Wonderful
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 7,347
- 6,001
Mkuu Igunga ni kubwa sana, inaanzia maeneo ya shelui mpaka sijui Ziba kwa barabara ya Singida Nzega. Labda ungejua kabila la mamako ingekua poa zaidi either ni mnyiramba, nyaturu, au msukuma au mnyamwezi. Nina mdogo wangu yuko pale igunga anaweza kutoa msaada, anaishi kijiji kimoja wanalima sana mpunga (Mwanzugi) na pia ana nyumba yake mjini igunga.Habari zenu wanaJF!
Natafuta ndugu zangu upande wa mama yangu: Jina lake ni Pendo/Khadija Rubeni mzaliwa wa Tabora (Igunga?) kwenye ukoo wa mzee Rubeni. Baadae alihamia Mwanza na kunizaa mimi baada ya kukutana na mwanaume (Baba) kwa jina: Ali Saidi (majina yake ya utani yalikuwa ni: King Solomoni Ali au Ali Manyege). Alikuwa maarufu sana Mwanza, alifariki mwaka 2015 kama sikosei.
Nawafahamu ndugu upande wa Baba lakini sikubahatika kujuana na ndugu upande wa mama baada ya kwenda nje kimasomo na kurudi nikiwa nimeshakuwa, na kwasasa ninaendesha maisha yangu hapa Dar es Salaam.
Msaada tafadhali.