Johnsecond
JF-Expert Member
- May 4, 2010
- 1,076
- 211
Nimetaja CCM kwa sababu jana nilikaa na askari polisi pale ubungo kwenye vurugu ambaye alikuwa analalamika kuwa ucheleweshaji wa matokeo unasababisha vurugu lakini wa kulaumiwa ni NEC. Na walikuwa wanaongea na sisi kwa upendo kabisaa na hata kusema kuwa na wenyewe wamepiga kura pia na wamewachagua viongozi wanaowataka hivyo kitendo hicho kilikuwa kinawatia hasira na wao pia. Na nikiangalia kote ambako vurugu zilitokea polisi walitumia mabomu laini ya machozi hawakutumia nguvu zaidi. Nadhani huo ni mwanzo mzuri mageuzi yanakuja na polisi wanachoshwa na system mbovu maana madhara wanayapata na wenyewe mitaani.