hata waazazi wako wa asili unawatambua?
Kazi kukashifu tu. We una habari mzazi wako wa Kiume aliyekulea sio babako?
Seme"Suu" nikuwekee picha ya babako mzazi hapa.
Utahama mji. Tumbaaaff
 
Mbona hujasema mama yako yuko wap? Au sijakuelewa??
 
Hakika huyu ni Ali Manyege siyo mchezo.

Haya majina yapo.Kuna mtoto wa shemeji yangu alinunua jina la mtu kusomea anaitwa manyege magunila.Huwa nacheka hilo jina nimeshangaa kuona na hapa.
 
Back
Top Bottom