Nawapongeza CHADEMA

Nawapongeza CHADEMA

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,276
Reaction score
7,691
Watanzania lazima tujifunze kuappreciate vitu vinavyostahili appreciation.

Mtu akifanya jambo zuri, hata kama ni mpinzani wako, kaza roho umpongeze.

Chadema ni watani wangu wa jadi. Katika historia yangu nimeshawahi kuwapongeza, lakini sijawahi kuanzisha thread ya kuwapongeza.

Leo ninawapongeza.

Kufutia hali ya mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda, kumekuwa na hali tete kisiasa.

Chadema kama chama cha upinzani kimeonyesha kwa kiasi kikubwa kutambua umuhimu wa kuwa makini katika swala hilo. Kitendo cha Katibu Mkuu wa Chadema, kwa utashi wake binafsi usiokuwa na uhusiano na maamuzi ya kikao chochote cha chama, kupinga maamuzi ya Tanzania na kutetea kejeli kwa nchi yetu toka Rwanda kumepingwa vikali na wanachama wa Chadema. Hii ni dalili nzuri na inastahili pongezi.

Kama tutaendelea kuweka mbele maslahi ya taifa na tofauti za kiitikadi za kisiasa na nyinginezo pembeni basi hakuna kitakachotuzuia kupiga hatua zaidi za maendeleo.

Nimefurahishwa na kitendo cha vijana wa Chadema kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu wa kuendesha operation maalum ya kuondoa wahamiaji HARAMU wanaofanya watanzania wasiendelee na shughuli zao za kila siku kwa amani.

Cha kufurahisha zaidi ni kwamba vijana wa Chadema wamesimama kidete kuwakemea wanaharakati (hasa wale wanaoishi nje ya Tanzania) wanaokejeli jitihada za Rais katika kuhakikisha wakazi wa mkoa wa Kagera, Kigoma na Geita hawapati bughudha.

Hii ndio Tanzania tunayoitaka, ya watu wanaojua wanachokitaka na kukipigania bila kujali itikadi zao. Wote tuendelee kupigania jambo moja - Tanzania iwe sehemu bora zaidi kuishi.

Mungu Ibariki Afrika,

Mungu Ibariki Tanzania...

Updates:::::
Kuna watu wanadhani upinzani maana yake ni kupinga kila kitu. Hata ukiwapongeza wanapinga!!!

Jamani, upinzani sio kupinga kila kitu...
 
....tanzania bora bila kujali itikadi. Sawa tumekusikia.

Ushauri wa bure ni kwamba endelea kupigania tanzania na utanzania siyo uchama na uchumia tumbo
 
Mimi naomba unitoe kwenye sifa za kijinga!
Wahamiaji haramu ni wanaofanya matendo yasiyokuwa na chembe ya huruma kwa wananchi wa Tanzania....yaani wanaosema wapigwe tu na wanaopiga tu (kama mercenaries)....!
 
Asante sana kwa ushauri...
 
Mimi naomba unitoe kwenye sifa za kijinga!
Wahamiaji haramu ni wanaofanya matendo yasiyokuwa na chembe ya huruma kwa wananchi wa Tanzania....yaani wanaosema wapigwe tu na wanaopiga tu (kama mercenaries)....!

Hii thread ni ya kuwapongeza wanachama wa Chadema. Kwani wewe ni Chadema?
 
hicho kikao cha hao vijana kilifanyika ukumbi gani mkuu ?

Mkuu,

Hongera sana kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa lako na kuunga mkono jitihada za kuhakikisha watu wetu wanaendelea kuwa salama.
 
Ila kwenye hili na mimi yanipasa nijikaze kisabuni na niwape hongera vijana wa CHADEMA (makamanda) kwa kumuunga mkono mhe rais Kikwete kwa ushauri wake kwa Kagame, ni jambo la kupongezwa kwani tumeonyesha umoja wetu na mshikamano kama taifa yanapokuja mambo ya mahusiano ya kimataifa.
 
Watanzania lazima tujifunze kuappreciate vitu vinavyostahili appreciation.

Mtu akifanya jambo zuri, hata kama ni mpinzani wako, kaza roho umpongeze.

Chadema ni watani wangu wa jadi. Katika historia yangu nimeshawahi kuwapongeza, lakini sijawahi kuanzisha thread ya kuwapongeza.

Leo ninawapongeza.

Kufutia hali ya mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda, kumekuwa na hali tete kisiasa.

Chadema kama chama cha upinzani kimeonyesha kwa kiasi kikubwa kutambua umuhimu wa kuwa makini katika swala hilo. Kitendo cha Katibu Mkuu wa Chadema, kwa utashi wake binafsi usiokuwa na uhusiano na maamuzi ya kikao chochote cha chama, kupinga maamuzi ya Tanzania na kutetea kejeli kwa nchi yetu toka Rwanda kumepingwa vikali na wanachama wa Chadema. Hii ni dalili nzuri na inastahili pongezi.

