Watanzania lazima tujifunze kuappreciate vitu vinavyostahili appreciation.
Mtu akifanya jambo zuri, hata kama ni mpinzani wako, kaza roho umpongeze.
Chadema ni watani wangu wa jadi. Katika historia yangu nimeshawahi kuwapongeza, lakini sijawahi kuanzisha thread ya kuwapongeza.
Leo ninawapongeza.
Kufutia hali ya mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda, kumekuwa na hali tete kisiasa.
Chadema kama chama cha upinzani kimeonyesha kwa kiasi kikubwa kutambua umuhimu wa kuwa makini katika swala hilo. Kitendo cha Katibu Mkuu wa Chadema, kwa utashi wake binafsi usiokuwa na uhusiano na maamuzi ya kikao chochote cha chama, kupinga maamuzi ya Tanzania na kutetea kejeli kwa nchi yetu toka Rwanda kumepingwa vikali na wanachama wa Chadema. Hii ni dalili nzuri na inastahili pongezi.
Kama tutaendelea kuweka mbele maslahi ya taifa na tofauti za kiitikadi za kisiasa na nyinginezo pembeni basi hakuna kitakachotuzuia kupiga hatua zaidi za maendeleo.
Nimefurahishwa na kitendo cha vijana wa Chadema kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu wa kuendesha operation maalum ya kuondoa wahamiaji HARAMU wanaofanya watanzania wasiendelee na shughuli zao za kila siku kwa amani.
Cha kufurahisha zaidi ni kwamba vijana wa Chadema wamesimama kidete kuwakemea wanaharakati (hasa wale wanaoishi nje ya Tanzania) wanaokejeli jitihada za Rais katika kuhakikisha wakazi wa mkoa wa Kagera, Kigoma na Geita hawapati bughudha.
Hii ndio Tanzania tunayoitaka, ya watu wanaojua wanachokitaka na kukipigania bila kujali itikadi zao. Wote tuendelee kupigania jambo moja - Tanzania iwe sehemu bora zaidi kuishi.
Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania...