Nawashukuru wote mlionipigia Kura hapa Jf Mungu awabariki nyote, Nje ya CCM na Chadema sisi ni Wamoja tunaoishi pamoja hapa Jukwaani!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Nasema ahsante sana kwa wale walionipigia kura Katika Jukwaa hili la Siasa.

Kiukweli nimeshika namba 3 na napenda kumpongeza Kamanda Ethryocyte aliyeshika namba 1 na Kada mwenzangu wa Kawe Pascal Mayalla aliyeshika namba 2, Kadhalika namtia moyo sana Malcom aliyeshika namba 4.

Mungu wa mbinguni awabariki WanaJf wote kwa namna tulivyoisaidia nchi kupitia Jukwaa hili.

Ikumbukwe bila vionjo fulani fulani kama vya akina Genta na Mrangi Jukwaa linakuwa dumavu cha muhimu tusiruhusu kutukanana.

Kuna maisha Nje ya Siasa na ni muhimu kujipima michango Yako ni kwa ajili ya kusaidia Taifa au kujipendekeza kwa Watu fulani ambao Wengi wao hata hawakujui kama unaishi hapa Duniani.

2022 namuona Freeman Mbowe kama mwanasiasa Bora kwa sababu baada ya Kutoka Gerezani ameendelea kuwapigania Wanachama wa Chadema walioko Jela kwa kubambikiwa kesi na Wengi wameanza kuachiwa. Nakukumbusha Freeman pale Gereza la Njombe kuna George Sanga wa Chadema.

Nawatakia Heri ya Mwaka Mpya!

RIP Pope Benedict XVI
 
Kukikwa na tume huru ya uchaguzi na wapiga kura wakiwa ni watu wenye akili timamu tu huwezi kushika hata nafasi ya 900.
 
Back
Top Bottom