Kama tutaendelea kuweka mbele maslahi ya taifa na tofauti za kiitikadi za kisiasa na nyinginezo pembeni basi hakuna kitakachotuzuia kupiga hatua zaidi za maendeleo.

Nimefurahishwa na kitendo cha vijana wa Chadema kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu wa kuendesha operation maalum ya kuondoa wahamiaji HARAMU wanaofanya watanzania wasiendelee na shughuli zao za kila siku kwa amani.

Cha kufurahisha zaidi ni kwamba vijana wa Chadema wamesimama kidete kuwakemea wanaharakati (hasa wale wanaoishi nje ya Tanzania) wanaokejeli jitihada za Rais katika kuhakikisha wakazi wa mkoa wa Kagera, Kigoma na Geita hawapati bughudha.

Hii ndio Tanzania tunayoitaka, ya watu wanaojua wanachokitaka na kukipigania bila kujali itikadi zao. Wote tuendelee kupigania jambo moja - Tanzania iwe sehemu bora zaidi kuishi.

Mungu Ibariki Afrika,

Mungu Ibariki Tanzania...

Leo ndio nimejua kwamba maccm yako radhi kwa lolote, ali mradi Dr Slaa Katibu mkuu wa CHADEMA Taifa(Rais ajaye wa 2015) anafanyiwa hujuma zozote na hila chafu. Unaonekana kiwango chako cha unafki kiko juu sana, nakushauri ufanye toba
 
Mie nawapongeza wanyarwanda waliotangaza kutowafukuza watanzania wanaoishi nchini mwao. Nadhani wametumia hekima zaidi. Sio vyema kwahukumu wanyarwanda wote kuwa ni wahalifu, nadhani wapo wengine ambao hawakuwa na tatizo. Ni vizuri Vyombo vya ulinzi vingejipanga ili kukamata wahalifu pamoja na mafisadi wanaotuletea sifa mbaya. Mfano mzuri ni huu wa Raisi wetu kutangaza kuwa anayo majina ya wauza unga!, mbona awachukulii hatua?, wengine wanatajwa hadharani kila kukicha akiwemo mwanae na wabunge wake. Yanamwisho haya.
 
Mkuu na mimi nakuunga mkono pamoja na kuwa najua baadhi ya viongozi wa chadema hasa wa lio nje wamecukizwa na kitendo hicho na mmojawapo ni Dr Alex Paurine ambaye ni mnyarwanda pure 100%
 
Ila kwenye hili na mimi yanipasa nijikaze kisabuni na niwape hongera vijana wa CHADEMA (makamanda) kwa kumuunga mkono mhe rais Kikwete kwa ushauri wake kwa Kagame, ni jambo la kupongezwa kwani tumeonyesha umoja wetu na mshikamano kama taifa yanapokuja mambo ya mahusiano ya kimataifa.

Ningeshangaa sana kama usingejiinua dogo, nilikuwa nasubiri udandie tu hii hoja. Atajwe Dr Slaa tena kwa ubaya alafu usichangie? Si rahisi
 
hicho kikao cha hao vijana kilifanyika ukumbi gani mkuu ?

Naisi ni wale wanyiramba 38 waliofanya mkutano na mwingulu... kwenye ukumbi wa watu 250 wakaja hao tu. ( mwenye picha pls nikumbushe kidogo)
 
Ila kwenye hili na mimi yanipasa nijikaze kisabuni na niwape hongera vijana wa CHADEMA (makamanda) kwa kumuunga mkono mhe rais Kikwete kwa ushauri wake kwa Kagame, ni jambo la kupongezwa kwani tumeonyesha umoja wetu na mshikamano kama taifa yanapokuja mambo ya mahusiano ya kimataifa.

Mkuu,

Nikiona vijana wanaungana kupigania maslahi ya taifa huwa naona vijana wetu wamekomaa kisiasa.

Wapo wachache ambao bado hawajakomaa lakini hata maembe hayawezi kukomaa yote kwa pamoja mtini.
 
Mkuu na mimi nakuunga mkono pamoja na kuwa najua baadhi ya viongozi wa chadema hasa wa lio nje wamecukizwa na kitendo hicho na mmojawapo ni Dr Alex Paurine ambaye ni mnyarwanda pure 100%

Hivi huyu jamaa bado anaexist, mimi nilishasahau kama duniani kuna mtu kama yeye!!!
 
Mkuu na mimi nakuunga mkono pamoja na kuwa najua baadhi ya viongozi wa chadema hasa wa lio nje wamecukizwa na kitendo hicho na mmojawapo ni Dr Alex Paurine ambaye ni mnyarwanda pure 100%
Vipi unamchukia Dr kwa vile alikushauri ukatibiwe ugonjwa wako wa akili? Pole sana! sasa huko Uingereza hujisikii aibu kuhusishwa na unyama waliofanyiwa wale mabinti kule Zanzibar?
 
Back
Top Bottom