Huduma nzuri sana kwa wateja lakini kwa upande mwingine sio salama kwa Tigo.
USSD application hazimpi mtu utundu na udadisi wa kutaka kujua kinachoendelea kwa sababu zinakuwa serverside na mtumiaji anazitumia kupitia simu yake lakini package inakuwa ipo kwenye mtandao.
Kwa upande wa smart phone apps kama hiyo ya Tigo pesa unakuta mtu anainstall kwenye simu yake na una uwezo wa kupata APK ya app hiyo na kinachofuata ni kufanya reverse engineering na kujua kinachoendelea nyuma ya kapeti. Hii ni risky sana.
Jana nimedown hiyo APK then nikajitahidi mpaka nikapata Java source code zote na kuanza kujifunza jinsi inavyofanya kazi. Ukikuta mtu mwenye nia mbaya na tigo anaweza kumodify source code na kuleta balaa. Ukicheza na variable zilizotumika kuna uwezekano wa kuzibadilisha zikawa static variable mfano kwenye fee ya kutuma pesa ukaweka 0 ukawa unatuma pesa bila makato, unaweza ukacheza nayo ukabadili namba ya receiver ikawa namba yako kwa hiyo watu wakituma pesa zinaingia kwenye simu yako. Just imagine ufanye modification ya namna hiyo halafu uinstall hiyo application kwenye simu za wenzako wasiojua yani utakuwa unaingiza pesa huku umekaa!
Kwa haraka haraka hii ni app nzuri sana na ina security ya hali ya juu especially pale inapofanya connection na bank. Zile connection zote zimekuwa secured (SSL) pia nimegundua hata kama ukifanya modification bado utahitaji valid certificates ambazo zinatakiwa ili ku-establish secure connection.
Kazi nzuri Tigo